Tanzania yetu ina majasusi wa aina gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yetu ina majasusi wa aina gani?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mtazamaji, May 23, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Katika soma soma zangu nimeona jinsi ujasusi wa kiteknolojia na kiuchumi ilivyoisaidia china kufika hapo ilipo. Lakini Nimekuwa najiuliza je serikali yetu ya Tanzani inao majasusi wa aina hii?

  Ninahisi bado serikali yetu ime concentrate kwenye ujasusi wa kufatilia maisha ya watu , wizi, ujambazi , na wale wa kuakikisha serikali iliyopo madarakani haipati vikwazo kutoka kwa wananchi wake, etc.

  Ingekuwaje kama Serikali ya Tanzani ingepata taarifa mapema za kijasusi ikafanya kila liwezekanalo kile kiwanda cha kukata dahabu kisijengwe Uganda na badala yake kijengwe Tanzania.

  Je Kuna majasui wa kichumi wanafuatilia au kujua bajeti za kenya na uganda zitafanya mabadiliko gani yatakoyotahiri upande Tanzania . Ujasusi wa aina hii ni muhimu ili kujipanga na kuwa katika advantage.

  nadhani Vision na Mission ya TISS au UWT inatakiwa iwe ya style hii. Kuwachezea faulo kenya na Uganda kwa manufaa ya watanzania sioni kama ni kosa.

  Je Tanzania tunao majasusi wa kichumi au kiteknolojia? Je si sawa moja ya wajibu wa mabalozi wetu nje ya nchi kuwa majasusi wetu wa kiuchum?

  Nawasilisha
   
 2. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
  Ni kweli asilimia kubwa ya information zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na human intelligence badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari. Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari ka kijasusi ili tuweze kupata information za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi information hizo.
  Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!
  Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo.
  Kwa mfano Malawi sasa hivi wanachimba uranium. Tuna majasusi ambao wanajua kinachoendelea kule au ndio hivyo tena watu wamekazana kufanya ubadhilifu kwenye balozi zetu wanasahau kuwa moja ya kazi za balozi ni kutufanya kila linalowezekana kuweza kupata information zenye kutuwezesha kama Taifa?
   
 3. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi mashushushu wa TZ kazi yao nini?..ukikaa hivi unasikIa mara fulani ni shushushu..mara taxi dreva fulani ni mtu wa system... mara mwanafunzi fulani naye yuko kwenye system....

  kaaazi kweli kweli...
   
 4. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .Hao majasusi wanahitajika tu kwa nchi zinazojua wanachohitaji na kikwazo nini?. kwetu rais kasema HAJUI SABABU ZA UMASIKINI WETU la pili NCHI HAIENDELEI BILA WAWEKEZAJI. Sasa hao majausi watafanya kazi gani kama Tanzania haijui imekwama wapi na kwamba maendeleo inaletwa na wa geni. nadhani mpango wao wa muda mrefu ni CCM kubaki madarakani daima. Na ndo kazi za majasusi wetu. kufanikisha hilo. Mambo ya hujumu uchumi unaoendeshwa na viongozi wetu kama epa, uwizi wa rasilimali, wakina RITES wamekuja juzi tu sasa wanaondoka na mabilioni,zain tayari wamefaidi, Kila mkataba ni feki na haiwezi kuvunjwa wajaja wameshakula chao, yanayojiri Loliondo, wamewaachia wakina kikwete wana siasa. kwao ajira si zaidi ya miaka 10 anahakikisha anavuna cha kumtosha na wajukuu zake basi. Tanzania haimuhusu.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Majasusi wa Tanzania wapo kwa minajili ya kunusana na kufuatiliana ilhali sisi wote ni watanzania. Tena kikubwa wapo kwa ajili ya kulinda WATAWALA na si kuilinda nchi kama katiba inavyosema. Nina maana kuwa hawaangalii wala kujishughulisha na mere people kama wapo salama kiuchumi, kiafya, kiustawi na kimaadili lakini wapo kwa ajili ya kuripoti kwa waliowaweka ktk post hizo ndo maana tunawaona wengi wamepewa zawadi za madaraka ilhali hawapaswi kuwa viongozi. wanapaswa kuwa viongozi wa viongozi wetu lakini wanaongozwa hawana jipya kwetu.

  Wanafukuzana na vijitu vidogo wakiacha keki ya Taifa ikiliwa na mijitu mikubwa.

