Tanzia: Mwanajamvi afariki Dunia.

Tanzia: Mwanajamvi afariki Dunia.

Poleni sana wana-JF, poleni sana ndugu na jamaa....RIP Wasaimon

Tunakushukuru sana PakaJimmy kwa uwakilishi............
 
Last edited by a moderator:
Mod embu tuwekeeni comment zake kama kumkumbuka.Mungu amlaze anapostahili
 
Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Poleni wote wana jf na ndugu wa marehemu
 
Gone so soon Brother ... Poleni sana wana familia, MUNGU awape faraja na nguvu ya uvumilivu!
 
Naogopa kuacha huu uzi bila maneno yenye kuonesha hisia nilizonazo dhidi ya tatizo hili! Pumzika salama uendako KAMANDA.
 
PakaJimmy, Asante kwa taarifa ya msiba wa mwana JF mwenzetu. Nina swali moja dogo, pamoja na kwamba mwenzetu ametangulia mbele ya haki bado tuna sababu ya kuficha jina lake halisi? Kwa nini usimtaje tu kwa jina lake? Nakumbuka kuna mwana jamvi mmoja alifariki mwaka juzi tulifahamishwa kifo chake na jina lake halisi lilitajwa. Lakini kama una sababu za msingi za kutotaja jina lake halisi, basi ibaki kama ilivyo. Kuna watu wawili watatu hapa JF wanajua jina langu halisi. Siku nikatagulia mbele ya haki, nilishawaruhusu kutangaza kifo changu na kutaja jina langu halisi. RIP Kamanda Waisamon!!! Tiba
 
Raha ya milele umpe ee Bwana, mwanga wa milele umwangazie, Apumzike kwa amani.
 
Nimepigiwa simu jioni hii, dakika kadha zilizopita kuwa Mwanajamvi mwenzetu anayekwenda kwa ID ya wasaimon amefariki dunia muda kama dakika 45 zilizopita, katika hospitali ya Selian hapa Arusha, na sasa hivi ndiyo anaingizwa chumba cha ubaridi.
:A S cry::A S cry:

Taarifa hizo zinasema kuwa amenguka akiwa katika harakati za kuonana na Daktari, akiwa amesindikizwa na baba yake mzazi.

Wasaimon alijiunga na jamvi 6.10.2010.

Binafsi nilikuwa nafahamiana sana na wasaimon, alikuwa ni mtu wa kutoa ushauri wa hekima sana kuhusiana na maisha ya miaka hii, na alikuwa mpiganaji asiyechoka, akitumikia kampuni mojawapo ya Tours mjini Arusha. Naelekea msibani, nitawajuza kinachojiri.
wasaimon alivinjari hapa majukwaani hadi juzi 14.01.2012, na naambiwa kuwa hadi jana alikuwa mzima wa afya.
Ameacha Mke na watoto 3.

Mungu Ilaze Roho ya Marehemu wasaimon Mahala Pema Peponi.

Pole kwa wafiwa R. I. P.
 
Pole kwa wafiwa,pole kwa wana JF.Bwana alitoa na Bwana ametwaa,jina lake lihimidiwe!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Poleni wafiwa. Hii ni habari ya kuhuzunisha sana.
Pakajimmy asante mkuu. Endelea kutupa updates
 
Back
Top Bottom