Tanzia: Mwanajamvi afariki Dunia.

PakaJimmy, jana nimekusoma sikujua kama ni Saimon, sitaki kuamini kabisa,uwiiiiiii. juzi asubuhi nilikuwa ofisini kwake tukanywa na chai, jana jioni napigiwa simu Sai ametutoka, haki ya nani nimechoka kabisa.
 
PakaJimmy, jana nimekusoma sikujua kama ni Saimon, sitaki kuamini kabisa,uwiiiiiii. juzi asubuhi nilikuwa ofisini kwake tukanywa na chai, jana jioni napigiwa simu Sai ametutoka, haki ya nani nimechoka kabisa.
nI MWENYEWE KABISA...
Kumbe ulikuwa unamfahamu?
 
rip wasaimon, usamehewe makosa yako kwa HURUMA YAKE MUUMBA WETU, akupumzishe kwa amani, AMEN!
 
R.i.p wasaimon!
Safari yetu wote ni moja,ila tunapishana tu!
Pole cna familia yake ya Baba/Mama/Mke na Watoto
 
nI MWENYEWE KABISA...
Kumbe ulikuwa unamfahamu?

PakaJimmy, bro wangu wacha tu, sitaki kuamini kama baba tony hayupo, hilo sitaliamini mpaka nimuone mara ya mwisho, hiyo juzi alinical alikuwa na shida fulani na me, nilikuwa EAC ikawa karibu kufika ofisini kwake, ndio nikamkuta anakunywa chai na mie nikaunga, tukaongea weee, leo saa tano ndio tulikuwa tuonane kwa ajili ya hiyo ishu tuliyoiongelea, wacha tu, shock niliyoipata jana sijui niielezee vipi, vizuri vinakwenda, yaani Sai alivyokuwa mtu wa watu/roho nzuri/kusaidia watu basi tu,nimelia nimechoka.
 

Pole dadaangu. Hata mimi unipe pole maana amekuwa mtu wangu wa karibu mno, isingewezekana zipite cku 3hatujawasiliana. alikuwa na mipango mingi mno ya future kiasi nahofia kama wife wake anaijua yote.
Umeshasikia kuwa mazishi ni Jumamosi?
RIP BRODA WASAIMN.
 



UPDATE1.
Mpaka sasa hivi (0940am)wanasubiriwa Baba zake wakubwa na wadogo ili wafanye kikao cha maamuzi ya mahala pa kuzika(kuna option mbili, kuzika Arusha au Kusafirisha kwenda kwao Mbeya).
Pia aliyekuwa Mwajiri wake yuko njiani tokea Nairobi, anakuja kusaidiana na familia kupanga hatima ya marehemu.
​







UPDATE 2.
MAZISHI NI KESHO-KUTWA JUMAMOSI HAPAHAPA ARUSHA,NADHANI KWENYE PUBLIC CEMETRY NJIRO. MTAKAOWEZA TAFADHALI TUWE PAMOJA SIKU HIYO.[/QUOTE]

samahani sijaweza kusoma post zote ili nijue kama ulishaelekeza msiba ulipo! ni kijenge maeneo gani PakaJimmy!
 
Last edited by a moderator:

pole sana Bro wangu,nimeenda mchana msibani but nikashidwa kabisa kuingia nikaishia bondeni bar huku, nilisikia watu wakisema ni jmosi but sikuuliza wapi coz nilijua nitajua tu kwa namna yoyote ile, kuhusu mama Tony ndio alinifanya nikashindwa kuingia mana naambiwa akiingia mtu anaemjua inakuwa balaa, sina cha kusema kuhusu mama Tony,Mungu ampe nguvu/ujasiri, siwezi kusema sijui ataanzia wapi Mungu mwenyewe ana makusudi yake, roho inaniuma zaidi kwa Tony, alivyopambana kumtafutiaa shule nyingine ili amtoe kata, amepata hajapelekwa Sai kaondoka, yaani my bro, imeniuma sana sana sana, sina maelezo kabisa, na jana mida ya saa 4 nilikuwa kwenye kikao nikakuta missed call yake nikajua ananikumbushia kumtafuta huyo mtu tuliekuwa tuna shida nae leo so sikupiga nikijua nimeshamaliza hiyo ishu ni suala la kukutana, laiti ningemcal niongee nae ya mwisho., R.I.P my Bro Sai, sijui kama nitamsahau kirahisi, nikipata shida najua nina wa kumtafuta chap na nikatatuliwa chap, Mungu anajua kwanini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…