  Nilishawahi kuandika kuhusu hili miezi kadhaa hapo nyuma kwamba tukitaka kufanikiwa kiuchumi, kiutamaduni na hata kuwa taifa lenye nguvu duniani tunapaswa kuhakikisha taasisi zetu za kijasusi zinapata right people na si wajomba wajomba. Wanalipwa pesa nyingi sana mpaka zinaundwa kampuni za kuchota pesa za nchi kwa jina la taasisi zetu za kijasusi lakini wao wako kimya wala hawajishughulishi kulinda utu na hazina nchi. Hivi ile sheria ya baraza la usalama la TAIFA mmeisoma? mnajua waliomo ndani yake? na je ni mahitaji yetu kwa sasa? Najua kuna watu unapowaamia USALAMA WA NCHI wao wanajua definition moja tu kuwalinda viongozi hata wakivunja katiba wasiguswe kwa kuwa vyeo vyao ni taasisi nyeti na haipaswi kuwashughulisha wakienda nje ya mstari.

  Naapa kama hatutakuwa na taasisi imara ya kijasusi tutaishia kulindana lindana kusiko na TIJA
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kulikuwa na mpango wa kujenga kiwanda cha kusafisha dhahabu Tanzania chini ya rais Mkapa. Nasikia aliyepiga stop ni Kikwete kwa sababu za uhusiano wake wa karibu na Sinclair.
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Duh hii tetesi kali kwa hiyo watu wanaotakiwa kuwa mstari wa mbele kutetea uhai wa taifa ndo wanakuwa mbele kuwa TISHIO la Taifa. Inawezekana kama ni kweli hao wawekezaji ndo wakaamua kwenda Uganda.

  Wenzetu china wameonyesha mfano. wanacheza hata faulo kwa sababuya kulinda maslahi ya taifa lao. nina hakika makampuni ya china yanajulishwa miradi inayotaka kuanzishwa tanzania /africa na ofisi zao za balozi . Sasa sijui kama Ofisa wa balozi tanzania nchini china ina wajibu wa kutuma opportunities za kibiashara kwa Watanzania.

  Mfano Kuna mfanyabiashara wa Tanzanite tanzania ana contact za moja kwa moja na mteja mkubwa wa hayo madini nchini China au India? Wenye contact za wateja wakubwa wa Tanzanite ni waafrika kusini au Kenya.

  Leo hii mtu akianza kutengenza oil filter za toyota feki tanzania nahika serikali ya tanzania itashirikiana na Toyota ya japan kufunga kiwanda. Lakini wenztu wachina hawalindi viwanda vya watu wasiokuwa na production site china.
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hiyo sheria ya baraza la usalama la TAIFA naweza kuipata vipi ningependa niisome. Nadhani utendaji wa hii taasisi yetu uko zaidi ki USALAMA Wa SIRIKALI.
   
 9. TingTing

  TingTing Member

  #9
  May 24, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Upinzani wa biashara ndio utasaidia kwenda mbele zaidi ingawaji soko ni huria lakini sheria bado ni za "monopolistic". Mfano ni pale ambapo unatetea maslahi ya msambazaji awa pekee katika usambazaji wa bidhaa fulani wakati inajulikana kabisa kuwa msambazaji ataweka bei yake tena ya juu ili mradi tu apate "profit" la asilimia zaidi ya 100. Vitu kama hivi ndivyo vinafanya milipuko ya bei ovyo ovyo. Tutoe mawazo na sheria za umimi umimi, tupunguze kodi kwa mwananchi na kurudisha kodi kwa kila mwekezaji maana wengine wanatumia vibaya mwanya huu, mfano ni Celtel, imekuwa Zain na itakuwa kitu kingine baada ya muda tu, nyingine ni ile hotel ya SHeraton. Hawa jamaa wakishapata hela zao basi wanajidai kufanya kama wameiuza kwa wengine kumbe bado tu unakuta bado wanayo sema kupitia kampuni mama na wanazidi kupewa "tax exemptions". Nchi hii, inapotezwa na wale wanaotuwakilisha katika kila kitu sijui ni kutokana na ufinyu wao wa elimu, mawazo yao binafsi au uwizi wao wa vyeti feki!
   
