Tanzania tumejiandaaje kwa Ebola?

Tanzania tumejiandaaje kwa Ebola?

Tusubiri tupate mmoja tu, utaona Tume nyingi zikitungwa kuchunguza chanzo cha ugonjwa.
 
Swali la leo: Tanzania iko tayari kwa kupata mgonjwa wa kwanza wa Ebola? Je, tunaangalia na kufuatilia wageni wanaoingia katika mipaka yetu na kuangalia kama yeyote kati yao ametokea Afrika ya Magharibi siku za hivi karibuni? Je, endapo itagundulika mtu ana dalili za ugonjwa huo ni protocol gani iliyoandaliwa kukabiriana na hili au tunaweza kujikuta tunafanya kama Nigeria kutengeneza protocol baada ya kuwa na mgonjwa?
Mapendekezo yangu:
a. Tuanze mara moja kumonitor watu wanaoingia kutokea nje hasa ambao kati pasi zao za kusafiria wanaonekana kupitia Afrika ya Magharibi hasa katika miezi hii mitatu au minne ya hivi karibuni.
b. Kuandaa vikosi vya afya (rapid response unit) karibu na viwanja vyetu na ndege vikiwa vimeandaliwa kupokea mtu mwenye dalili za maambukizi.
c. Hospitali kubwa karibu na maeneo ya mipakani ziandaliwe sehemu ya kuwatengea watu wenye dalili za ugonjwa huu (isolation units) pamoja na magari ya kuwasafirishia.
d. Tutenge fedha ya kutosha kukabiriana na hili.
Kama tulivyoona kwenye ugonjwa wa dengue kujiandaa kwa majanga ndio kujiepusha na maafa kama ambavyo nimewahi kusema mara nyingi. Isije kuwa tuna watu "wanaombea" kuwa Ebola isije kwetu. Kwamba uwezekano wa kutokea unaongezeka siku kwa kwa siku kwa kadiri ya kwamba watu bado wanaweza kusafiri kutokea nchi zenye maambukizi.
Vinginevyo, tusije kushangaa tutakapoambiwa kuwa kuna mtu ana Ebola itakuwa tayari mtu huyo alishatembelea Kariakoo, kwenye vilabu, n.k na tukajikuta tunashindwa hata pa kuanzia.
Mkuu Mwanakijiji, tumeshindwa kuchimba vyoo kwenye shule zetu za msingi na sekondari, tumeshindwa kusafisha miji yetu, tumeshindwa kusambaza maji safi na salama katika jamii zetu, tumeshindwa kudhibiti malaria na magonjwa mengine yatokanayo na uchaufu... Tutaiweza Ebora? Rushwa na ufisadi havitaturuhusu kufuata ushauri wako!
 
Hivi kwani hii nchi imejiandaa kwa Crisis ya aina gani ? au ghafla umekuwa mgeni wa hili taifa letu...

tumejiandaa na tuko tayari kuidhibiti chadema na ukawa kwa gharama zozote hata kama wafanyakazi hawatalipwa mishahara yao hadi 2015
 
Jibu kwa swali ni kuwa hatupo tayari kuwa na mgonjwa wa Ebola. Nani anayetaka kukumbwa na majanga?

Hata kama ingekuwa ni marekani ambao wana uwezo mkubwa wa kukabili majanga watakujibu hawapo tayari kuwa na hilo janga.

Mkuu ungelisoma swali sawia , na maelezo ya sred yenyewe uenda ungekuwa na katita nafasi tofauti.
 
MM hujamsikia JK anasema hili Tatizo la West Africa?huyu bwana sijui vipi.

Saudi Arabia wamereport cases za Ebola, na wako outside Africa, huyu anadhani TZ ni mwezini.If this disaster makes its way to TZ, people will die in hundreds, because of irresponsible leaders.here is to hope nature rescues our poor souls again.

