Tanzania yetu ina majasusi wa aina gani?

Status
Not open for further replies.
Tanzania hakuna intelligence, majasusi wala shushushuu. Kuna wahuni ambao kazi zao ni kufuatilia nani anaipinga CCM au serikali ambayo inawapa ulaji. Wengi utawakuta kwa wahindi wakipewa hela.
 
Tafadhali naomba kueleweshwa kwa maneno machache maana ya UJASUSI au tafsiri yake kwa kiingereza niigoogle kuongeza ufahamu wangu, TZ ya zamani maneno kama MAJASUSI na MAFISADI ilikuwa misamiati ila siku zinavyozidi kwenda naona ni kama vyeo flani au wajihi wa mtu..... Thanks.
 
Katika soma soma zangu nimeona jinsi ujasusi wa kiteknolojia na kiuchumi ilivyoisaidia china kufika hapo ilipo. Lakini Nimekuwa najiuliza je serikali yetu ya Tanzani inao majasusi wa aina hii?

Ninahisi bado serikali yetu ime concentrate kwenye ujasusi wa kufatilia maisha ya watu , wizi, ujambazi , na wale wa kuakikisha serikali iliyopo madarakani haipati vikwazo kutoka kwa wananchi wake, etc.

Ingekuwaje kama Serikali ya Tanzani ingepata taarifa mapema za kijasusi ikafanya kila liwezekanalo kile kiwanda cha kukata dahabu kisijengwe Uganda na badala yake kijengwe Tanzania.

Je Kuna majasui wa kichumi wanafuatilia au kujua bajeti za kenya na uganda zitafanya mabadiliko gani yatakoyotahiri upande Tanzania . Ujasusi wa aina hii ni muhimu ili kujipanga na kuwa katika advantage.

nadhani Vision na Mission ya TISS au UWT inatakiwa iwe ya style hii. Kuwachezea faulo kenya na Uganda kwa manufaa ya watanzania sioni kama ni kosa.

Je Tanzania tunao majasusi wa kichumi au kiteknolojia? Je si sawa moja ya wajibu wa mabalozi wetu nje ya nchi kuwa majasusi wetu wa kiuchum?

Nawasilisha

Kusimamia Mambo ya uchaguzi mkuu pia ni wakali sana TISS ; hope na hilo la Tech. wataliongezea kwenye mission yao
 
Tafadhali naomba kueleweshwa kwa maneno machache maana ya UJASUSI au tafsiri yake kwa kiingereza niigoogle kuongeza ufahamu wangu, TZ ya zamani maneno kama MAJASUSI na MAFISADI ilikuwa misamiati ila siku zinavyozidi kwenda naona ni kama vyeo flani au wajihi wa mtu..... Thanks.

UJASUS wa CHINA nadhani umewasaidia kwa kuwa kila mtu anayepewa kazi hiyo anapewa na hadidu rejea na deliverables! Kwetu yumkini yakawepo mambo ya kupeana kazi, ulazi na bila shaka hii inakinzana na dhana ya uadilifu. Kwa mtazamo wa nje ujasusi ni zaidi ya usalama wa taifa, ni pamoja na 'kuiba technolojia' pale inapowezekana, ni pamoja na kujua fursa zilizopo za kiuchumi na kuwajulisha waajiri wako ili muweze kufaidi fursa kama nchi.
 
Majasusi wapo ila kazi zao ni kuonesha vitambulisho vyao wakiwa bar, Beer ikichelewa 'unanijua mimi'??
 
Tafadhali naomba kueleweshwa kwa maneno machache maana ya UJASUSI au tafsiri yake kwa kiingereza niigoogle kuongeza ufahamu wangu, TZ ya zamani maneno kama MAJASUSI na MAFISADI ilikuwa misamiati ila siku zinavyozidi kwenda naona ni kama vyeo flani au wajihi wa mtu..... Thanks.

Angalia maneno yafuatayo kwenye mtandao, Intelligence, Espionage, Spying, military intelligence, industrial espionage, Intelligence agencies. Kama ni msomaji mzuri, utaelewa vizuri nini maana ya ujasusi.

Ila ujue kuwa ujasusi haufanywi nchini mwako, unafanyika kwenye nchi nyingine na majasusi wenu kwa manufaa ya nchi yako. Ndani yako kunakuwepo na watu wa usalama, ambao wao wana kitengo cha counter-intelligence ili kuzuia majasusi wa nje wasikusanye habari zenu.
Uingereza kwa mfano, wana MI6 (British Intelligence agency) ambao ni majasusi, wakati MI6 ni counter intelligence.

