Tanzania ni nchi huru, a Sovereign State, Mahakama zetu ni huru? Hizi ndizo hukumu zetu za haki, who the hell is Marekani kutuingilia? Je, tukubali?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,599
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa kuzungumzia Maslahi kwa Taifa, huwa nazungumza. Watanzania wenzangu, tuwe watu wa shukrani kwa yote, kukifanyika mazuri tushukuru, na hata kwa mabaya tushukuru, huwezi jua, hii hukumu ya kina Mbowe japo imegeuzwa ni mtaji, lakini tushukuru. What is TZS 350m compared to liberty? Tena usikute hukumu hii ikageuka a blessing in disguise kwa kuwaunganisha wapinzani wote wa kweli against a common enemy na kuunda a strong united front for the first time Tanzania tukapata a strong credible na serious opposition ambayo inaweza kuwa mbadala wa CCM.

Hata kama kina Mbowe hawakuhukumiwa kwa haki, lakini watakuwa huru na hizi ndizo haki zetu. Haki za kweli zinatolewa na karma pekee! Kwavile Aquiline aliuwawa na risasi moja, na kwenye kundi la wale polisi 6 waliofyatua risasi za moto, na wote kukamatwa na kuachiwa baada ya kujengwa hoja kuwa hiyo risasi iliyomuua Aquiline haikulengwa kwake, bali ilifyatuliwa juu ikaenda juu angani, kisha ikapinda kona, ikashuka chini, ikaingia kwenye daladala ikamchagua Aquiline na kumuingia!.

Polisi aliyeifyatua by now, atakuwa ameishashughulikiwa na karma, na haya ndio maajabu ya mfumo wetu wa utoaji haki. Mtu anauwawa kwa risasi, askari sita wenye silaha waliofyatua risasi wameachiwa, huku kina Mbowe waliokuwa wakiandamana mikono mitupu ndio wanakamatwa, wanaswekwa mahabusu, wanashitakiwa, wanakutwa na hatia na kuhukumiwa!. Kama wamehukumiwa kwa kuonewa, karma itamshughulikia muonevu na kuwafidia waonewa, tushukuru Mungu kwa yote.

Bandiko hili ni bandiko la swali, kuwa Tanzania ni nchi huru, a sovereign state, mahakama zetu ni zinapaswa kuwa huru, independent bila kuingiliwa. Hii kukumu ya kesi ya kina Mbowe, ni moja tuu ya hukumu nyingi za mahakama zetu, na hukumu hizi ndizo hukumu zetu za haki zetu kwa viwango vyetu vya mahakama zetu, sasa hawa Wamerekani ni nani hadi watuingilie mambo yetu ya ndani?. Who the hell are they kutuingilia?. Je, Tanzania tukubali kuingiliwa ingiliwa tuu hadi uhuru wa mahakama zetu kuingiliwa? Tukikubali kuingiliwa ingiliwa hivi si watakuja kutuingilia hadi kinyume cha ...na hata kututia vidole....machoni.

Nimesoma mahali kuwa Marekani imetuingilia kwa kuingilia uhuru wa mahakama zetu katika kutoa haki kama anavyoeleza mwana JF huyu.
The conviction of @ChademaTZ members, incl. @freemanmbowetz, on spurious charges, is more evidence of deteriorating political space & freedoms in #Tanzania. The govt's efforts to criminalize the opposition further undermines the possibility of democratic polls later this year.
View attachment 1383707
Mkuu Infomer, kwanza asante kutu inform kama jina lako lilivyo, kutuletea kile kunachoendelea duniani kwenye baadhi ya mitandao kama Twita, maana sio Watanzania wengi wanatajua haya mambo ya Twita na ku Twiti.

Tanzania ni ni nchi huru, a sovereign state, hiki kinachofanywa na Marekani, huku sio ni kuingilia mambo yetu ya ndani na kuingilia uhuru wa mahakama zetu?

No one anaruhusiwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, hata Marekani haipaswi kutuingilia!, au wenzetu mnaona raha kuingiliwa?.

Mimi ni story teller, hivyo kwa wapenda short and clear ishieni hapa, wale ma story tuendelee
Mahakama ni mmoja kati ya mihimili mitatu ya dola ambayo inapaswa kuwa huru. Huu ndio Mhimili responsible kwa utoaji wa haki ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na inapaswa kuwa huru, independent na haipaswi kuingiliwa na yeyote, kuingilia mahakama ni contempt, kikawaida kosa la contempt of the court hufanyika kabla ya hukumu lakini hawa Wamerekani wanalifanya baada ya hukumu ili kuzibagaza mahakama zetu mbele ya jamiiforumi ya kimataifa.

