LoyalTzCitizen
JF-Expert Member
- Sep 15, 2010
- 2,323
- 1,088
Mbona kimya! Au jamaa wameshatupuliza goli la 2?
Draw mkuu 1-1
Mbona kimya! Au jamaa wameshatupuliza goli la 2?
Binafsi pia sijaona lolote la muhimu lililoletwa na Poulsen....Poulsen: hana jipya kwa Starz, tangu akabiziwe timu kiwango kinazidi kushuka, kuna haja ya kuachia ngazi si mpaka aundiwe tume.
Binafsi namlaumu sana Poulsen........Kwa leo naweza kusema ametunyima ushindi......Mtalaumu makocha bure. System nzima ya mpira Tanzania ni mbovu. Msitegemee maajabu yoyote bila ya kusafisha system yote kwanza.
Naunga mkono hoja, tutumie makocha wazalendo huenda wakawa na jipya!Binafsi pia sijaona lolote la muhimu lililoletwa na Poulsen....

Ni kwa nini kamuweka bench Victor Costa?,

Ni kwa nini hakumuanzisha Mrisho Ngassa?.....

Ni kwa nini amemtoa Shaban Nditti ambaye alionesha kuelewana vizuri sana na Henry Joseph kiasi cha kuleta uhai pale kati?...

Mechi ya leo ilikuwa ni rahisi sana kwa Stars,tungeweza kushinda hata kwa magoli matatu kama sio manne....Victor Costa ni beki ambaye yupo kwenye kiwango bora kabisa lakini kocha kamuweka benchi na kuwaanzisha Nyosso na Aggrey na sote tumeona uzembe wa Nyosso na Nsajigwa ndio umepelekea Algeria wasawazishe goli,Nyosso kachelewa kuruka hivyo kumpa nafasi mchezaji wa Algeria kufunga goli....Ifikie kipindi Shadrack Nsajigwa apumzike sasa,awaachie vijana wacheze mpira....kawa mzito sana...

Pale katikati kulikuwa na maelewano amzuri sana kati ya Henry Joseph na Shaban Nditi na walikuwa wanapeleka mipira sana mbele kiasi cha kufanya Mbwana Samatta ang'are pale mbele lakini cha kushangaza kocha anamtoa Nditti na kumuingiza Machupa ambaye hajafanya lolote...Kutolewa kwa Nditti kumepelekea Abdi Kassim arudi kwenye kiungo cha kushambulia na Henry Joseph kucheza kiungo cha kukaba hivyo kupooza mchezo/kupunguza kasi ya mchezo.....Baada ya kutoka Nditti mipira mingi haijaenda mbele hivyo kumfanya Samtta asing'are tena kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza.....

Kule mbele Abdi Kassim na Danny Mrwanda walikuwa ni mzigo......Walitakiwa kutolewa mapema sana....Sijui ni kwa nini kocha alimuweka mchezaji kama Ngassa benchi....Sote tunamjua Ngassa kwamba ni mchezaji ambaye daima hutengeneza ushindi kwa timu ama kwa kufunga ama kutengeneza magoli..........Inaumiza sana.....

Namkumbuka sana Marcio Maximo.....Sijaona jipya lolote lililoletwa na Jan Poulsena wala Kim Poulsen tangu waje nchini......

Je kuna haja ya kurudi nyuma na kufikiri kwamba sasa ni wakati wa kuwapa timu aifa ya Taifa makocha wazalendo(akina Jamhuri Kihwelo,Dkt.Mshindo Msolla,Juma Mwambusi na wengine) badala ya kupoteza fedha za walipa kodi kwa makocha wageni ambao hakuna jipya lolote wanalolileta kwa Taifa letu????

Tafakari.....................Chukua hatua
Au inahitajika kafara??Sasa wadau, nchi ye2 tutaitofautishaje na Jehanamu! Kwani kila kona Maumivu. Tanzania bwana du.

Mkuu Bala umetoa tathmini nzuri sana, wengi wetu tunakerwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona uwezo na mapungufu ya mchezaji mmoja mmoja na kujipanga namna ya kutengeneza "combinations" za kutupatia ushindi, hii haikuwa mechi ya kutoka sare.

Poulsen na kurugenzi ya ufundi TFF hovyo kabisa, wamesababisha tukose ushindi leo!
Binafsi namlaumu sana Poulsen........Kwa leo naweza kusema ametunyima ushindi......
Ni system ipi hasa unayoizungumzia?.....Maana mfumo wetu na wakenya na Uganda hauna tofauti.....Kenya wameshinda leo na uganda wanahitaji sare tu kuqulify kwa ajili ya AFCON 2012
Tafa Stars:
1. Juma Kaseja
2. Shadrack Nsajigwa
3. Amir Maftah
4. Aggrey Morris
5. Juma Said Nyoso
6. Shaban Nditi
7. Nizar Khalfan
8. Henry Joseph
9. Mbwana Samatta
10. Abdi Kassim
11. Danny Mrwanda
Ngassa kaanza benchi
Watch Tanzania vs Algeria Live Stream Online
Lakini mbona Stars wamecheza vizuri wakuu!!

Mzanzibari 1 (Abdi) Watanganyika 10. Ili kutoa haki, ratio ya wabunge, etc. ilitakiwa iwe hivi hivi