Tanzania Royal Tour ilivyoudumaza utalii wa Kenya

Bibititi1

JF-Expert Member
Sep 28, 2014
464
218
Royal Tour itatupa faida gani ile movie ya kazi gani? Haya ndiyo maneno yaliyojaa kinywani kwa wanaharakati wa Tanzanaia kujaribu kufifisha Juhudi za Rais Samia suluhu Hassan.

Sisi tuliozaliwa kwenye mazingira ya utalii tuliona na kufahamu kuwa sekta ya utalii ililala usingizi wa pono.
Moja sera yetu ya kujifungia kama Kijiji na hali ya kisiasa iliyokuwepo nchini. Pili janga la UVIKO19 hii ilikuwa tishio kwa Taifa letu kwani sekta ilidorora na kuanguka zaidi uchumi ulirudi nyuma na biashara zilikufa nyingi maelfu walipoteza ajira na pato la Taifa lilidondoka.

Huko nyuma kulikuwa na jitihada zilizofanywa na wenzetu majirani wa Rwanda na Kenya katika kukuza utalii wao walifanya marketing na mbinu za kila namna ilibidi watumie udhaifu wetu kutangaza vivutio vyetu vya asili kuwa vipo kwao. walitumia kila nafasi kujinasibu juu ya utalii kwa kutumia uzembe wetu sisi wenyewe.

Ujio wa filamu ya Tanzania Royal Tour imekuwa nuru kwenye kiza kwa dunia matunda yake yanaonekana kwenye kukuza utalii katika masoko makubwa ya utalii hivi karibuni nchi yetu ilitembelewa na mwanasoka wakubwa ulimwengu Andre hererana Mauro Icardiwote nyota kutoka kunako klabu ya PSG.

Umaarufu wa Tanzania umekuwa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo hii kupitia kurasa wa klabu ya Manchester Unitedyenye mashabiki milioni 75 na utajiri wa takribani dola bilioni 4.2 za kimarekani ndiyo klabu namba moja kwa utajiri katika ligi kuu Uingereza na klabu namba ni 3 kwa utajiri Duniani. Klabu hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram imepost picha wa shabiki wa Manchester United akiwa kileleni mwa mlima Kilimanjaro akiwa na bendera ya klabu hiyo.

Kwa muda mrefu Kenya wamekuwa wakijinasibu juu ya mlima Kilimanjaro huku baadhi ya ndege zake zikiwa zimeandika maneno juu ya mlima huo mrefu. Watoto wa mjini wanasema Royal Tour ya Rais Samia imekuja kumaliza mzizi wa fitna leo Tanzania imejitokeza free kwenye ukurasa wa klabu Tajiri dunia yenye mashabiki milioni zaid ya 75 huku ikiwa na wafuasi milioni 58 kwenye mtandao huo.

Walibeza na leo wanayaona matunda ya Royal Tour kanyaga Samia watakuelewa tu.
 
Screenshot_20220614-000453.png
 
Siyo pumba nii kweli. Sema uwasilishaji umekuwa tatizo kwa mleta mada.
Hawaletwi na Royo tua; balli huwa wanakuja kila mwaka katika kipindi hiki cha summer. Nilibadilisha safari yangu ya kwenda Tanzania kwa wiki tatu lakini bei ya tiketi ikapanda sana kwa vile kuna watalii wengi wanakwenda Afrika kipindi hiki; ikabidi nisubiri hadi August.
 
Wewe ni mburula tu mshangiliaji na kwani walipokuja kina David Beckham, Will Smith, Kenny Rogers, Serena Williams, Arnie Schwarzenegger, Richard Branson, Strive Masiwiya na wengi wengineo Royo Tua yako ilikuwepo!? Au hujui na huwajui hao?! unajitekenya na kucheka mwenyewe?!
Kwendraa! Nyau wewe
 

Attachments

  • Screenshot_20220605-144718.png
    Screenshot_20220605-144718.png
    69 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220606-184120.png
    Screenshot_20220606-184120.png
    67.1 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220610-210036.png
    Screenshot_20220610-210036.png
    150.6 KB · Views: 3
  • Screenshot_20220610-210104.png
    Screenshot_20220610-210104.png
    113.1 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220611-071446.png
    Screenshot_20220611-071446.png
    93.9 KB · Views: 3
  • Screenshot_20220612-164000.png
    Screenshot_20220612-164000.png
    134.5 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220612-163951.png
    Screenshot_20220612-163951.png
    131.6 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220612-163931.png
    Screenshot_20220612-163931.png
    126.4 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220613-113438.png
    Screenshot_20220613-113438.png
    90.1 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220604-125735.png
    Screenshot_20220604-125735.png
    92.9 KB · Views: 4
Hawaletwi na Royo tua; balli huwa wanakuja kila mwaka katika kipindi hiki cha summer. Nilibadilisha safari yangu ya kwenda Tanzania kwa wiki tatu lakini bei ya tiketi ikapanda sana kwa vile kuna watalii wengi wanakwenda Afrika kipindi hiki; ikabidi nisubiri hadi August.

Umeandika kama upo Oslo kumbe upo migori una swaga Punda
 
Wewe ni mburula tu mshangiliaji na kwani walipokuja kina David Beckham, Will Smith, Kenny Rogers, Serena Williams, Arnie Schwarzenegger, Richard Branson, Strive Masiwiya na wengi wengineo Royo Tua yako ilikuwepo!? Au hujui na huwajui hao?! unajitekenya na kucheka mwenyewe?!
Kwendraa! Nyau wewe

Walikuja kulikuwa na exposure ipi walifanya zaidi ya kujificha
Elewa muktadha kaka, kirefu cha MTK ndiyo matako siyo.
 
Royal Tour itatupa faida gani ile movie ya kazi gani? Haya ndiyo maneno yaliyojaa kinywani kwa wanaharakati wa Tanzanaia kujaribu kufifisha Juhudi za Rais Samia suluhu Hassan.
Acha porojo bana.

Hivi unazani walikuwa hawajui kama mlima Kilimanjaro uko Tanzania na Dunia hii ya digitali?

Mtu asiweze hata ku google hadi asubiri Royal tua?

Hizi akili za mwaka 1980.
 
Back
Top Bottom