Tanzania tunaweza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tunaweza!

Discussion in 'International Forum' started by Ubungoubungo, Mar 22, 2009.

 1. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Jamani, tuboreshe reli ya kati toka Dar hadi Kigoma, pale tuunganishe reli toka Tabora au kigoma hadi Burundi na Rwanda(waziri wa Rwanda alishakuja hapa unakumbuka), pia tutengeneza barabara nzuri itakayopitia kule Bukoba au kama kuna uwezekano tuunganishe na reli hadi Uganda, huku zambia wanatutegemea kwa Tanzania Zambia Road authority, tanzania railway authority(Tazara) na bomba la mafuta tazama. kule mozambique, daraja likiisha tu mwaka huu mtu anaweza akasafiri kwa gari haraka sana hadi s.africa kwasababu wareno walijenga barabara safi toke mozambique hadi sauz, malawi ni kuwaunganisha kidogo tu pale Kyela au hata na barabara au reli toka Mtwara(mtwara corrido) hado Kyela au hata mpakani na malawi. tumezungukwa na milango mingi ya kuexport.

  nimeangalia kuna jamaa mtz mmoja hivi kule mashada ya wakenya, aisee amefafanua sana hili nikapenda. itaisha lini watz wanaoenda bukoba au mwanza kupitia kenya na uganda wakati wanaenda kwenye nchi yetu humuhumu? hivi kwanini? au hili lilishaisha wajameni wanaojua tuelezeni. kwanini tusitengeneza na barabara toka Bongo hapa hadi bukoba na mwanza mtu asafiri kwa siku moja hata kwa gari ndogo ya mark two? sina uhakika kama ni solved mtanirekebisha, lakini kitu cha muhimu, nilitaka watu wajue namna tz inavyowez kufanya mambo makubwa hapa.

  Burundi inatutegemea kuingiza mizigo yao, Rwanda nayo hata kama kwasasa wanawategemea kenya through uganda, lakini wanataka direct isipitie nchi nyingine. uganda itafika tu kipindi watakapoona kupitia kenya ni ukoloni, hivyo tutawanyang'anya wakenya wateja wao wa mombasa port.

  kuipiku mombasa port ni muhimu sana. tufanyeje? ni kuiboresha bandari ya Dar, na pia kama tulivyoambiwa kipindi sha nyuma kuwa wawekezaji toka Saudi Arabia wanakuja kujenga Bandari kubwa Bagamoyo, hiyo ingekuwa kitu kikubwa sana. hivi hili wazo lilienda wapi? UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO? na kuboresha bandari ya Tanga na Mtwara daraja la mzumbiji likiisha? vipi hapo? kama viongozi wetu ni wazalendo na wana uchungu na nchi kama sisi wengine tulivyo, hivi tutashinda kufika mbali kweli? hapana, tunaweza. Mungu ibariki Tanzania. Amin.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Bado tu kama kms 120 barabara pale Singida yote iwe na lami toka Dar hadi Mz- na kuna mkandarasi anaendelea na kazi!

  Ni kweli toka dar hadi Mz kwa sasa unafika siku hiyo hiyo.. basi ni nyingi tu Muhamed Transp n.k.. ni chache sana sasa hupitia Kenya!

  Je wewe haujapitia hii njia karibuni? Pitia kwa gari ujionee!

  Reli ndo naona bado..bado tunasuasua!
   
 3. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  basi viongozi walioshika rungu(ambao hawataki ushauri wa watu)wajaribu kufikiria vitu vya muhimu zaidi kama infrustructures wakijua kuwa, hizo zikiwa bora, basi mambo yataenda murua haraka.
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa si kms 120 tena ni kama kms 70 tu zilizobaki, na jamaa wanakwenda spidi nzuri, sehemu iliyobaki nadhani mpaka mwisho wa mwaka au mapema mwakani itakuwa imekamilika ni sehemu ngumu sana, kabla na baada ya Manyoni.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ubungo ubungo,
  Nimependa sana mawazo yako. Yana target nzuri kiuchumi. Lakini nina hakika watawala wetu hili hawalioni. Na kama wameliona hakuna mwekezaji ambaye kesha kubali kuwapa ten% hivyo hata kama ni mawazo mazuri yataendelea kubaki kabatini mpaka apatikane yule atakayekuwa tayari kuwapa 10% yao au kama si hivyo miradi kama hii itasubiri awamu ya 23 ndipo yatafanyika.
  Kwani hujasikia mipango yao mingi wanasema itakuwa imetekelezwa ifikapo 2025? nani kati yetu atakuwa karibu kuwaambia kuwa hawakutimiza?
  Ni wakati huo vijana wao watakuwa madarakani wakiendeleza ufisadi na kusema mambo hayakuwezekana maana hayatekeleziki. Na watakuja na sababu lukuki kuwa hali ya uchumi wa dunia ilkuwa mbaya kwa hiyo mambo hayakwenda kama ilivyotegemewa. Na hapo itakuwa mwisho wa story.
  Viongozi wetu wasisikie kuna tatizo la kimataifa hapa wamepata scape goat maana mara utasikia hali ya bei ya mafuta mbaya, hali ya chakula mbaya, hali ya hewa mbaya, na sasa ngoja uje usikie story inayofuata kuwa hali ya uchumi wa dunia mbaya. Na kwa sababu hiyo hawakutekeleza ahadi zao.
  Wamenikumbusha yule mwanafunzi ambaye alimuonyesha baba yake msomi wa zamani karatasi zake za shule lakini zikiwa na alama ya chini. Na mzazi alipomuuliza kwa nini umepata alama za chini? alimjibu short and clear kwamba shule haikuwa na metamophosis hivyo ikamfanya vipindi viweze kuwa sawa pia. Stay tuned.
   
 6. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Ubungo ubungo,
  Thanks for you patriotic idea. Ni jambo lisilokuwa na ubishi kuwa, kama tutaunganisha nchi kama Rwanda, Burundi, Uganda na DRC kwa njia ya Reli na Barabara tunaweza kupata pato kubwa kutoka kwa hawa jamaa.

  Sasa nikueleze hatua iliyofikiwa ambayo naiona ingawa inamapungufu lakini jamaa wamejitahidi. Kuna Barabara ya kutoka Itigi, Tabora hadi Kigoma weneyewe wanasema mkandarasi amepatikana na wameanza kuikwaruza. Kuna mto malagalasi kunahitajika daraja kama lile la mto rufiji, mkandarasi wa kikorea ameshapatikana. Kutoka Kigoma mjini kuna barabara inatengenezwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa kichina, barabara hii ni ile inayopita kwenye jimbo la Mhe. Zitto na kuishia kwenye mpaka wa Tanzania na Burundi. Kwa upande wa Rwanda, kuna barabara ya kasahunga ambayo nayo iko katika kiwango cha lami kwenda Rwanda wanaojua zaidi watatuelewesha. Ninavyoona mimi tayari serikali imejitahidi kutenegeneza baraba unganishi ambazo kwa kweli ni muhimu kwa uchumi wa nchi yetu. Lakini Reli ingefaa zaidi kutoka na uwezo wa kubeba mizigo mingi kwa wakati mmoja.
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  nisahihishe kidogo, barabara ya kwenda rwanda ni kutoka rusahunga na siyo kasahunga na hii ilijengwa miaka ya zamani inahitaji marekebisho kidogo
   
 8. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mawazo mazuri naamini viongozi wetu watayaona haya na kuyafanyia kazi kwa haraka na kuepuka migongano ya kisiasa tu.
   
 9. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  barabara ni muhimu kwa kusafirisha binadamu na mizigo isiyo mizito.kinachotakiwa tuangalie RELI yetu,na sisi wananchi na serikali yetu tusimame kidete kuiboresha reli.
  reli inauwezo wa kubeba mizigo mizito,mingi na wakati mfupi kuliko barabara.
  Serikali imiliki reli na kuruhusu kampuni nyingi zitumie reli,yani kuwe na makampuni yanayomiliki mabehewa ya abiria na mizigo.kama ulaya eg.UK kuna kampuni zaidi ya 6 zenye kutumia reli kwa mizigo na abiria.
  Je sisi tufanyaje kuiwajibisha serikali. what process should we use to make our leaders answerable.naomba mawazo jinsi ya kuwafanya walio madarakani kutuwakilisha wawajibike vizuri,at the moment TRL wanatumia tu pesa,huduma mbovu na hakuna maendeleo
   
 10. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Si kuna dili lile la Tanzania na Rwanda kuunganisha reli, siku ile si alikuja hadi waziri wa mawasiliano wa Rwanda yule mdada, si mnakumbuka, dili hilo, Rwanda wanategemea mombasa, wakenya ndio wakoloni wao, ndio maana hata east africa headquoter utakuta walikuwa wanajibembeleza kwa kenya kuwaunga mkono kwasababu wameshikwa masikio. tukifanikiwa kufanya lile dili la reli toka tabora au kigoma hadi Rwanda itakayounganisha reli ya kati, aisee tumesha nyakua dume. Burundi ndo wako kusini mwa rwanda, wafanyeje lazima watapitishia mizigo yao hapa Dar. Congo nao ni muhimu. wanatumia sana bandari yetu, sasa tujitahidi ili bandari ya Angola isitupiku. nimependa sana pia huu mjadala, tuendelee kujadili pengine viongozi wetu watapitia humu na kujaribu kuyafanyia kazi zaidi, pamoja na kwamba mengine yameshaanza kufanyiwa kazi.

  Naipongoza selikali kwa daraja la msumbuji. tukiwa na usafiri mzuri kuingia msumbiji kupitia bandari ya mtwara, na malawi, tukawa wazuri kwenda zambia, congo, burundi na rwanda, na baandae kwa mseveni, jamani Mungu atupe nini? kenya hakuna dili, ndo maana hata ile reli toka tanga hadi mpakani mwa kenya haina dili hadi inaoza, kwasababu kenya hamna dili. tukamatie hizi nchi, Mungu ametupatia ni zetu.
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Yote haya 9 sasa kumi je Bandari zetu haswa Dar mbona hakuna mkakati kuipanua unaoeleweka? Ni bla bla tu kila siku!
   
 12. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hata Raila Odinga lipokuja siku ile, sio kwamba alikuja kutalii hapa bongo, alikuja kule bandarini aone madhaifu yetu ili akaipanue zaidi mombasa kuendelea kutupiku. nilisikia kuna watu kule kurasini watabomolea nyumba zo ili kupisha kupandua bandari ya Bongo, tatizo sema wabongo tunakuwaga wa polepole sana kwenye masuala muhimu kama haya, linaweza kuwa limewekwa kapuni hadi kampeni za uchaguzi zitakapoanza ndo wanaanza kujenga msingi ili iwe silaha kwao. wanachojali wao ni kupigania wasiondoke madarakani, sio kwamba watz tuone wamefanya kitu wakiwa madarakani.
   
 13. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  God bless Tanzania
   
Loading...