Tanzania Now Faces Sanctions & Diplomatic Crisis Over Iran

Tanzania Now Faces Sanctions & Diplomatic Crisis Over Iran

Status
Not open for further replies.
Inadaiwa hizi meli zilisajiliwa Zanzibar maana Znz inaruhusu reflaging ya meli za nje. Hii implication zake kama SMZ ikikataa kuzitoa hizo meli kwenye usajili ni kubwa. Maana ukiangalia sisi serikali yetu ni tegemezi sana na hata kama tusingekuwa tegemezi hii dunia ecosystem yake inategemea sana USA na Ulaya, mfano angalia hao Iran wanavyohaha sasa kutafuta mtu wa kuweka bendera kwenye meli zao.

Nafikiri muda huu tunaoongea simu ziko busy kati ya JK, Karume na mawaziri wao wa transport pamoja na wakala husika, hili si jambo dogo, kasheshe hapo...
 
Tanzania kama nchi ina haki ya kujichagulia marafiki na maadui. America na Ulaya hawana haki hata chembe ya kutuchagulia marafiki na maadui. Misaada wanayotupatia kamwe isiwe kigezo cha kututawala kwani tukiamua tunaweza kuishi bila kutegemea misaada yao. Tanzania ni taifa huru na hatufungamani na upande wowote. Mungu ibariki Tanzania.

Huo uwezo ndugu yangu hatuna, ni ndoto tu...labda miaka kumi ijayo na hata haposijui. Hii dunia yote imetawaliwa na mfumo dume ambao unatawaliwa na USA kwa taarifa yako. Hivi vikwazo vya sasa walivyowekewa Iran ni kuhusu bima ya meli zao...makampuni pekee yanayotoa bima ya meli hizi kubwa za mafuta ni ya USA na UK basi dunia nzima! hakuna kampuni za uarabuni wala Asia zinazoweza kutoa bima hizo. Na bila bima kwenye meli hakuna mtu atakeyenunua hayo mafuta, upo hapo? kwa mfumo huu ndio maana nakweleza kuwa ukiwachokoza hawa mabwana kuna namna watakubana tu kwa sababu mfumo wote umeelemea kwao...kwa hiyo fikiri kwanza kabla ya kuanza kudai kuwa hatuhitaji misaada yao kitu ambacho si kweli na uhuru wetu ni wa bendera tu kwa taarifa yako.
 
Tanzania kama nchi ina haki ya kujichagulia marafiki na maadui. America na Ulaya hawana haki hata chembe ya kutuchagulia marafiki na maadui. Misaada wanayotupatia kamwe isiwe kigezo cha kututawala kwani tukiamua tunaweza kuishi bila kutegemea misaada yao. Tanzania ni taifa huru na hatufungamani na upande wowote. Mungu ibariki Tanzania.
Kumbuka huko ndiko tumeelekeza nguvu zetu kwenda kuita wawekezaji na tumeshaambiwa bila uwekezaji nchi hii haitabadilika , hivyo walete mitaji ya kilimo , Uranium , Gold , Gas , Symbion, Kigamboni etc kama walivyomuahidi aliyewaita otherwise wataonekana wahuni tu
 
Dear President Kikwete,

I am writing to express my deep dismay that Tanzania has permitted the National Iranian Tanker Company (NITC), to reflag at least 6 and as many as 10 of its vessels under the Tanzanian ship registry, allowing them to remain under NITC ownership and continuing to transport Iran’s crude oil exports. This action by your government has the effect of assisting the Iranian regime in evading U.S. and EU sanctions and generating additional revenues for its nuclear enrichment and weapons research programs and its support for international terrorism.

It is profoundly disappointing to me to learn that your government has acted in contravention of the broad international coalition that is working together to use peaceful means, including economic sanctions, to change the threatening behavior of the Iranian regime. The decision to accept the re-flagging of NITC vessels casts a shadow over Tanzania’s international reputation.

I respectfully request that Tanzania cancel the re-flagging of the NITC vessels. Given the close and cooperative relationship that our two governments now enjoy, it would be unfortunate if this action were permitted to stand.

