Tanzania ni nchi yenye bei ndogo zaidi ya mafuta ukilinganisha na nchi za Afrika Mashariki

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
FeTFxeIWYAIhXN0.jpg
Tanzania tunabahati sana kuwa na Rais anayejali wananchi kutokana na ruzuku ya mafuta Bilioni 100 inayotolewa na Rais Samia Suluhu kila mwezi imepelekea bei ya mafuta kuendelea kushuka kila leo.
Kupelekea Tanzania kuwa nchi yenye bei ndogo zaidi ya mafuta Afrika Mashariki.

Kuanzia leo mafuta yataanza kuuzwa kwa Dar, Petroli itauzwa Tsh. 2,886, Dizeli Tsh. 3083 na Mafuta ya Taa Tsh. 3,275 kwa lita, wa kupungua bei ya mafuta itapelekea kushuka gharama za huduma na bidhaa mbalimbali.

Rais Samia Suluhu amefanikisha kupunguza gharama za maisha Tanzania.
 
..bado bei ya mafuta ni aghali kwa watz waliowengi.

..hizo bei za rwanda, kenya, na kwingineko, hazituhusu.
 
..bado bei ya mafuta ni aghali kwa watz waliowengi.

..hizo bei za rwanda, kenya, na kwingineko, hazituhusu.
FeSIOt4XoAAKmNT.jpg

Angalia hapo tungenunue kiasi gani bila ruzuku mama kajitahidi sana aisee tnajivunia kua na Rais anaejari watu wake
 
Kisa jirani hajala na wewe ufurahie kulala njaa?

Sisi tunahoji mafuta kupanda bei kwa asilimia zaidi ya miamoja kutoka mwaka jana hadi sasa

Wakati nchi majiran mafuta hayajapanda hata kwa aslimia thelathini

Acheni kuchagua habari nzuri tu
 
Miezi iloyopita ilivyo kuwa elf 3460 na 3600. Bado watanzania waliendelea kujaza amfuta kwenye gar zao Tena demand iliongezeka Sana watu walinza tamaduni ya kujaza tank au nusu tank kuacha kununua za vidumu mtu anaenda sheli anamimina mafuta ya la mbili

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania tunabahati sana kuwa na Rais anayejali wananchi kutokana na ruzuku ya mafuta Bilioni 100 inayotolewa na Rais Samia Suluhu kila mwezi imepelekea bei ya mafuta kuendelea kushuka kila leo.
Kupelekea Tanzania kuwa nchi yenye bei ndogo zaidi ya mafuta Afrika Mashariki.

Kuanzia leo mafuta yataanza kuuzwa kwa Dar, Petroli itauzwa Tsh. 2,886, Dizeli Tsh. 3083 na Mafuta ya Taa Tsh. 3,275 kwa lita, wa kupungua bei ya mafuta itapelekea kushuka gharama za huduma na bidhaa mbalimbali.

Rais Samia Suluhu amefanikisha kupunguza gharama za maisha Tanzania.
Hivi ukiwa mkuu wa familia una iga watoto wa jirani wamekula makande huvyo wako wakila ugali wasilie au una tamani familia yako iushi vizuri?
Acheni ujinga na upuuzi wa kujilinganisha na majirani. Watendeeni best watu wenu.
 
Bei za mafuta ni GHALI sana Bado.

Serikali ipunguze TOZO lukuki kwenye Kila Lita ya mafuta Ili kupunguza Inflation.

Inawezekana petrol kuuzwa 2000 Kwa Lita DAR.

Serikali ikusanye KODI inazowasamehe WAKWEPA Kodi na Wawekezaji uchwara, pia ipunguze gharama za uendeshaji.

V8 zipigwe mnada. Viongozi watumie gari za kawaida.

Ameeeen.
 
Kisa jirani hajala na wewe ufurahie kulala njaa?

Sisi tunahoji mafuta kupanda bei kwa asilimia zaidi ya miamoja kutoka mwaka jana hadi sasa

Wakati nchi majiran mafuta hayajapanda hata kwa aslimia thelathini

Acheni kuchagua habari nzuri tu
Wewe jamaa unachuki tu na Mama si lingine
 
Unalinganisha maisha ya familia yako na maisha ya jirani yako, ni hatari na aibu!
 
Back
Top Bottom