Tanzania sio maskini na IMF ni mabeberu, Magufuli ukatae msaada wao sasa

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,246
35,556
Siku ya leo, taasisi ya kimataifa ya fedha duniani (IMF) imetangaza kutoa msaada wa kifedha kwenda kwa nchi 28 maskini zaidi hapa duniani. Katika orodha hiyo, Tanzania imekuwa ni nchi mojawapo.

Japokuwa sote tunajua misaada hii haiji hivi hivi, mara zote nchi husika 'hupiga magoti na kuwalamba viatu mabeberu' wakati wa kuomba kupewa hiyo misaada. Pia IMF hutoa misaada hiyo kwa masharti mazito. Kwa leo tusijadili hili. Tuliweke kando.

Tuje kwenye kuamua tu, kwa kuwa sisi Tanzania tunajijua sio nchi maskini na pia tunajua IMF ni taasisi ya kibeberu kwa 100%, na msimamo wetu ni kupambana na hawa mabeberu kwa nguvu zetu zote. Sasa huu ndio wakati muafaka zaidi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli kuukataa wazi wazi huo msaada kwa sababu mbili kuu.

(i)Tanzania sio nchi maskini.
(ii)Mabeberu ndio wametoa huo msaada.

Sasa tusimame pamoja na Magufuli kuukataa msaada wa IMF!!!
 
Back
Top Bottom