FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,883
- 109,211
Tanzania tuachane kabisa na mfumo wa kuwapandishia watu mishahara au vyeo bila kuwa na vigezo na vipimo vya "performance" zao.
Nashauri kwanza viwekwe vigezo na vipimo vya "performance" kazini ndivyo vitumike kuwapandisha watu vyeo na mishahara.
Ni wepesi sana kupanga vigezo vya ubora wa utendaji kwa kila kazi katika kila sehemu ya kazi. Tena siku hizi kila kitu kinakuwa kwenye data base kidigitali ni wepesi sana. Wale watendaji bora (best performers) watapanda mishahara na vyeo haraka na wale wazembe (kama ilivyo kwa Watanzania wengi) watasota hapo hapo na mshahara wa "entry level" mpaka wabadilike au wajiachishe wenyewe kazi.
Mfumo huu wa "performance based" upo na unatumika sana ulimwenguni, hususan kwenye kazi zisizo za Serikali, pia serikali nyingi zimeanza kutumia mfumo huo, bila kuoneana aibu wala huruma za kijinga.
Uzoefu wangu wa kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda mrefu sana katika nchi zilizoendelea umenifundisha hayo.