Nimepigiwa simu jioni hii, dakika kadha zilizopita kuwa Mwanajamvi mwenzetu anayekwenda kwa ID ya wasaimon amefariki dunia muda kama dakika 45 zilizopita, katika hospitali ya Selian hapa Arusha, na sasa hivi ndiyo anaingizwa chumba cha ubaridi.
:A S cry::A S cry:
Taarifa hizo zinasema kuwa amenguka akiwa katika harakati za kuonana na Daktari, akiwa amesindikizwa na baba yake mzazi.
Wasaimon alijiunga na jamvi 6.10.2010.
Binafsi nilikuwa nafahamiana sana na wasaimon, alikuwa ni mtu wa kutoa ushauri wa hekima sana kuhusiana na maisha ya miaka hii, na alikuwa mpiganaji asiyechoka, akitumikia kampuni mojawapo ya Tours mjini Arusha. Naelekea msibani, nitawajuza kinachojiri.
wasaimon alivinjari hapa majukwaani hadi juzi 14.01.2012, na naambiwa kuwa hadi jana alikuwa mzima wa afya.
Ameacha Mke na watoto 3.
Mungu Ilaze Roho ya Marehemu wasaimon Mahala Pema Peponi.

Daaaah msiba mzito sana umetupata JF hasa Arusha. Mkuu itabidi tutafutane.
Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe