Tanzania tuna safari ndefu na ngumu sana chini ya CCM

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Wakati Tanzania tukiwa na mawazo ya KIJINGA kufikiria kukamata wanaotumia VPN kisa huduma ya internet bongo ni mbovu na TZ inazuia baadhi ya mitandao ya kijamii kupatikana nchini bila sababu za msingi.

Wenzetu wanajenga vinu vya nyuklia kwaajili ya nishati ya umeme. Juzi kati serikali ya kijeshi ya Burkinafaso imeingia mkataba na Urusi kujenga vinu vya Nuklia vya kuzalishia umeme kwa ajili ya kugawa umeme kwenye maeneo ya BurkinaFaso ambayo hayakuwa na umeme kwa asilimia 80%. Sisi bado tuko kwenye kufungiana kutumia VPN, na kufunga baadhi ya mitandao kupatikana Tanzania.

Ni Tanzania hii hii Bilionea Elon Musk aliomba kibali cha kutoa Internet ya bei Rahisi na ya Kasi kubwa yaani 1GB kwa 100/= (shilini mia moja). Lakini serikali ya CCM inayosema inawajali Watanzania ikakataa na kuona bora tuendelee kuibiwa na makampuni ya simu yanayouza 1GB kwa 2,500/=. Starlink wamekwenda Rwanda, Zambia, Kenya nk, Wameona TZ tubaki na upuuzi wetu siku tukijitambua watakuja. Unajiuliza hivi CCM inawatakia nini hasa watz?

Tanzania tuna utajiri mkubwa wa madini ya Uranium yanayotumiwa katika urutubishaji na uzalishaji wa nishati ya nyukliavinu ambayo yangetumika kutengeneza umeme, Tanzania ina gas asilia ambayo ingetumika kutengeneza umeme, Tanzania ina mito mingi ambayo ingetumika kutengeneza umeme, Lakini Tanzania ni nchi inayoongoza kwa mgao wa umeme kusini mwa jangwa la Sahara ambako chama tawala kiko madarakani kwa zaidi ya miaka 60 sasa toka tupate Uhuru, utafikiri Nchi imekuwa ya utawala wa chama kimoja, single party system.

Serikali imejaa watu wa chama kimoja, bunge limejaa wanasiasa wa chama kimoja, Polisi na askari ambao walipaswa kuwa neutral yani wasiofungamana na siasa nao ni wafuasi wa icho chama. Ikifika wakati wa uchaguzi mnatuma majasusi wakajiunge na vyama vya upinzani ili ionekane Tanzania kuna demokrasia huko kimataifa, mkishavuruga vyama hivyo ndipo mnarejea kwenye chama chenu.

Nchi ina tatizo la uongozi, nchi ina kila aina ya raslimali lakini ni masikini kupindukia....! Miaka 60+ ya uhuru, ati tunafikiria maji, barabara, shule, umeme nakadharika kweli?

Inasikitisha sana. Tunazidiwa hadi na Nchi tunazozizidi rasilimali, top 10 ya matajiri wamejaa waarabu na wahindi tu ambao wengi background za familia zao ni za kuamia Tanzania, huku mtanzania mweusi akibangaiza tu kwenye ardhi yake.

Bado tukihoji mnatufungia na kutukamata, wasanii wanaoimba nyimbo za kupinga matendo mabaya serikalini mnawakamata na kuwabambikizia kesi. Where are we heading as a nation.
 
Wakati Tanzania tukiwa na mawazo ya KIJINGA kufikiria kukamata wanaotumia VPN kisa huduma ya internet bongo ni mbovu na TZ inazuia baadhi ya mitandao ya kijamii kupatikana nchini bila sababu za msingi, Wenzetu wanajenga vinu vya nyuklia kwaajili ya nishati ya umeme...
Duuh...hatari na nusu
 
Adui mkubwa wa Mtanzania yeyote ni ccm (Chama Cha Mapinduzi) na siyo Maradhi,Umasikini wala Ujinga kwa kuwa hivyo ndivyo vinavyokibeba chama cha Ccm!
 