 10. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hiivi wandugu kwa serikali hii--namaanisha hii mnazani tunaweza kuwa na majasusi wenye manufaa? Majasusi tulio nao ni wale wakufatilia vyama vya upinzani na kuwamaliza wanaoonekana Tishio la kisiasa kwa vyama vya Kipinzani? au hamkumbuki DR Slaa alivyowekewa vinasa sauti kule Dodoma? Au hamkumbuki mkasa Wa Salome Mbatia ? Au hamkumbuki wale waliomwaga unga bungeni? Hawa ndo majasusi wetu. Hivi tutafika kweli. MIMI KWA MTAZAMO WANGU BILA KUWABANDUA WALIO MADARAKANI tutaendelea kuwa na majasusi wa kihivi hivi!
  Nawakilisha
   
 11. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Mbona umemsahau KOLIMBA & SOKOINE ukitaka kujua kazi ya majasusi wa Bongo rejea historia ujue kazi ya majasusi wa Hitler hutaumiza kichwa kama mimi nisivyoumiza kichwa
   
 12. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hii ni kweli kwa sababu sinclair ni rafiki yake mkubwa na vasco dagama wetu tangu akiwa waziri wa nishati na madini hivo isingekuwa rahisi kiwanda hicho kijengwe tz wakati mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kwenda kusafishwa na kutoa madini mengine (ores) una dhahabu kibao
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kweli kwa majasusi wa bongo kazi yao kubwa ni kuilinda ccm na serikali yake idumu milele ndicho wanachowaza nani yupo kinyume na ccm nani anataka kuwania uraisi kupandikiza upinzani feki wapo bize kwa hilo kiasi kwamba awawezi kugawa makundi ili lishugulike na ujasusi wa kitekenolojia na biashara
   
 14. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ujasusi wa tanzania ni kitetea ccm ibaki madarakani 100 yers to come, kuna mambo madogo tu ambya hayaitaji hata ujasusi kuyaelewa, lakini twaingia kichwa kichwa. 1.... Kiwanda cha mwananchi gold kilipigwa vita na world bank... Watanzania tukaingia na kushabikia 2... World waliwahonga maafisa pale madini na nishati mradi wa umeme wa makaa ya mawe chini ya ndc usianze, kisa mradi wao wa umeme wa gesi usingekuweza kufanikiwa, mh. Nyimbo aliupigania wakamtema,,, sasa ebu angalia national interest iko wapi? Tuna enda wapi.....kuan maandiko yaliwahi tolewa na mtaalamu juu ya resort katika security secotr reform na akatoa mfano kwa nchi kama tz
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Najua tunavyojimwaga humu jukwaani kuna jamaazetu, watanzania wenzetu wanakosa usingizi kwa kutufuatilia na how to eliminate some of us. halafu utashangaa wametumwa na tuliowaweka madarakani. Shame to those.

  Ninyi majasusi wetu, mnapaswa kufahamu kuwa mnalipwa kodi za mere people, na hao wanaowakalia kichwani hawalipi wala kukatwa kodi hata chembe, na kibaya zaidi wanaliibia taifa kwa miradi feki kibao. Ninyi majasusi wa TZ mnapaswa kuumiza kichwa kujua how shilingi isishuke thamani kama mkulo anavyo chekelea, na ni nani yupo kwa tija ya TAIFA na si kwakujihalalisha madarakani ilhali hana uwezo. Angalieni kuna watoto wangapi wanayimwa haki ya kuishi punde wanapozaliwa kwa kukosa huduma sahihi, angalieni wimbi la vijana wanaokosa elimu kutokana na sera za elimu za ubabaishaji za serikali yetu. Tunashindwa hata kufikiria kwamba kuna siku tutarusha satelite yetu angani kwa sababu kila tunachokusanya ktk KODI hakiwekwi reserve kinaliwa na kuundiwa mfumuko wa bei kwa kuongeza pensheni za watawala wastaafu na mishahara pia marupurupu. Fikirini kuhusu mikataba ambayo watawala wetu wameingia kwa sura ya kuiuza nchi. Je inawezekanaje kule Loliondo kuwa kipande cha Mfalme wa Saudia na akapandisha bendera yake wakati tuna usalama wa Taifa mahiri? Mtajitoaje kwenye lawama za kuruhusu rais mtendaji kuamua kuitumia ofisi ya UUMa kusaliji kampuni yake na mkewe akiwa madarakani huku kalumekenge ambaye ni afisa wilayani haruhusiwi kufanya hivyo? Mtajitengaje na kashfa za usambaaji holela wa silaha nchini? Mnajinasuaje na mipango ya chini ya meza ya kushinikiza maamuzi ya CHAMA ilhali ninyi mpo serikalini? Mbona mnatuaibisha jamani? Sina shida endapo more funds zikapelekwa kuimarisha ujasusi wa kimaendeleo na si imla za kifalme zinazojitokeza na kujiimarisha nchini. Kumbukeni kwamba moto huunguza mpaka chuma hivyo mafuriko yakija huzoa kila kisafi na kichafu.
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wewe umeona hadi gari la rais limechomoka gurudumu kweli kuna majasusi hapo? Niliwahi kusema na narudia tena kiwanda chetu cha nyumbu kilikufa kwa kuuliwa na wamarekani CIA kwani leo hii Tanzania ingekuwa inatengeneza magari yake ya kijeshi. Hapo majasusi wa bongo wako wapi???