Bahati mbaya vitengo vya namna hii hapa bongo vinaajiri viazi, mara nyingi kwa kujuana.
 
Kustudy Uchumi hauhitaji kuwa na jasusi kufanya kazi hizo. Nchi zilizoendelea zinatumia zaidi maprofessor ktk university kufanya research kwenye uchumi.
Nchi kama Marekani, wana institution ambazo zinastudy change on economy, consumer price index, nk. Wasomi wa vyuo vikukuu ndiyo wanaimput information zaidi ktk serikali zilizoendelea.
Serikali ya Marekani inatumia zaid hela ktk R&D research and development ktk vyuo vikuu.
Shule za TZ bado hazina vitu muhimu ktk research and development. Serikali yetu inabidi itumie hela nyingi kuinvest ktk vyuo vikuu.
 
Majasusi wapo ila kazi zao ni kuonesha vitambulisho vyao wakiwa bar, Beer ikichelewa 'unanijua mimi'??

haha haa, inachekesha halafu baadaye inatia huzuni kuwa mtanzania wa karne ya 21 huyo!. Wengi wao ni viwembe wa hali ya juu, halafu wanamtandao wa kueneza moto kwa makusudi. hatari,hatari ni moto wa kuotea mbali! Mungu ibariki Tanzania!
 
Tanzania tuandae vijana ambao wataweza kuchangia maendeleo kwa kutumia vizuri ujasusi kwa maendeleo yetu.
thanx the topic is very useful
 
naomba unisaidie majina ya vitabu vyenye story za kijasusi,maana napenda sana kufuatilia mambo hayo,kuna ambacho nilikisoma kidogo kwa mshkaji lakini sikumbuki jina lake

please assist!
 
Katika soma soma zangu nimeona jinsi ujasusi wa kiteknolojia na kiuchumi ilivyoisaidia china kufika hapo ilipo. Lakini Nimekuwa najiuliza je serikali yetu ya Tanzani inao majasusi wa aina hii?

Ninahisi bado serikali yetu ime concentrate kwenye ujasusi wa kufatilia maisha ya watu , wizi, ujambazi , na wale wa kuakikisha serikali iliyopo madarakani haipati vikwazo kutoka kwa wananchi wake, etc.

Ingekuwaje kama Serikali ya Tanzani ingepata taarifa mapema za kijasusi ikafanya kila liwezekanalo kile kiwanda cha kukata dahabu kisijengwe Uganda na badala yake kijengwe Tanzania.

Je Kuna majasui wa kichumi wanafuatilia au kujua bajeti za kenya na uganda zitafanya mabadiliko gani yatakoyotahiri upande Tanzania . Ujasusi wa aina hii ni muhimu ili kujipanga na kuwa katika advantage.

nadhani Vision na Mission ya TISS au UWT inatakiwa iwe ya style hii. Kuwachezea faulo kenya na Uganda kwa manufaa ya watanzania sioni kama ni kosa.

Je Tanzania tunao majasusi wa kichumi au kiteknolojia? Je si sawa moja ya wajibu wa mabalozi wetu nje ya nchi kuwa majasusi wetu wa kiuchum?

Nawasilisha

Sisi ni kilimo kwanza badala ya kuwekeza kwenye ELIMU Inahitajika tuwe viongozi makini na wazalendo wenye maono ambao ni waelewa kutambua kwamba dunia yetu iko kwenye vita kuu ya uchumi kwa hivi sasa na sio cdm na ccm wageni wamesha ingia kwa nembo ya wawekezaji wanakula bila kunawa
 
naomba unisaidie majina ya vitabu vyenye story za kijasusi,maana napenda sana kufuatilia mambo hayo,kuna ambacho nilikisoma kidogo kwa mshkaji lakini sikumbuki jina lake

please assist!

Tafuta vitabu vya Frederick Forsyth kama vile The Odessa File (chanzo cha neno “desa” pale UDSM), The Day of the Jackal, The Afghan, The Avenger, The Fist of God, The Deceiver and The Devil's Alternative just to mention a few.

