Tanzania Plant Health and Pesticide Authority (TPHPA) kuwa bussiness as usual na kupoteza lengo la kuanzishwa kwake

Amo90

Member
May 20, 2020
26
75
Tanzania Plant Health and Pesticide Authority kifupi TPHPA ni mamlaka ilioanzishwa kwa uunganisha taasisi ilioitwa TPRI na Plant Health Service (PHS) iliokuwa chini ya wizara ya kilimo. Taasisi hii ilitegemewa kuwa mkombozi ktk kudhibiti afya ya mimea kwa kuzuia uingiaji au usafirishaji wa vipando vyenye magonjwa kwa kufanya ukaguzi wa kutosha maeneo ya mipakani na viwanja vya ndege. Pia taasisi hii ilitegemewa kuwa na kuwa msimamiz mkuu wa viatilifu yaan pesticides ili kuhahikisha viuatilifu vyote vinavyotumika nchini vinakidhi matakwa ya kisheria na kimazingira.

Uanzishwaji wa TPHPA unaonekana utashindwa kufanikiwa kutokana na uongozi wa taasis kufanya vitu as business as usual hivo kuwa haina utofauti na taasis zingine au kutoleta tija iliokusudiwa kama ifuavyo.

1. Taasisi imeshindwa kuintergrate watumishi wake kuwa kitu kimoja yaan PHS na TPRI watumishi wake hawaongei lugha moja kumekuwa na matabaka hivo kudhorotesha utendaji kaz wa taasis. TPRI wamekuwa superior kuliko PHS kiasi kwamba taasis moja lkn hata vyeo na mishahara ni tofauti kutegemeana ulikotokea.

2. Kukosa kwa vifaa na maabara ktk vituo vya ukaguzi, vituo vingi vya ukaguzi mipakani na viwanja vya ndege hakuna maabara au vifaa vya kuwezesha maafisa kufanya kazi zao kwa ufanisi. Maafisa wanafanya bora liende tu maana huwez kufanya uchunguzi wa kitu bila vifaa.

3. Kukosekana kwa uwazi ktk utendaji kaz yaan maafisa wanafanya kazi bila transparent hata kati yao wenyewe. Afisa anaenda kufanya ukaguzi na kutoa cheti cha ubora au usafi kwa siri kiasi kwamba kuna wakati wateja wanarubudi maafisa na kuandika phytosanitary certificates bila kuona au kufanya ukaguzi wa mzigo au sample inayokusudiwa kusafirishwa au kuingizwa nchini kwa incharge pekee yake ndo anatakiwa kutoa hicho cheti na kufanya utafiti. Hii imekuwa ikitumiwa vibaya na incharges kuona hiyo ni kama kzi yao binafsi na kufanya vitu kinyume na utaratibu.

4. Maafisa viongozi (incharges) wasio na sifa. Ktk vituo vingi hasa vya mikoan na mipaka maafisa incharge ambao ndio wanategemewa kuongoza maafisa wengine ktk utendaji kazi hawana sifa za nafasi hizo. Mfano kituo kina maafisa nane wenye BSc. hadi Masters ila incharge ana certificate au diploma huyu incharge hawez kuwaongoza hao senior kwake ktk utafiti na utendaji kazi. TPHPA ni taasis inayojikita ktk utafiti na sayansi huwez kutegemea mtu wa certicate au diploma au masters kumlead mtu wa BSc, Masters au PhD hilo haliwezekani hata awe na uzoefu kiasi ngani. Science is about principles and facts.

Ni vizuri mtendaji mkuu wa TPHPA Prof. Nduguru kuangalia upya utendaji kaz wa taasisi yake na kushughulikia masuala haya kabla hawajapoteza malengo ya kuanzishwa kwake.
 
Back
Top Bottom