Mchungaji amchumbia mjane kwenye mazishi ya mumewe

Mchungaji amchumbia mjane kwenye mazishi ya mumewe

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,039
Wakuu hii kitaalamu imekaaje?

Mchungaji mmoja alimchumbia mjane kwenye mazishi ya mume wake, naye akakubali. Tukio hili lililotokea katika mazishi nchini Afrika Kusini, limezua mijadala na ukosoaji kwa kuhisiwa kutojali na kukosa heshima kwa marehemu.

Soma pia: Mahakama yaamuru kupigwa mnada nyumba ya mjane ili kumfidia aliyeumia mguu kwa ajali ya bodaboda



Tukio hilo lililotokea wakati wa ibada ya mazishi iliyoongozwa na mchungaji huyo, iliyohusisha kumchumbia mjane huyo ambaye naye alikubali ombi lake.

Kitendo hiki kimelaaniwa pakubwa kuwa hakifai na wengi wametilia shaka muda wa ishara hiyo ya kimapenzi kwenye mazishi, huku mumewe akiwa bado hajazikwa.
 
Wameshindwa kuficha mahaba yao,hao wanfurahia kifo cha huyo jamaa
 
Uyo mchungaji tayar alikuwa anapakua kitambo sana
 
Back
Top Bottom