Swali la leo: Tanzania iko tayari kwa kupata mgonjwa wa kwanza wa Ebola? Je, tunaangalia na kufuatilia wageni wanaoingia katika mipaka yetu na kuangalia kama yeyote kati yao ametokea Afrika ya Magharibi siku za hivi karibuni? Je, endapo itagundulika mtu ana dalili za ugonjwa huo ni protocol gani iliyoandaliwa kukabiriana na hili au tunaweza kujikuta tunafanya kama Nigeria kutengeneza protocol baada ya kuwa na mgonjwa?
Mapendekezo yangu:
a. Tuanze mara moja kumonitor watu wanaoingia kutokea nje hasa ambao kati pasi zao za kusafiria wanaonekana kupitia Afrika ya Magharibi hasa katika miezi hii mitatu au minne ya hivi karibuni.
b. Kuandaa vikosi vya afya (rapid response unit) karibu na viwanja vyetu na ndege vikiwa vimeandaliwa kupokea mtu mwenye dalili za maambukizi.
c. Hospitali kubwa karibu na maeneo ya mipakani ziandaliwe sehemu ya kuwatengea watu wenye dalili za ugonjwa huu (isolation units) pamoja na magari ya kuwasafirishia.
d. Tutenge fedha ya kutosha kukabiriana na hili.
Kama tulivyoona kwenye ugonjwa wa dengue kujiandaa kwa majanga ndio kujiepusha na maafa kama ambavyo nimewahi kusema mara nyingi. Isije kuwa tuna watu "wanaombea" kuwa Ebola isije kwetu. Kwamba uwezekano wa kutokea unaongezeka siku kwa kwa siku kwa kadiri ya kwamba watu bado wanaweza kusafiri kutokea nchi zenye maambukizi.
Vinginevyo, tusije kushangaa tutakapoambiwa kuwa kuna mtu ana Ebola itakuwa tayari mtu huyo alishatembelea Kariakoo, kwenye vilabu, n.k na tukajikuta tunashindwa hata pa kuanzia.