Askari Polisi Watano, Mahabusu 8 wafariki kwa ajali ya gari Mlima Sekenke, Singida

Askari Polisi Watano, Mahabusu 8 wafariki kwa ajali ya gari Mlima Sekenke, Singida

rafael mkumbos

Senior Member
Joined
Sep 12, 2024
Posts
197
Reaction score
384

Askari na mahabusu wanadaiwa kufariki dunia baada ya gari la polisi walilokuwa wakisafiria kugongwa na lori la mizigo katika eneo la Mlima Sekenke, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea leo majira ya saa 2:00 asubuhi, akisema taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na vikosi vya uokoaji, gari hilo la Polisi lilikuwa na watu 13, wakiwamo mahabusu wanane na askari watano, ambao walikuwa wakisafirisha mahabusu kutoka Kituo cha Polisi Shelui kwenda Mahakama ya Wilaya ya Iramba iliyopo Kiomboi.

Chanzo hicho kimesema ajali hiyo ilitokea baada ya lori la mizigo lililokuwa likisafirisha mafuta ya dizeli kutoka Bandari ya Dar es Salaam kuelekea Rwanda kufeli breki wakati likishuka eneo la Mlima Sekenke na kuligonga gari hilo la Polisi.

Soma Pia: Askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Mbeya wafariki katika ajali ya gari

Taarifa za awali zinaeleza kuwa watu 12 wamefariki dunia katika ajali hiyo, huku wengine wawili wakijeruhiwa na kupelekwa katika Hospitaki ya Wilaya ya Iramba kwa ajili ya matibabu.


1789983792362.png
 

Taarifa nilizopata ni kuwa, kuna ajali imetokea asubuhi ya leo, ikihusisha gari la Polisi na Semi, Mlima wa Sekenke uliopo Iramba, Singida.

Gari la Polisi lilikuwa limebeba Mahabusu na Askari Polisi, likitokea Shelui kwenda Kiomboi.

Askari watano wamefariki papo hapo na mahabusu kadhaa.

View attachment 3675029
inna lillahi wa inna ilahi rajirun 🌹
 
Back
Top Bottom