TANZIA: Mmiliki wa NAF Hotel Mtwara afariki dunia

Mungu ailaze mahala pema Peponi roho ya marehemu... Sisi kama nchi tumepata pigo kwa kuondokewa na muwekezaji ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwenye kutoa ajira, kulipia kodi na kubadilisha mandhari ya 'jiji' la Mtwara...
 
Kuna mwingine hapa kwetu alikunywa sumu kwa ajili ya madeni.

Vifo vya magonjwa ya moyo na stress vitaongezeka zaidi awamu hii kuliko vifo vya magonjwa ya kuambukiza.
 
Binafsi hii hotel nilishafika pale mara mbili. Kuna Band huwa inapiga live pale inaitwa NAF BAND. Kwa maelezo ya mtoa mada huyo aliyefariki hawezi kuwa mmiliki wa hiyo hoteli. NAF BAND wakiwa wanapiga mwanzo mwisho wanamsifia aliyekuwa mbunge wa mtama. Ndipo nilipouliza kumbe ndio mmiliki wa NAF HOTEL
 
Siasa kwenye kila kitu! Taarifa ya msiba alafu inapigwa na polish ya "masimango" ya kisiasa kwa mbaaali ....Ama kweli uchawi una maana pana sana ..
Hiyo sio siasa bali ameeleza kisababishi cha kifo mkuu
 
Mmiliki wa Hoteli ya Kifahari mjini Mtwara (NAF) Ndg. Shebby amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko India alikoenda kutibiwa kutokana na maradhi ya moyo. Walio kuwa karibu na Ndg. Shebby wanadai kwamba siku za hapa karibuni.

Bwana Shebby alikuwa na msongo wa mawazo akilalamika madeni kuongezeka kutokana na kukosa wateja katika biashara yake ya hoteli.

Hoteli nyingi Mtwara zilitegemea sana wageni katika makampuni ya gesi ambao tangu mwaka jana wameondoka nchini na kuridi makwao.

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.

Amina..
Kwa mwendo huu tutapoteza wengi sana, RIP Mr Shaby
 
Back
Top Bottom