Mnakumbuka kilichofanyika wakati wa uchaguzi mkuu 2020 chini ya dikteta jiwe? Walizima internet.

Sasa uchaguzi unakaribia, wanajipanga kufanya yao.

Hili taifa sijui linaelekea wapi?
 
CCM inatakiwa atolewe madarakani
 
Wakati Tanzania tukiwa na mawazo ya KIJINGA kufikiria kukamata wanaotumia VPN kisa huduma ya internet bongo ni mbovu na TZ inazuia baadhi ya mitandao ya kijamii kupatikana nchini bila sababu za msingi.

Wenzetu wanajenga vinu vya nyuklia kwaajili ya nishati ya umeme. Juzi kati serikali ya kijeshi ya Burkinafaso imeingia mkataba na Urusi kujenga vinu vya Nuklia vya kuzalishia umeme kwa ajili ya kugawa umeme kwenye maeneo ya BurkinaFaso ambayo hayakuwa na umeme kwa asilimia 80%. Sisi bado tuko kwenye kufungiana kutumia VPN, na kufunga baadhi ya mitandao kupatikana Tanzania.

Ni Tanzania hii hii Bilionea Elon Musk aliomba kibali cha kutoa Internet ya bei Rahisi na ya Kasi kubwa yaani 1GB kwa 100/= (shilini mia moja). Lakini serikali ya CCM inayosema inawajali Watanzania ikakataa na kuona bora tuendelee kuibiwa na makampuni ya simu yanayouza 1GB kwa 2,500/=. Starlink wamekwenda Rwanda, Zambia, Kenya nk, Wameona TZ tubaki na upuuzi wetu siku tukijitambua watakuja. Unajiuliza hivi CCM inawatakia nini hasa watz?

Tanzania tuna utajiri mkubwa wa madini ya Uranium yanayotumiwa katika urutubishaji na uzalishaji wa nishati ya nyukliavinu ambayo yangetumika kutengeneza umeme, Tanzania ina gas asilia ambayo ingetumika kutengeneza umeme, Tanzania ina mito mingi ambayo ingetumika kutengeneza umeme, Lakini Tanzania ni nchi inayoongoza kwa mgao wa umeme kusini mwa jangwa la Sahara ambako chama tawala kiko madarakani kwa zaidi ya miaka 60 sasa toka tupate Uhuru, utafikiri Nchi imekuwa ya utawala wa chama kimoja, single party system.

Serikali imejaa watu wa chama kimoja, bunge limejaa wanasiasa wa chama kimoja, Polisi na askari ambao walipaswa kuwa neutral yani wasiofungamana na siasa nao ni wafuasi wa icho chama. Ikifika wakati wa uchaguzi mnatuma majasusi wakajiunge na vyama vya upinzani ili ionekane Tanzania kuna demokrasia huko kimataifa, mkishavuruga vyama hivyo ndipo mnarejea kwenye chama chenu.

Nchi ina tatizo la uongozi, nchi ina kila aina ya raslimali lakini ni masikini kupindukia....! Miaka 60+ ya uhuru, ati tunafikiria maji, barabara, shule, umeme nakadharika kweli?

Inasikitisha sana. Tunazidiwa hadi na Nchi tunazozizidi rasilimali, top 10 ya matajiri wamejaa waarabu na wahindi tu ambao wengi background za familia zao ni za kuamia Tanzania, huku mtanzania mweusi akibangaiza tu kwenye ardhi yake.

Bado tukihoji mnatufungia na kutukamata, wasanii wanaoimba nyimbo za kupinga matendo mabaya serikalini mnawakamata na kuwabambikizia kesi. Where are we heading as a nation.
chama tawala kiko madarakani kwa zaidi ya miaka 60 sasa toka tupate Uhuru, utafikiri Nchi imekuwa ya utawala wa chama kimoja, single party system,

sasa tatzo ni la nani hapo?
 
Back
Top Bottom