It would be preferable that Tanzania take this action of its own accord. However, your government should take note of President Obama’s Executive Order 13608, signed May 1, 2012, which provides for the imposition of sanctions on any entity worldwide, including foreign governments, that assists Iran in evading U.S. sanctions. In my view, reflagging Iranian oil tankers falls within the scope of sanctionable activity under that Executive Order. In addition, if Tanzania were to allow Iranian vessels to remain under Tanzanian registry, we in the Congress would have no choice but to consider whether to continue the range of bi-lateral U.S. programs with Tanzania.

Sincerely,

Howard Berman
Ranking Democrat, House Foreign Affairs Committee
 
Tanzania kama nchi ina haki ya kujichagulia marafiki na maadui. America na Ulaya hawana haki hata chembe ya kutuchagulia marafiki na maadui. Misaada wanayotupatia kamwe isiwe kigezo cha kututawala kwani tukiamua tunaweza kuishi bila kutegemea misaada yao. Tanzania ni taifa huru na hatufungamani na upande wowote. Mungu ibariki Tanzania.
Say that again man!
 
Maskini hana uchaguzi, by the way huyu bwana mkubwa wetu nae anapenda mahaba kila kona. Waarabu anawataka na wazungu pia!
 
Say that again man!
Muache anakiburi huyo! huenda naye yuko kwenye jopo la ushauri la Mr. President wetu!! Ukishakuwa tegemezi huna lolote hapa duniani, utafanywe na huyu unayemtegemea anavyotaka. Bila kuwa na mipango dhubuti tutaendelea kuwa followers. Ngoja viongozi wetu wakaidi waone! Navyojua watanywea tu vinginevyo tukubali kulambishwa mchanga, sijui kama tutaweza!!
 
huyu mtu hovyo kweli. sijui mwaka huu kichwa chake atakificha wapi. Kila siku marekani, marekani, sasa aibu hiyo inamkuta. ***** kweli... hata na mimi mwanamke ntamuita dhaifu.. Dhaifuuuuuuuuu.... mfyuuuuuuuu
Lakini kwa wanawake ni kidume wala sio dhaifu. Ulizia wakuu wa wilaya. Ukitaka jiunge na uandishi wa habari akuone.
 
Hili halina mjadala wala kulitafiti, ni kweli tupu. Tafadhali EU , US wekeni hiyo sanction upesi.
 
Tanzania kama nchi ina haki ya kujichagulia marafiki na maadui. America na Ulaya hawana haki hata chembe ya kutuchagulia marafiki na maadui. Misaada wanayotupatia kamwe isiwe kigezo cha kututawala kwani tukiamua tunaweza kuishi bila kutegemea misaada yao. Tanzania ni taifa huru na hatufungamani na upande wowote. Mungu ibariki Tanzania.

Ndio, Tanzania ni taifa huru na lina uhuru wa kuomba pia. NYINYIEM mnatuchefua sana, hivi kweli unadiriki kusema tz ni taifa huru! Kama hamwajui US na CNN, NBC, Reuters wao watatuchafua na kuleta ngome za kijeshi ktk ardhi yetu, na itakuwa kwisha. Ebu mwambieni Kikwete akaombe msamaha kwa mabwana zake.
 
Tanzania kama nchi ina haki ya kujichagulia marafiki na maadui. America na Ulaya hawana haki hata chembe ya kutuchagulia marafiki na maadui. Misaada wanayotupatia kamwe isiwe kigezo cha kututawala kwani tukiamua tunaweza kuishi bila kutegemea misaada yao. Tanzania ni taifa huru na hatufungamani na upande wowote. Mungu ibariki Tanzania.

Thubutuu! sema su.
 
