Nzuri tu, Mkuu. Slightly disappointed na hali ya jamvi niliyoikuta.
Pamoja na wewe kudai kuwa si mbaguzi, maneno yako yanakusuta. Kuishi na watu wengi hakukuondolei hiyo sumu ya kibaguzi kama unayo. Hata wakina Rush Limbaugh wakibanwa wanasema wana marafiki wengi weusi.
Unataka kujua ni sheria gani ya kimataifa imevunjwa na hili zoezi? Ni ile inayosema kuwa mtuhumiwa yeyote atapewa nafasi ya kujitetea dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake mbele ya chombo chenye dhamana ya kutenda haki. Chombo hiki ni mahakama na si Afisa Uhamiaji, polisi au mtendaji wa kijiji. Ukiondoa banana republic (ambako mnataka kutupeleka) , wale ambao wanashukiwa kuishi nchini nje ya utaratibu wanapelekwa Mahakamani ambako wanapata nafasi ya kujitetea. Ni Mahakama ndio inayowatamka kuwa Wahamiaji haramu na si vigilantes waliojaa wivu. Mbona Jenerali Ulimwengu aliposhukiwa kuwa ni mhamiaji haramu hakuswagwa kwenye lori na kupewa siku 14 awe nje ya nchi? Au haki na taratibu zinafuatwa kwa wale wenye uwezo tu?
Unatuambia kuwa ushahidi uliowazi ni kuwa majambazi wengi huko mipakani ni wanyarwanda. Ushahidi huo ni matamshi ya wenyeji wa huko ambao bila shaka watakuwa wepesi kuwahukumu wageni kuliko ndugu zao. Mara ngapi humu ndani tumekazania kuwahukumu wahindi na kusahau ushiriki mkubwa wa wazawa wenzetu? Rafiki yangu, Ogah nae ni kama wewe. Amejaa xenophobia na racism. Huyu rafiki yangu anatusimulia jinsi alivyopambana na wasomali wahamiaji haramu bila kutueleza alipata wapi muda wakati wakirushiana risasi wa kuuliza pasi zao, vitambulisho vyao n.k. Kwake yeye msomali yeyote ni mhamiaji haramu, conveniently akiwasahau wakina Rage ambao wako humu kwa miongo mingi na ni watanzania kama yeye!
Kuna mmarekani maarufu mmoja kwa jina alikuwa akiitwa William Bennet ambae alisema kama watoto wote weusi wakiwa aborted nchini mwake, uhalifu utashuka sana. Na sisi tumefikia hapo, kwa kuamini kuwa wanyarwanda wote wakitimuliwa basi nchi yetu itageuka paradiso tukisahau kuwa bado tutaendelea kuua maalbino, kuwapiga nondo bibi vizee, kuwasachi majeruhi wa ajali, kubeba unga, kuvamia mabenki n.k. Kama kuna muovu mnyarwandwa akamatwe, apelekwe mahakamani na akipatikana na hatia ahukumiwe kama binadamu mwingine. Hii kuhukumu jamii nzima kutokana na maneno na imani ya baadhi yetu kutatutokea puani. Baada ya wanyarwanda tutawageukia wachaga n.k. ambao wote tunajua ni majambazi sugu. Msitupeleke huko Amandla......
Mkuu
Fundi Mchundo timbwili hili lilipoanza nimesimama katika point yako muhimu ya sheria.Nimesema alichokifanya JK ni sahihi lakini nimemlaumu kwa kutochukua sheria.
Hawa watu walitakiwa mahakamani kama ulivyosema na nilivyowahi kusema nyuzi zaidi ya 10.
Ikithibitika ni mhamiaji haramu hapo hakuna msamaha ni kifungo na baadaE kurudi alipotoka bila kupewa fursa ya kubeba sanduku. Hakuna suala la mimba wala mtoto kwasababu hayo hayapo katika sheria za uhamiaji.
Mtoto na mimba au mke watabaki na haki zao wakati mhalifu anaswagwa.Nakubaliana nawe na ndilo kosa lililofanyika.