Pia kuna mwandishi wa zamani zaidi anaitwa Desmond Bagley naye stories zake zilikuwa kali. Kitabu kimoja ninakikumbuka kilikuwa "Running Blind"
 
tatizo la Tanzania ni Siasa, hiki kitengo kinafanya kazi kwa nguvu ya kisiasa, kinajitahidi sana kukusanya information ambazo ziko creative na zenye maana, lakini maamuzi yanakuja kuwa ya kisiasa zaidi, Huu ni usalama wa Taifa, siwezi kukukubalia kuwa wale wezi Wa EPA walichota fedha pale BOT kuwa hawa jamaa wa UWT walikuwa hawajuhi, walikuwa well informed lakini fedha zilikuwa zinaenda CCM so what?, hii mikataba yote mibovu ilikuwa uinajulikana lakini hipo kisiasa zaidi

wanangu TISS na UWT pamoja na wananchi tubadilike nchi inaangamia tutakuwa wageni wa nani?ona hatua za wananchi kuchoma moto vibaka imepunguza sana vibaka wakati sheria kanuni mahakama polisi vimeshindwa unapoona KIWINGU chukua hatua mbadala kila mafanikio yana KAFARA afadhali ya lawama kuliko FEDHEHA heri mmoja aangamie kuliko TAIFA LIANGAMIE! TZ KWANZA
 
Sidhani kama tanzania tunahitaji ujasusi ili tupige hatua kutoka hapa tulipoi tangu uhuru......naamini ujasusi ni hatua ya juu kabisa na matatizo yetu watanzania ni ya kipekee kabisa na hayahitaji ujasusi.......tukizingatia yafuatayo tutaondoka kwanza hapa tulipo na ndipo baadaye nasi tutakuwa na uwezo na nafasi ya kufanya ujasusi.........

"tanzania ina kila baraka kutoka kwa mungu"...sina haja kuzitaja kwani karibia kila siku wanaharakati wanasiasa na hata kikwete mwenyewe alipokuwa anaaingi madarakani alisema "kwa tz yenye neema inawezekana"...rais anajua nchi ina neema na ndivyo mungu alivyo tupa...lakini rais huyohuyo anapoulizwa na wale wanaotufadhiri chanzo cha umasikini anasema hajui kwa nini na hachukui hatua za makusudi kuondoa umasikini.......

"nasikia ikijakutokea miujiza siku moja tukaamka asubuhi tukajikuta watz wote tupo marekani(usa) na wamarekani wote wakajikuta wapo tanzania na tukapeana miaka mitatu tu......matokeo yake marekani itageuka kuwa km tz ya sasa na tz itageuka kuwa zaidi ya marekani ilivyo sasa"...kwa nini inaweza kuwa hivyo kwa sababu viongozi wetu wa sasa wanajua kupanga matumizi yasiyo ya maendeleo...nakumbuka wakoloni walituachia viwanda vingi sana ambavyo vilikuwa vinaliingizia taifa pesa nyingi na vilisaidia sana kupunguza tatizo la ajiras nchi......natamani wakoloni wangekuja wajenge viwanda ili mradi tupate ajira na serikali ipate kodi

1.kwanza tunahitaji viongozi waadilifu na ambao wako tayari kuweka mbele maslahi ya taifa...kuanzia rais na wafuasi wake
2. Selikali kama ya tanzania ina matumizi na matanuzi makubwa sana wakati bajeti yetu inategemea wafadhiri ambao serikali zao zina matumizi na matanuzi madogo......(fikiria uingereza ambayo ni mfadhiri wetu mkuu, waziri mkuu amependekeza kupunguza matumizi kwa kukata mishahara na marupurupu wkt tz masikini wa kutupwa rais wa nchi anatapanya mali ndogo za nchi kwa anasa
3. Tukajifunze kwa wenzetu kuhusu uwekezaji na wenzetu wana masharti gani kwa wageni wanaotaka kuwekeza na serikali inanufaika vipi na uwekezaji, tusiende china tuende nigeria,kenya, zambia kwani kutoka kenya tunapata vikombe vya plastic na tooth stick......tukaangalie huko ili nasisi tuondokane na ujinga wa mrahaba wa 3%(ajabu duniani)

