Tanzania ni tishio kwa kitu gani kwa nchi za africa mashariki?

segwanga

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,789
729
Sijawahi kuwa katika moja ya nchi za Afrika mashariki na kusikia raia wa nchi hizo wanatuogopa kwa vitu gani hasa.
Sisi tunawagopa wakenya katika nyanja nyingi mfano elimu yao inatutisha balaa hasa jinsi wanavyoweza kuongea kiingereza kuzidi wabongo, kwa sababu wabongo kipimo chao cha elimu ni uwezo wa kuongea kiingereza.

Wakenya pia wanatisha kwa ujanja wa kibiashara na wamekuwa wakijipatie mapato mengi kutokana na rasilimali zetu kama mlima kilimanjaro na Tanzanite hata babu wa Loliondo.

Ukija kwa waganda, pia wanatutisha kwenye elimu na ujanja kiaina. Je sisi tunatisha kwa lipi?
 
Ya kuongea. ukimpa ajitetee au atoe maelezo fulani au uongo ushirikina na aandike andiko ni tunataisha. Ukikamatwa kenya ni ndani tu no maelezo.
 
Ya kuongea. ukimpa ajitetee au atoe maelezo fulani au uongo ushirikina na aandike andiko ni tunataisha. Ukikamatwa kenya ni ndani tu no maelezo.

umenikumbusha dada mmoja mkenya!! alinambia wa TZ wanaongeaa!! akanambia hawezi akabishana na m TZ .. sansana wasichana wa ki TZ
 
Sisi tunatisha kwa kuwa na Mlima Kilimanjaro (the roof top of Africa), Ngorongoro (Oldupai Gorge) - Cradle/Origin of Mankind na Tanzanite - only found in Tanzania
 
Uganga, Tanzania mnatisha kwa uganga. Kenya kila eneo kuna mabango ya kupromote waganga toka sumbawanga, inaonekana mme specialize on this. Kenya pia wanatisha kwa utapeli, its not a good thing but I guess we are being honest here.
 
kwa ufisadi, ubabe na kutotimiza wajibu wetu kutaka vya bwerere kama misaada wakati tun raslimali kibao za kutosha!
 
uganga, tanzania mnatisha kwa uganga. Kenya kila eneo kuna mabango ya kupromote waganga toka sumbawanga, inaonekana mme specialize on this. Kenya pia wanatisha kwa utapeli, its not a good thing but i guess we are being honest here.

very true...wakenya wanaogopa wa tz kwa ushirikina mno..
Ukiwaambia we ni mganga umetoka tz tu...wanatetemeka.....its sad but funny also....
 
Tanzania is feared for one thing, potential. Tanzania holds enormous potential. it is scary to think what Tanzania would do if it actually got serious.

but so far it seems that the potential will remain as just that, Potential and nothing else thanks to CCM
 
Mi nadhani tunatisha zaidi kwenye sanaa hasa filamu kiukweli kwa afrika mashariki kifilamu tumekuja juu na ni tasnia inayokuja kwa kasi sana ukienda rwanda burundi uganda na hata kenya kwenyewe wanaisoma namba ingawa ndio kwaaaanza tumeanza
 
WaTanzania wanasifika kwa kutojiamini..kutokana na msingi mbovu wa elimu..
 
Tz tunatisha kwa RUSHWA na UFISADI duniani na siyo East Africa tu


Kuna hatari ya kuanza ku-export uswahili na ubabaishaji. Hivi vitu viwili ni common sana hapa Tanzania, inaonekana havipo kwenye nchi hovyo kama Somalia na Burundi.
 
East Africa Tanzania pia mwatisha kwa mziki wa kizazi kipya esp HIPHOP, ukiwaangalia akina chidi benz, nako tu Nako, mzee mzima FidQ, Profesa Jay, Langa, Mwana FA, Noorah aka baba star.. Imagine mimi ni mkenya, napenda HipHop sanaa, but i'd rather listen to Bongo HipHop than our Kenyan bullshit.
 
Back
Top Bottom