  Labda kumtafuta mwanzilishi wa CCJ...hilo wanaweza....kushinda kwenye bar.
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Usisahau kuwa huyu anaitwa mwanzilishi wa CCJ naye alikuwa afisa usalama jeshini. Na maafisa usalama jeshini wako na TISS bega kwa kichwa. Kazi kwenu!
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wakuu majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi ni informers. Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT kazi yao kubwa iko kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti opposition na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against himaya ya CCM.

  Usalama wa Taifa ulianzishwa na CCM kwa hiyo bado unaiserve CCM na sio Taifa, kama ungekuwa unaiserve Taifa mambo mengi tunayolalamikia sasa yasingekuwepo.

  In simple words, kazi yao ni kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

  Kazi kubwa nayoweza kusema naikumbuka kwa hivi karibuni ni kukama wale majambazi wakubwa waliokuwa wanavamia mabenki. Naweza kusema they did an excellent job, wangefanya hayo kwenye mengine tungekuwa mbali sana.
   
 19. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Security Sector Reform in​
  Developing and Transitional Countries........................

  Domestic commitment and ownership: many, but limited reforms​
  Virtually every state is involved in some sort of reform that changes the way security
  institutions and actors operate. This, however, does not imply that these reforms can all be labelled
  ‘security sector reform' as it is understood in the development community (see box 1). Questions
  remain about the direction of such reforms and how reforms are implemented. Often, the reform
  efforts are not directed at improving the security of the population but are exclusively aimed at
  rationalising or modernising armed forces and police to save money or to enhance their postures
  and capabilities.
  We can identify several contexts or reasons for reforms with some of these categories
  obviously overlapping:
  • Budgetary necessity (almost all countries with reform programmes)
  • End of war or conflict and post-conflict peace-building (Afghanistan, Cambodia, Sri Lanka, East
  Timor, Mozambique, South Africa, Haiti)
  • Continued war or unsettled conflicts with strengthening of the security sector organs (Columbia,
  Ethiopia, Eritrea, Nepal)
  • Transitions from military rule (several Latin American countries, Ghana, Benin, Mali,
  Indonesia)
  • Post-authoritarian experience (all successor states of the former Soviet Union)
  • Single-party authoritarian dispensation (Cap Verde, Tanzania, Laos, Vietnam)
  • Participation in UN peacekeeping (several West African and Central European states, Argentina,
  Bangladesh)
  • Joining military or political alliances or blocs (the new members or candidates of NATO and the
  European Union).​
  Box 5: Intelligence Services​
  "The role of intelligence services in the security sector should be recognised and
  addressed. Practically all governments find it necessary to maintain specialised forces in
  this area... Intelligence agencies should be included in security sector reform where their
  work is concerned with internal security threats. In this area, donors have been reluctant to
  contribute, as the need for transparency that pervades all other efforts in security sector reform
  is difficult to reconcile with the development of secret services. To counteract the obvious lack
  of transparency, the intelligence agencies must be subject to some form of civilian control. A
  complete detachment of such services from a general process of reform may easily undermine
  constructive development in other areas."​
  (NUPI 1999. p. 19)
   
 20. Red pepper

  Red pepper Member

  #20
  May 28, 2010
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa hakuna majasusi. Waliopo ni informers tu. Kwanza jasusi huwezi kumjua kwa sababu anafanya kazi kwa usiri mkubwa, hio ni sifa ya kwanza. Pili, ni 'intelligent' sana, anajua mambo mengi nk. Hapa watu wanaona ujiko kujulikana tu ni informer.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...