Are you sure?!!!!
 
nimechoka! leo nimepata fursa ya kuongea na senior intelligence officers wa serikali ya uingereza wanasema wanafuatilia hili sakata kwa ukaribu zaidi na wakijiridisha bila shaka Tanzania itawekewa vikwazo vya kiuchumi pamoja na kufuta misaada yote. Pia jamaa wamenitonya hapa Washington DC kuwa wanafuatilia kwa ukaribu suala la Dr . Ulimboka na kusema endapo akifa tu na chanzo kuwa ni mateso aliyoyapata kuna kitu kikubwa chaja (kwa sasa ibaki siri).Nilipojitambulisha natoka tanzania mmoja wao amenijibu . nanukuu

"WE HATE CHAMA CHA MAPINDUZI"

mwisho wa kunukuu

Asante sana muungwana, ni katika jitihada za watu kama nyie tutajinasua kutoka katika mikono ya mafisadi.
 
nimechoka! leo nimepata fursa ya kuongea na senior intelligence officers wa serikali ya uingereza wanasema wanafuatilia hili sakata kwa ukaribu zaidi na wakijiridisha bila shaka Tanzania itawekewa vikwazo vya kiuchumi pamoja na kufuta misaada yote. Pia jamaa wamenitonya hapa Washington DC kuwa wanafuatilia kwa ukaribu suala la Dr . Ulimboka na kusema endapo akifa tu na chanzo kuwa ni mateso aliyoyapata kuna kitu kikubwa chaja (kwa sasa ibaki siri).Nilipojitambulisha natoka tanzania mmoja wao amenijibu . nanukuu

"WE HATE CHAMA CHA MAPINDUZI"

mwisho wa kunukuu
haya ya kweli au unafurahisha jukwaa!!!
 
Uamuzi ni juu yako JK sasa kusuka au kunyoa.Wabanie waarabu tununue kiwese(Petrol na Diesel) tsh 5000 kwa lita au wabanie wazungu utulie nyumbani auche kupiga misele kwenye nchi zao na bakuli.
 
Ulafi na ufisadi wa serikali ya Kikwete sasa unaliingiza taifa katika mgogoro wa kidiplomasia. Juzi tumeionya serikali, leo serikali ya Marekani inatoa onyo kwa Kikwete. Sababu IRAN. Watueleze ni kitu gani viongozi wa IRAN wamekuwa wakifuata Tanzania ! Mwakyembe, Membe Rostam na Kikwete Kazi Kwenu

Tanzania must stop re-flagging Iran tankers: U.S. lawmaker

WASHINGTON | Fri Jun 29, 2012 1:39pm EDT (Reuters) - Tanzania must stop the practice of "re-flagging" Iranian oil tankers or it will face the threat of U.S. sanctions and damage its ties with Washington, a U.S. lawmaker warned on Friday.

Howard Berman, the ranking member of the House Committee on Foreign Affairs, accused Tanzania of reflagging at least six and possibly as many at 10 tankers owned by the National Iranian Tanker Company.

"This action by your government has the effect of assisting the Iranian regime in evading U.S. and EU sanctions and generating additional revenues for its nuclear enrichment and weapons research program and its support for international terrorism,"

Berman said in a letter to President Jakaya Kikwete that was obtained by Reuters. Berman said if the tankers were allowed to continue sailing under the Tanzanian flag, Tanzania could face the sanctions that President Barack Obama signed into law.

He said Congress would also have "no choice" but to consider whether to continue the range of bilateral U.S. programs with Tanzania.Officials at Tanzania's embassy were not immediately available to comment on Berman's letter.

The sanctions, along with similar action by the European Union, are aimed at pressuring Iran to curb its nuclear program, which the West believes aims to develop nuclear weapons but which Tehran says is for peaceful purposes. The United States gave China a six-month reprieve from Iran financial sanctions on Thursday. The Obama administration has now spared all 20 of Iran's major oil buyers from its unilateral sanctions, rewarding them for cutting purchases of Iranian oil.

Below are some of the Super-Tankers that have been renamed, and flying the Tanzanian Flag:

Davar (previous name): Companion – Tanzania
Haraz: Freedom – Tanzania
Susangrid: Daisy – Tanzania

Hii ni akili ya kitoto. Mtoto anafikiri nikiiba sukari sitajulikana. Kumbe akila anajipaka mdomo wote!
 
...mmmmh, this saga gonna be an overwhelming stinker over "our TANKED marashi ya karafuu" and the union gov overall!!! 'Coz I don't see how serikali ya mapinduzi Zenj would back down na kuacha kusajili meli za nje, i.e Iran, knowing the ties between the two... But on the other hand, JMT nayo itakuwa katika songombinde just to protect her interests, i.e. misaada. Taking into consideration recent deals at the G8!! We heading towards collision...
 