Nina wasi wasi kuhusu maelezo yako na suala la ubinadamu. Sijui wangepatikana na hatia na kufungwa ungesemaje.
Endapo wameambiwa warudi makwao inaonekana hakuna ubinadamu, je mbele ya mahakama wakatiwa hatiani hapo sijui ingekuwaje.Kuna kujichanganya huku ubinadamu ukitangulia sheria sehemu fulani, sehemu nyingine sheria ikitangulia ubinadamu. Naelewa ni katika jitihada za kuwatetea kwahiyo kila taulo litatupwa katika ulingo.
Pili, wananchi wanaolalamika kuhusu ujambazi wa Wanyarwanda hawana chuki, wapo nchini mwao chuki iyoke wapi.
Mbona hawasemi Waganda au Wakongo?Viongozi kama Zitto wamewahi kuomba serikali iingilie kati hali usalama sijui nalo una maoni gani.
Ujambazi uponchini, kuna wakati majambazi wa Kenya walichachamaa hadi walipouawa 7 hali ikatulia.
Walisemwa kama Wakenya na hakuna aliyesema ni xenophobia.
Wasomali wahamiaji haramu waliua OC-CID Arusha, wakatandikwa kwa Helicopter leo wananchi wapo salama.
Vipi ionekane xenophobia na racism tukisema Wanyarwanda? Wao wenyewe wanakiri kwanini sisi tukatae.
Nime clarify kuwa hakuna tatizo la raia kuishi nchini provided anaishi kwa njia halali. Nikatoa mfano wa wamakonde, wamakua, wawemba, wajaluo, wadigo na wabondei(home) n.k. Je, ukarimu tuuendeleze kiholela ili kuwaburudisha wasiofuata sheria kwasababu wana mbegu za kutosha kuzaa na kujaza mabinti mimba! Basi tufute sheria na idara ya uhamiaji kila atakaye na aje tu, Tanzania ni shamba la bibi.
Kuhusu usalama, hivi huyu unayesema ana watoto anaihtaji uniform za jeshi za nini na machine gun ya nini?
Na kwanini unadhani ni vema wananchi wa Kagera wakaishi kwadhiki, dhalili mateso na mihemuko ili kuwafurahisha wahamiaji haramu ?
Na kwanini unakubaliana na wapiga propaganda kuwa wahamiaji haramu ni watutsi. Tulipopokea wakimbizi waliokuwa wanafyekana vichwa huko Rwanda, tuliwabagua kwa Ututsi na Uhutu. Hivi huoni spinning za hawa jamaa unaowatetea ni hatari za kipuuzi kitoto na kiwendawzimu. Nani atasimama kuitetea Tanzania kama si mimi na wewe. Yaani tumefika mahali tunatoa pass kwa watoa kashfa kama hawa ili tu tuwaridhishe waendelee kuua watu wetu Kigoma na Kagera! real mkuu
Unaposema mimi na Ogah tuna xenophobia na racism kwakweli hututendei haki. Binafsi ni critic mkubwa wa serikali ya JK na niko disappointed sana hata kudhani ana miaka miwili zaidi. Lakini hilo halinifanyi nisisimame kwatika kile ninachoona ni sahihi na kina ukweli.
Tofuati iliyopo ni kuwa kusimama kwa ajili ya wananchi wa Kigoma, Kagera na Geita mimi nasema ni uzalendo.
Kusimamia sheria mimi nasema ni jambo jema. Kuwatetea wahamiaji haram wewe unasema ni uzalendo, kwanini basi useme nina xenophobia na racism kwa kusimama katika kile ninachoamini kuwa ni sahihi kwa mtazamo wangu?
Je, ungeshauri niunge mkono wahamiaji haramu amabao ni wahalifu wakubwa to begin with ili ni qualify katika uzalendo. Ndivyo unamaanisha mkuu na huoni unaninyima haki yangu ya freedom of speech and expression without abuse..........