-sijawahi kuona mantiki yoyote ya kugawa mikoa na wilaya na majimbo ya uchaguzi kwani hii ni kuongeza mzigo wananchi kwani huko kote kunahitaji gharama kubwa.....hakuna takwimu zozote hapa tanzania zinazoonesha kuwa mikoa midogo ina maendeleo makubwa kuliko mikoa mikubwa au wilaya ndogo zina maendeleo makubwa kuliko zile ndogo na kadhalika...hapa ni matakwa tu ya viongozi wetu ili mradi waonekane wamefanya kitu fulani hata kama ni cha kipumbavu
-baraza letu la mawaziri ni kubwa mno kuliko hata mabara ya wafadhiri wetu na lina hitaji fedha nyingi kuliendesha wakati rais wa nchi hayuko kuwawajibisha hata pale wanapoamua kusaini mikataba usiku na nje ya nchi.......haya yote ni matumizi yasiyo ya lazima ...linatakiwa baraza dogo na lenye tija...
-bado kikwete haamini kuwa viongozi wanaishi kwa mishahara na marupururpu ya anasa kupindukia na hayuko tayari kupunguza mshahara wake na wa wasaidizi wake ambayo ni mikubwa sana,,,,,,,sitaki kutaja mishahara yao hapa kwani wananchi wengine wakijua sana wana ghadhabu kupita kiasi na si vizuri watu km hao wakajua sana kwani wanaweza kuasi
-hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa wezi wa mali ya umma, wanaendelea kutanua na rais ananendelea kuwakejeli watz kwa kuwasafisha na hata wengine ambao kesi zipo mahakamani.....nchi haiwezi kuendelea na tunahitaji majasusi wa kuwafanyia ujasusi viongozi wetu ili kuwajua kama kweli wana nia ya dhati ya kutukomboa ana wana lao jambo km kikwete anavyopenda kusema..........

-kikwete alipoingia madarakani 2005 kitu cha kwanza alichofanya ni kuangalia namna gani atarudisha fadhira kwa marafiki zake......kitu cha kwanza kufanya yeye lowasa,rostamu waliamua kujitengenezea kampuni feki ya richmond na kuwaibia watz 152,000,000 kila siku.........baada ya hayo unatakiwa ujasusi kujua kikwete kwa sasa anataka kuwapa fadhira watu wa kundi gani? Makundi ya dini?...dini gani? Kwa nini?...marafiki zake?...familia yake?...tumfanyie ujasusi....tukifanya hivyo tutaepusha mengi....
-nchi haina dira kila kiongozi akiingia anaendesha nchi kama wamasai wanavyoswaga ng,ombe....tumefikia mahali rais anaangalia nani wa upande wake na nani wa upande wa yule .....hatuhitaji ujasusi ktk haya

naamini nimewachosha sana...poleni sana hii ni kwa sababu ya machungu nani nawakilisha machungu ya wengi ukiwemo wewe unayesoma either ni ccm,chadema au.....
 
Sidhani kama tanzania tunahitaji ujasusi ili tupige hatua kutoka hapa tulipoi tangu uhuru......naamini ujasusi ni hatua ya juu kabisa na matatizo yetu watanzania ni ya kipekee kabisa na hayahitaji ujasusi.......tukizingatia yafuatayo tutaondoka kwanza hapa tulipo na ndipo baadaye nasi tutakuwa na uwezo na nafasi ya kufanya ujasusi...................
Nakubalina na wewe kiasi lakini hoja yangu nimetumia neno UJASUSI kuhoji sera zetu na mwelekeo wetu.

  • Piga simu ubalozi wa tanzan china kuulizia China inanuaa chai kahawa ya ton ngapi kwa mwaka. Hutapata jibu.Utarushwa rushwa. Wachina wakipiga simu ubalozi waokuuliza info za kiuchumi wanapata kirahisi? kandarasi wa china akipiga simu ubalozi kwake ataambiwa tenda ngapi za barabara zimetangazwa na watatumiwa. Mchumi yeyote aliyemaliza Chuo anaweza kupewa kazi kama hizi kwenye balozi zetu. huu sio ujasusi unahiitaji kificho.
Ujasusi naosema mimi sio ujasusiwa kisiri siri. Ni ujasusi wa karne hii wa kuajiri mfano wachumi kwenye ofisi za balozi zetu nje wa wapewe kazi ya kutuma taarifa ambazo wala sio za siri kwa manufaa ya Tanzania.