ROSTAM AZIZ NA BIASHARA BINAFSI KATI YA IKULU ZA TEHRAN NA MAGOGONI KUTUINGIZA MAJARIBUNI KAMA TAIFA KATIKA USO WA JUMUIA YA KIMATAIFA

... wengine tumeonya sana tu juu ya Biashara za Rostam Aziz kutuingiza motoni lakini hata siku moja hatukusikilizwa na badla yake hili li-mdudu lilipewa heko kwenye jukwaa la siasa kule Igunga na kupachikwa jina la
'Simba wa Vita'.

Yeyote anayesema kwamba kwanini tuchaguliwe marafiki;

1. kwanza tangulia kujibu swali kwamba ni lini Bunge letu tukufu kule Dodomaliliporidhia hili zoezi la Meli za Irani kupachikwa Bendera yetu ya taifa na kuchanja mbuga kwa jina letu lakini kwa faida yao?

2. Je, maridhiano kama hayo yako kwenye Hansard ya bunge letu ukurasa wa ngapi?

3. Je, kitendo cha taifa letu kuingizwa kwenye biashara HARAMU na HATARISHI kama hii mbele ya uso wa Jumuia ya Kimataifa, hadi leo hii taifa letu limenufaika kiasi gani cha fedha kwa kuamua kujitwisha 'kiroba cha bangi' kilichomshinda M-Irani?

4. Je, kati ya wabunge wetu zaidi ya 350 kule Dodoma, ni wangapi wanaojua undani wa makubaliano kati ya Rais Kikwete na uongozi wa Tehran?

5. Je, Iran imekua ikiifadhili CCM kupitia 'Mwekahazina wa Taifa Rostam Aziz' kwa miaka hiyo yote huku wao wakipata maslahi-rejea gani over the counter?

6. Je, iweje Zanzibar iruhusiwe kutumia jina la 'Tanzania' ambalo wako bize kila leo KULIKANA na kutaka Muungano ufe kwa haraka sana huku wakiendelea kufanyia biashara hatarishi kama hili kwa kutumia jina hilo hilo BAYA AMBALO WAKO RADHI WAFE KULIKO KUBAKIA NDANI YAKE kujinufaisha CCM kimtindo kwa ajili ya kukusanya fedha kupitia MCHONGO BINAFSI YA KUNDI MOJAWAPO NDANI YA CCM na Iran kuja kununulia tena madaraka 2015?

7. Viongozi wa CCM wanapoingiza taifa letu kwenye biashara za kunufaisha kile kinachosadikiwa kuwa ni 'ugaidi na juhudi za kigaidi kwa mapana na marefu yake katika ukanda wetu huu na kuchinja ovyo wananchi gizani kupitia vikundi hatari vinavyofadhiliwa na serikali hiyo hiyo ya CCM' je tutawezaje kujitenga na dhambi hii kama sisi kama walazwahoi wa taifa hili hatuoni sababu yoyote ya kumwambia Dr Kikwete kwamba huko unakotupeleka HATUKO TAYARI?

NB: Swala la uhusiano binafsi kati ya Magogoni na Irani kamwe si salama kwa taifa letu kwa kuwa wananchi hata siku moja hatujawahi KUSHIRIKISHWA wala kuwekwa bayana faida na hasara zake zaidi ya kila kitu kuzungukwa na USIRI NA UFISADI WA KIFAMILIA kwa mgongo wa taifa zima. Hili halikubaliki hata kidogo hapa nyumbani na hata huko Ughaibuni.

Mwisho; sote tusisahau kukumbuka hili neno hapa - Dr Stephen Ulimboka kwa bahati mbaya sana itokee kwamba ataaga dunia au mwanaharakati mwingine yeyote yule kuguswa tena visivyo basi Magogoni wakae wakijua kwamba gharika la damu ya hao wote watakaodhurika leo ama kesho ndio itakayogeuka Tsunami la kulifunika kabisa CCM kabisa hata kabla ya jua la muula wake wa utawala wa kichakachuaji huu kuzama.

Wananchi sote tuamke na tuseme usiri katika biashara binafsi na Iran pale Ikulu lazima ikome mara moja.
 
  • Thanks
Reactions: Bob
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom