Tanzania tumejiandaaje kwa Ebola?

Tanzania tumejiandaaje kwa Ebola?

Mara ya mwisho kuona stats za miji mikubwa michafu katika Afrika Dar ilikuwa nafasi ya tatu, sijui kama kuna update. Na si uongo jiji la Dar ni chafu jamani!!!! Dah!!!!

update ipo,sasa dar ni ya pili. Kwa jinsi inavyojitahidi itakua ya kwanza kufikia octomber. Miji mingine wanajitahidi kua wasafi,dar inajitahidi kwa uchafu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mara ya mwisho kuona stats za miji mikubwa michafu katika Afrika Dar ilikuwa nafasi ya tatu, sijui kama kuna update. Na si uongo jiji la Dar ni chafu jamani!!!! Dah!!!!

acha tu na tena siku hizi kuna nunuka acha kabisa..............
watu wachafu, mazingira machafu miferej ya maji taka inatiririka njian kama vile sio shida
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama tunashindwa kupambana na uchafu tu katika miji yetu mingi, je tutaweza kupambana na Ebola? Katika hiyo mikakati ya tahadhari ili kujiepusha na Ebola usafi wa miji yetu ungepewa kipaumbele nambari moja, lakini hilo sijalisikia, au kampeni zozote za kuhamasisha Watanzania kufuata taratibu mbali mbali husika ili ugonjwa huu usipige hodi nchini. Je, hiyo idara husika inajiandaa kimya kimya bila kushirikisha Watanzania!?

shaka ondoa BAK na Gefu idara husika wamejipanga. ishu kubwa hapa kwetu kuna wale wenzetu wanao pita njia za panya hao ndio watakao tuletea.

umeskia madereva wa malori wamepewa angalizo sasa sijui wangapi watakao chukua hatua
 
Mimi nadhani huu ugonjwa utaletwa hapa tanzania na wauza Unga wa west africa wakishirikiana na hawa mademu wa bongo wanao jigongaga kwao!
 
Wako makini usiwe na wasiwasi

...mkuu wasiwasi wangu ukipenya wote sirikali na wananchi tutapaniki hapo ndo tutapigwa vilivyo,we si umeona ishu ya imtu wote na serikali tulipaniki alafu tukapigwa butwaa mpaka baada ya siku tatu ndo tumepata akili angalau ...
 
Toka lini Tanzania ikachukua tahadhari kabla ya hatari,
subiri ugonjwa ukianza mauaji ndo tume zitaundwa.
 
Kama tunashindwa kupambana na uchafu tu katika miji yetu mingi, je tutaweza kupambana na Ebola? Katika hiyo mikakati ya tahadhari ili kujiepusha na Ebola usafi wa miji yetu ungepewa kipaumbele nambari moja, lakini hilo sijalisikia, au kampeni zozote za kuhamasisha Watanzania kufuata taratibu mbali mbali husika ili ugonjwa huu usipige hodi nchini. Je, hiyo idara husika inajiandaa kimya kimya bila kushirikisha Watanzania!?

...yaani mkuu nikivuta picha ya dengu ilivyotupeleka..!? Mungu atusaidie ninamashaka sana na uwezo na uratibu wa plan za kupambana na majanga bado sana,watu watawaza kujenga badala ya kusaidia...
 
Kuna kitu kinaitwa Global Pharmacy...Yaani kuna magonjwa mengi ambayo yapo bara la afrika na asia ambayo hayana tiba na ni kwasababu pharmaceutical companies hawafinance kutafutwa kwa dawa,na ebola ni ugonjwa unaowaua sana waafrika,ngoja ufike ulaya uone kama hawajafuta dawa kwa spidi ya umeme. Ijapokuwa pia ikumbukwe ebola ni aina ya virusi ; na virusi wa aina yoyote hakuna dawa ya kuwaua japo zipo ya kupunguza dalili since wanavamia immune system! Mfano ugonjwa kama parkinson's disease unawaua sana wazungu na ni maarufu sana scandanavia lkn dawa zipo za kupunguza symptoms na hatimae kuongeza life quality na muda wa kuishi 🙂
 
Mh huo ukifika bongo watu watapukutika kama sisimizi,japo naongea kwa uchungu hebu fikiria homa ya dengue tu na watu wamefariki wengi tu,kusema kweli hali si nzuri!na tatizo jingine hapa sisi tunaongea kuhusu kuchukua tahadhari lkn jamii inayotuzunguka haichukulii suala hili kwa umakini,na itachukua muda sana mpaka kubadili hali hio kwa kweli maana usafi wa mazingira tu ni tatizo itakuwa kudhibiti kusambaa kwa virusi.Hivi kuna sheria za kuzingatia watu wanaoingia na kutoka tz na hizi hongo zilizojaa?
 
Nadhani serikali kupitia wizara ya afya na wanasiasa watakua wanaandaa mchakato kwa ajili ya kuaandaa mchakato wa kuleta mpango wa kuandaa timu ya kuunda tume ili iandae mchakato wa kuweka wataalam na elimu kwa umma kabla ya kuanza rasmi kujiandaa na kuzuia ebola, mchakato huu wote utahitaji posho, magari, study tour, warsha, makongamano na heshima maalum kwa wajumbe wateule

waziri anawasiliana na watendaji wake kuangalia nani hasa ataweza kucoordinate zoezi zima

msiwe na wasiwasi, we have A+ in planning
 
...hahahaaa loh mkuu naamini wakimaliza hayoyoote watapelekewa consultant kwaajili ya upembuzi yakinifu..hapo watanzania watakuwa wamebaki wawili tu...
 
...hahahaaa loh mkuu naamini wakimaliza hayoyoote watapelekewa consultant kwaajili ya upembuzi yakinifu..hapo watanzania watakuwa wamebaki wawili tu...
usicheke aisee... nchi sio mchezo

michakato, mipango-kazi, maandalizi, upembuzi, rasimu, marejesho, sera nk ndio way to go

we are not action oriented, we are the thinkers and dreamers!!
 
Mara ya mwisho kuona stats za miji mikubwa michafu katika Afrika Dar ilikuwa nafasi ya tatu, sijui kama kuna update. Na si uongo jiji la Dar ni chafu jamani!!!! Dah!!!!

Best hebu shika fagio tuanze usafi... :couch2:
 
  • Thanks
Reactions: BAK
usicheke aisee... nchi sio mchezo

michakato, mipango-kazi, maandalizi, upembuzi, rasimu, marejesho, sera nk ndio way to go

we are not action oriented, we are the thinkers and dreamers!!

Dah huu ugonjwa usifike tu kabisa mana tutaumia mana vitu vya kawaida kama usafi wa mazingira unatushinda na hapo mpaka waandae tume kuchunguza huo ugonjwa na magumashi mengi si tutaisha ukichangia hata mipakani hongo na uelewa wa jamii husika Mungu auepushie mbali
 
Mungu ailinde Tanzania jamani huo ugonjwa ni hatari.
 
Back
Top Bottom