Tanzia: Ezekiel Malongo wa TBC afariki dunia

Tanzia: Ezekiel Malongo wa TBC afariki dunia

Maziko yake yalifanyika Simanjiro.
Nilishuhudia. Apumzike kwa amani.
 
TBC kuna nini, watangazaji 3 kukata kamba ndani ya miezi miwili!!!?

Mmmmmh, however R.I.P Ezekiel Malongo!
 
Naona kuna wingu zito kwa waandishi wa habari...inaonekana kama msimu wao... nimeshaona wasanii wanafuatana katika vifo, au wanasiasa au taasifu nyinginezo... ila sijui kwanini inatokea hivi???? Sijapata jibu bado!!!!

Poleni wafiwa!!
 
Rip.
Msiulize Tbc kuna nini. Ni kwasababu kile ni chombo cha habari hivyo kila member wao anaefariki lazima atangazwe. Wengi wanafariki TRA,TANESCO,Mawizarani nk lakini hamuwasikii sababu hawatangazwi. Simple idea!
Uko sawa mkuu binadamu huwa wana tabia ya kushangaa kifo kinapotokea sehemu flani na kusahau vifo vinavyotokea kila siku kwenye familia zetu na majiran zetu na sehemu nyingine! kifo ni kifo hakijalishi uko wapi ndg zangu ka msingi ni kutambua kuwa saa na muda wowote waweza tangulia, polen wafiwa
 
Malaria ni ugonjwa unaotibika, inakuwaje Mwananyamala Hospital wameshindwa kumtibu? ifike mahala vifo vichunguzwe na uzembe ukibainika watu wawajibishwe!!!
 
Heri Yake kamaliza kazi,hakimu mwema atamtendea haki huko aendako.
 
Malaria ni ugonjwa unaotibika, inakuwaje Mwananyamala Hospital wameshindwa kumtibu? ifike mahala vifo vichunguzwe na uzembe ukibainika watu wawajibishwe!!!

mkuu kifo hakitibiwi bali malaria inatibiwa
 
kuna haja AMREF wakaenda pale TBC kufanya utafiti ..haiwezekani watu wanakufa hivi kama panya wamewekewa sumu.. Pumzika wewe Ezekiel Chibulunje Malongo
Tatizo pale wanazunguukana wenyewe kwa wenyewe na bado kwani mnyororo ni mrefu
 
Ila huyu jamaa ni kama alishajikatia tamaa. Mara ya mwisho kumuona sikutaka kuamini kama ni yeye Ezekeil kweli tuliekua tunakaa nae pale MeryLand na akina Rweyunga Deo tunaongea vya kujengana. Mwenzetu kachakaa na kuchoka kalewa ile saa 12 ya asubuhi pale Ubungo standi hajitambui. Anyway RIP my fellow in business
 
Back
Top Bottom