  • Mbona kampuni za kichina zinainajua barabara ngapi na za KM ngapi zinatakiwa kujengwa Tanzania. Kupata Info hizi wala hatuhitaji watu wenye mafunzo ya ule UJASUSI wa zamani.
  • Je nani anajua taarifa ambazo balozi zetu za nje zinatuma zinatakiwa kuwa na nini. Je kuna requirement ya mabalozi wetu wafuatilie opprtunities nchi zilizopo na kutuma taarifa ili watanzania wafaidike?
  • Ninajiuliza utasikia Kuna mwambata wa kijeshi nchi fulani na nchi sijawai kusikia kuna mwambata wa kiuchumi. Why?

My point sera ya TISS inatakiwa kubadilika pia. Na TISS kushirikiana na Foreign affairs wanaweza kuwa chachu ya kupiga hatua. Sikubaliani nawewe Ujasusi wa kiuchumi na kitekenolojia hauwezi kuwa na mchango wake.

Tatizo kubwa la decion makers wetu ni kufanya kazi kwa style ya Business as usual. No creative and Innovative ideas za New way of doing things. iwe Ni TISS, wizarara na Idara za serikali na hata mashirikika.
 
Kwan tanzania ina majasusi???... As far as i can think tuna mashushu tuu!....
 
Shell walipoingia NIGERIA walijipenyeza kila idara ya serekali wan watu amabao wanawapa information za nini kinaendelea kwenye serekali hadi Raisi/Govenor anawazanini, wanapata taarifa ( According to CABLES from Wikileakes)

Nadhani sisi hatuhitaji kuwa namna hii!

Tuanze na KATIBA MPYA KWANZA
 
wandugu mmenishika pabaya ngoja nami nitoe dukuduku langu,UWT na serikali kwa ujumla hawana qualified people kwa kazi za kijasusi. Mf.sekela yupo UWT,baada ya kufeli std 7.babake anampeleka kusoma sekondary huko malawi, baada ya kufeli form 4 ya huko, babayake anampeleka CBE,dar, baada ya kushikwa na majibu ya mtihani anafukuzwa chuo,kwa vile babake ni mbunge na ana urafiki wa kunywa bia pamoja na mzee kijiko wa usalama,anamuunganisha mwanae huyo kupata kazi usalama wa taifa then baada ya miezi6,huyo huyo kijiko anampa ujauzito binti wa rafiki yake ki umri ni sawa na binti yake, akiwa ni mfanyakazi mwenzie,uhasama unaingia kati ya kijiko na baba sekela then, hakuna outcome yoyote, hao ni wachache kati ya wengi ambao ni disqualified people waliopo ktk kitengo nyeti kama hicho,wanatabia za kupenda anasa, hapo kuna uzalendo kweli? Ujasusi wao ni kuwachezea rafu wapinzani wao na wenye mitazamo tofauti na wao,kama walivyo muua imran kombe,kolimba hata kigoma malima. Kazi ipo wana jf. Niishie hapa. Naomba kuwasilisha.
 
Kwan tanzania ina majasusi???... As far as i can think tuna mashushu tuu!....
hoja ni kwamba je kuna kitengo cha mashushusu au minformer au jin lolote lile wa Uchumi, teknolojia. Hii idara yetu inavyo vitengo hivi.

Nimesoma cables za USA utaonna balozi za marekani zinatafuta si data za kiuchumi lakini zinasaidiia hata kampuni zao.

Russsia walitaka kuanzisha Huduma yao ya kadi kama za master card na VISA. Wamerakni wakajua russia wakianzisha kampuni zao ( master Visa) zitaanza kupteza masoko. Guess Balozi wa USA alishauri nini.

Kwa hiyo utaona nchi kama USA zinatumia ofisi za balozi kama kama source ya taarifa za ki ushushu za Kiuchumi/ Kiteknolojia zinazowez kusaidia au kuathiri nchi zao. Je Tanzania wapo. China hao wamefika mbali sababu hiyo hiyo.

Shell walipoingia NIGERIA walijipenyeza kila idara ya serekali wan watu amabao wanawapa information za nini kinaendelea kwenye serekali hadi Raisi/Govenor anawazanini, wanapata taarifa ( According to CABLES from Wikileakes)

Nadhani sisi hatuhitaji kuwa namna hii!

Tuanze na KATIBA MPYA KWANZA
Teh Teh teh kwenye katiba mpya ni vitu gani unataka viwekwe ambavyo vitatua matatizo? Maana upya tu wa katiba tu sio issue . Kama mada hapa wanajadili katiba. ebu njoo tunadilishane ideas.https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tiba-mpya-katiba-mpya-je-inatakiwa-iweje.html
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom