Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,111
- 2,743
Mmiliki wa Hoteli ya kifahari mjini Mtwara (NAF) Ndg. Shebby amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko India alikoenda kutibiwa kutokana na maradhi ya moyo. Waliokuwa karibu na Ndg. Shebby wanadai kwamba siku za hapa karibuni bwana Shebby alikuwa na msongo wa mawazo akilalamika madeni kuongezeka kutokana na kukosa wateja katika biashara yake ya hoteli.
Hoteli nyingi Mtwara zilitegemea sana wageni katika makampuni ya gesi ambapo tangu mwaka jana wameondoka nchini na kurudi makwao.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
Amina.
==================
Habari Zaidi

Mtoa huu Uzi analeta siasa, huyu jamaa ni kweli kafariki lakini, hakufia INDIA, amefia hosptali ya mkoa SOKOINE LINDI.
Amepelekwa juzi usiku baada ya kujisikia vibaya na jana saa 12 asubuhi akaitikia wito wa muumba, RIP BRO SHEBBY!