Alivyotoa hoja yake mimi nilibaki mdomo wazi! Bado watu wa FC b7 Lumumba wanampongeza eti huo ulikuwa ni makakati wa kuvutia wawekezaji na utalii - please give me a break! Lakini siku hiyo hiyo tukasoma kwenye magazeti ya bongo kuwa nchi za SADC zinaandaa mkutano wa ku-address issue ya ebola. Nikajiuliza, washauri wake walikuwa bado hawajapata habari hizo - maana kwa mantiki hiyo angeunganisha hoja yake kwamba tatizo la mlipuko wa ebola huko WA ni tatizo linalohitaji jitihada za global community na hususan nguvu za umoja wa Afrika, na nchi za SADC tayari zinaanda mkutano!! John Kerry alikuwa tayari ameishawapa vidokezo kuwa dunia ya sasa ya mtandawazi imeshonana kama wavu.
 
Huyu rais wetu sijui alikuwa anaongea nini nafikiri angekaa kimya angeonekana yuko sawa kuliko alivyo zungumza mi nimekimbia tv sikuweza kuimalizia ile aibu.
 
Alivyotoa hoja yake mimi nilibaki mdomo wazi! Bado watu wa FC b7 Lumumba wanampongeza eti huo ulikuwa ni makakati wa kuvutia wawekezaji na utalii - please give me a break! Lakini siku hiyo hiyo tukasoma kwenye magazeti ya bongo kuwa nchi za SADC zinaandaa mkutano wa ku-address issue ya ebola. Nikajiuliza, washauri wake walikuwa bado hawajapata habari hizo - maana kwa mantiki hiyo angeunganisha hoja yake kwamba tatizo la mlipuko wa ebola huko WA ni tatizo linalohitaji jitihada za global community na hususan nguvu za umoja wa Afrika, na nchi za SADC tayari zinaanda mkutano!! John Kerry alikuwa tayari ameishawapa vidokezo kuwa dunia ya sasa ya mtandawazi imeshonana kama wavu.

Kwakuwa jamaa ni average Cue's kama za Kerry hakuweza kuzinasa, yani yeye alikuwa oveerwhelmed na ile occasion,Matatizo mengi ya Serikali ya JK yanatokana na kuwa jamaa kazunguwa na D Team, wakati yeye mwenyewe ni C player.hivyo akikutana na A players hupwaya sana, refer to his interview Obama alivyokuja TZ, aliulizwa maswali mepesi, bado akatoa upepo tu.

Watanzania Please, kwa kuwa CCM wote ni corrupt, please do us all a favour and select a smart corrupt technocrat come 2015.
 
Watu wako bize na bunge la katiba na kutengeneza vijembe kwa UKAWA.

Badala ya kuandaa mpango mkakati na mazingira ya kuzuia kuingia kwa ugonjwa huo ambao umeshaua more than 800 people in West Africa, watu wamekaa tu wanakula allowance huko Dodoma.
 
Hili ni jambo la kuombea tu kwamba lisitufikie

Hali yetu ya kujiandaa na kukabiliana na hali za dharura kama hizo (mergency preparedness and response) ni ya kiwango cha chini mno

Ingekuwa na uwezo ningezuia safari zote za watu wanaoenda au kutokea afrika mangaribi!

Kama tu vipimo vya kawaida mahospitalini ni shida itakuwa kwa huu ugonjwa wa ebola?
 
inahitajika 'bajeti' na 'warsha' na 'semina' na vikao vya 'kupanga mikakati' ya kupambana na hilo gonjwa....kama Dengue ilivyo kuwa

Nakuunga mkono,vilevile wananchi waelimishwe kuzuia kwa kuelewa chanzo cha ugonjwa. Repoti mbalimbali zinasema chanzo ni wanyama pori kama nyani,na popo na wengine. Pia nguruwe anaweza kuwa na virusi vya ebola. Unaambukizwa kwa kula hizo nyama au mizoga yao kuingiliana na vitu mbalimbali vya makazi ya watu. Hivyo tujiepusha kula nyama hizo,tujitahidi kula nyama salama kama kuku,ngo'ombe,mbuzi,kondoo,samaki.
 
Back
Top Bottom