Ogah hakika mimi sielewi kwanini watu wnakubali hizi spinning za wahamiaji haramu.
Sheria zipo na kutojua sheria hakutoi msamaha kwa mtu.
Mtu ameingia na kuamua kununu au kupora kkiwanja, akazaa watoto kama 'human shield' leo sheria inapomhukumu mhalifu huyo sheria hiyo inageuka kuwa mbaya, very strange!
Kenya wana kitu inaitwa kipande, (piece of ID) kama huna hiyo wewe unalako tu. Sisi tupo katika process eti bado watu wanataka watu 20,000 wahamiaji haramu wapewe vitambulisho ili kuwafurahisha wananchi wa nchi zingine! very strange
Kuzaa watoto si sehemu ya sheria za uhamiaji na aliyekiuka ni mhalifu mkubwa tu.
Kuhamia miaka 20 si sehemu ya uhamiaji kama umezamia, mzamiaji ni mhamaiji haramu tu.
Hatuwezi kuwa wakimbizi ndani ya nchi yetu. Wananchi wa Kagera wameteseka sana. Nimeshuhudia haya.
Ogah watu walionya kuwa kusafiri na mzigo wa maiti kuna Wanyarandwa.
Watu wana maiti wanafikiria kuizika porini kwasababu hali inakuwa mbaya kwasababu tu wahalifu wa Kinyarwanda na nchi za jirani wameamua kuvuna mali kwa mateso ya watanzania, bado tunadhani hawa ni wanadamu wema kabisa.
Inasemwa wazi, kuna wahalifu wa Rwanda wapo na wanatesa watu, leo tunaona kama raia wema. Jamaani!
Kama tutatoa fursa kwasababu wamezaa basi tuachie majambazi yaliyoko magereza kwasababu nayo yana watoto na sheria inatoa msamaha kama kwa wahalifu hawa.
Lazima ifike mahali tuwe na uchungu na taifa letu na watu wetu. Kuwatelekeza wananchi wa Kagera ili kuwafurahisha raia wa kigeni ni moral decay ya hali ya juu. Kwanini mtu wa Kagera aishi kwa mashaka na hofu kwa katiba ya JMT, wakati huo huo sheria zinazotokana na katiba hiyo zimtetee mhalifu. Please!
Kwanza walitakiwa wafikishwe mahakamani kama wasomali na waethipoia, baada ya hapo kwao.
Eti mhalifu anadai hakupewa nafasi ya kuaga nyumbani, wakati anakuja kwa njia za panya alipiga hodi.
Kibaya zaidi wao wamegeuza hii issue na kuwa Wanyarwanda, hali warundi, wakongo n.k. wameondolewa pia.
Sasa wanaipaka matope Tanzania kwa neno target Watusi, hivi hawa wana jema na nchi yetu kweli.
Tuache tu wawe makanali na wakuu wa majeshi kwasababu sisi ni watu wema sana kwa majirani zetu! please please.
Sheria ifanye kazi, kama kuna aliyesalimika naye ichukue mkondo wake lakini hakuna sheria inayotoa msamaha kwasababu mbona fulani hajahukumiwa! hakuna sheria inayotoa msamaha kwa kutoijua.