Tanzania yafuzu kushiriki kombe la dunia la mchezo wa kabaddi

Kahema juma fimbo

New Member
Jul 29, 2022
1
0
Timu ya taifa ya Tanzania ya mchezo wa kabaddi imefuzu kushiriki mashindano ya dunia ya mchezo huo ambayo yanatarajiwa kufanyika nchini India mwishoni mwa mwezi Oktoba. timu hiyo imefuzu baada ya kushika nafasi ya pili katika mashindano ya afrika ambayo yalimalizika mnamo julai 28 katika mji wa Sharm el Sheikh nchini misri.

Timu hiyo imeweka historia kwa kuweza kufuzu huko kushiriki mashindano hayo kwani kunaifanya kuwa ni timu ya tatu ya taifa kufuzu kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya timu ya taifa ya walemavu na timu ya soka ya wanawake chini ya miaka 18 kufuzu awali mwaka huu kushiriki katika kombe la dunia.

Kufuzu huko kunatarajiwa kuongeza hamasa ya mchezo huo kwa wadau mbalimbali ambao wanajihusisha na mchezo huo. timu mbili za tanzania ambazo ni za wanawake na wanaume zote zimefuzu kushiriki mashindano hayo ya kimataifa ambayo yanatarajiwa kuchezwa nchini India.​
 
Kama vipi tutafute na mchezo mwingine wa kizembe zembe kama huo wa Kabadi, ili tuwe tunafuzu mara nyingi kushiriki hayo mashindano ya dunia. Maana kule kwenye soka, hali tete kweli kweli.

Ukiona tu mapaka Somalia wasio na ligi wanatutoa jasho! Basi ujue hali tete kweli kweli.
 
Back
Top Bottom