Elizaa
Senior Member
- Oct 19, 2010
- 136
- 46
Kwa kweli hii lodge ni master piece. Ila kwa mtazamo wangu hii siyo property ambayo mtanzania anaweza kujivunia nayo. Tunaweza kusema nchi inanufaika kwa mapato kutokana na park fees (kuna wakati huko nyuma kulikuwa na mpango wa kuwatoza wageni wanaokaa kwenye lodge hiyo extra park fees kama USD 500 kwa mtu kwa siku baadala ya USD 50 kwa mtu kwa siku), vinginevyo mimi nakerwa sana kuona mbuga zetu mashuhuri zimetekwa na hao wawekezaji kutoka nje. Kwa mfano, hakuna hata lodge moja ambayo iko kwenye National Park zetu inayomilikiwa na mzawa. Zote ni za hao wazungu, wahindi kupitia Agakhan Foundation na wahindi wengine kutoka Kenya. Kuna zile ambazo serikali ilishindwa kuziendesha nazo ni Lake Manyara National Park, Ngorongoro Wildlife Lodge, Seronera Wildlife Lodge na Lobo WildlifeLodge. Hizi zote ziliuzwa kwa mhindi mmoja anaeitwa Kotak wa GAPCO.! Tatizo kubwa la kiuchumi hapa kwetu ni hiki kisingizio cha Globalization (Ukoloni Mamboleo). Tanzania kuna watu serious ambao wangeweza kuzi run hizo hoteli kama wangewezeshwa kifedha, lakini umasikini wetu unatuhukumu na hizi Funding Institutions au mabenki yaliyozagaa hapa nchini hayana shughuli na watanzania hasa wazawa. Mikopo watapewa watu wenye pesa tu, sisi tutabakia kuwa washangiliaji siku zote tukiona hivi hivi urithi wa maliasili yetu ukibakwa kila kukicha na hao manyan'gau wa nje wakishirikiana na mafisadi wachache kwenye wizara mbali mbali.
Ili tuweze kufaidi rasilimali zetu inabidi tubadilike, Watanzania wengi tumeridhika sana au niseme tunaridhika kwa kupata mlo wa siku nyumba ya kuishi na gari.
Ubinafsi ni tatizo kubwa sana, mtu anaona akipaform vizuri kwenye kazi yake anamfaidisha bosi wake, bila kujua ni kwa faida yake mwenyewe na jamii inayomzunguka.
Watanzania wengi hawapendi kuumiza vichwa vyao, na wakiona mtu anaumiza kichwa ili afanikiwe au afanikishe anachofanya hawafurahii, hii inasababisha wale waliofanikiwa kutokushirikisha watanzania wenzake kwa kuogopa kuharibiwa. Mfano mzuri ni jinsi baadhi ya watanzania wanaoishi nje nchi wanavyosengenyana badala ya kufikiri jinsi ya kuleta maendeleo nnchini mwao, wengi wanaishia kurudi bila hata kuwa na kitu cha kueleweka nyumbani.
Unapofungua biashara yako na ukamuachia mtu aisimamie, huwezi kukuta faida badala yake utakuta madeni, tofauti na mzungu ukimkabidhi biashara yako anajitahidi azalishe faida, maana ni aibu kupata hasara.
Kwa ajili hiyo na ndivyo wazungu wengi wanavyotuangalia. Wanapokuja kuinvest kwetu wanakua tayari na huu mtazamo ndio maana tunaishia kuwa wafagiaji na wabeba mizigo.
Hotel industry needs committed people, its called hospitality industry. Is not a Joke! we need to change and to help our future generation to change. To let them know Job is life, we are not working because we don`t have something to eat or where to sleep, but working is life.
We have to change, we have to accept our weakness and find a way out.