Tanzia: Ezekiel Malongo wa TBC afariki dunia

Tanzia: Ezekiel Malongo wa TBC afariki dunia

Nimesikia kwa mbali juu ya huyu mtangazaji machachali kutokuwa nasi tena sijui kuna ukweli hapo?
 
TBC kuna nini mbona watangazaji wake wanakufa hivyo?? R I P Malongo
 
Jamaa wasifu wake unasema alikuwa mlevi wa kupindukia ndiyo maana hata akatimuliwa TBC.

Na taarifa za Kifo chake Mwananyamala Hospital zinasema alikuwa amewekewa dripu lakini huku alikuwa akipiga kirobo na dripu inateremka.

R.I.P Malongo.
 
Namkumbuka sana jamaa, alipokuwa akitangaza kabumbu enzi zile na kina marehemu halima mchuka(ALLAH akurehemu), Juma Nkamia, evance muhando nk. Malongo alikuwa na utangazaji fulani ambao kama una presha inaweza kupanda ,yani mpira uko katikati lakini anavyotangaza utadhani ndio goli linaingia kimiani....yani hatumwi mtoto dukani aisee!
Poleni wafiwa, tutakumbuka brother, pumzika mahala ulipoandaliwa!
 
R.i.p malongo nilikuwa nakufurahia sana kwenye michezo nilivokuwa mdogo
 
Back
Top Bottom