Hii ndio Tanzania ambayo ndio nchi yetu, huu ndio mhimili huru wa mahakama zetu, hizi ndizo hukumu za mahakama zetu, na hukumu hiyo ndizo haki zinazotolewa na mahakama zetu, sisi wenyewe Watanzania tumekubali hukumu hizi na hapa tumechangishana usiku kucha ili hiyo faini itimie tukawanusuru mashujaa wetu, who the hell is Marekani anayeibagaza mahakama yetu?.

Where is our sovereignty?.
Watanzania wazalendo wa kweli wa taifa letu, jee tukubali kuingiliwa au tusikubali kuingiliwa uhuru wetu na mataifa ya nje!, huu sio ni ubeberu?!.

Tena hawa Wamerekani wamezoea sana kutuingilia ingilia, walianzia kutuingilia kisiasa kwa kutulazimisha kufuata model yao ya demokrasia. Hawaamini kuwa nchi ya vyama vingi vya siasa, inaweza kufanya uchaguzi wa vyama vingi, halafu chama kimoja kikashinda kwa ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9%. Hivyo ndivyo Watanzania wenyewe walivyochagua kama kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, mabeberu wa Marekani, EU, na vibaraka wao hawaamini kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na wa haki. Wakatuingilia!.
Hiyo ndio the Tanzania Democracy ambayo ni part of African Democracy.

Sasa kipindi hiki tunajiandaa kwa uchaguzi Mkuu, na kufuatia precedent ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa, hiki ndicho kinakwenda kufanyika kwenye uchaguzi Mkuu, mabeberu hawa hawaiamini Tume yetu huru ya uchaguzi, NEC, wanataka NEC ipanguliwe!. Huku ni kutuingilia mambo yetu ya ndani, jee tukubali au tusikubali?. NEC ni Tume huru japo sio Shirikishi.

Kwenye hili la NEC, mimi naomba kutofatiana na wengi, kuwa kiukweli kabisa kwa mujibu wa sheria iliyounda NEC, NEC ni Tume huru, independent ila tatizo sio Shirikishi, not inclusive. Lakini my honest opinion ya matatizo ya uchaguzi Tanzania, sio NEC, ni sheria!. Tuna sheria mbovu ya uchaguzi ambayo haitoi haki sawa kwa vyama vyote, the political playground of the game of thrones in Tanzania is not level.

Uchaguzi wa October tutawashangaza sana dunia, mabeberu na vibaraka wao, tutumie masanduku ya kioo kabisa, tena tuwaruhusu hata mabeberu walete mawakala wao na mawakala wa vyama vituo vyote wawe na smart phones. Kura zinahesabiwa kituoni, kisha kila wakala aruhusiwe ku scan matokea na kuyatuma kwenye vyama vyao. Vyama vyote na yeyote aruhusiwe kufanya independent tallying ila sio kutangaza matokeo.

NEC iwe maximum transparent iweke randama ya scanned copies za matokeo ya vituo vyote.
Mtashangaa kuona CCM ikishinda kwa between 87%-93% kufuatia yale majimbo mawili ya Zanzibar na kusiwa cha Pemba kutibua ushindi wa kishindo cha 99.9% katika uchaguzi Mkuu huru na wa haki.

Juzi kati hapa, rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni Mkristo safi, na mtu mwenye maadili, anasisitiza watoto wafundishwe maadili mema, kama ni kusoma watoto wasome tuu, na sio kusoma huku wanafanya mapenzi kitu ambacho ni kinyume cha maadili ya Kiafrika, na kufanya mapenzi nje ya ndoa ni dhambi kwa dini zote.

Katika kusisitiza nidhamu na maadili, rais Magufuli akatangaza serikali yetu haitasomesha watoto wa kike watakaopata ujauzito wakiwa shuleni kutokana na kuendekeza mapenzi na ngono badala ya masomo!.

Marekani na mabeberu wengine wakatuingilia kwenye msimamo huu. Wao wanataka watoto wetu wa kike wafanye mapenzi kwa raha zao huku wanasoma na mimba zikiingia, wakazae halafu waje kuendelea na masomo.

Tena Waziri Prof. Kabudi akalitangazia Bunge letu kwa sauti ya ukali na authority kabisa kuwa kamwe, Tanzania haitawapigia magoti mabeberu hawa.

Marekani na vibaraka wao na mashirika yao ya kibeberu ikiwemo IMF na WB wakaanza kutuwekea vibano.

Huku ni kuingilia mambo yetu ya ndani, Watanzania wazalendo sisi tukasimama na rais wetu na kumsitiza kamwe tusikubali kuingiliwa uhuru wetu na tusikubali kuwapigia magoti mabeberu hawa.

Nasikia sikia juu juu tuu kuwa Waziri Kabudi, kapeleka barua kutoka kwa rais Magufuli kwenda kwa Trumpu, ndani ya barua hiyo pamoja na mambo mengine ya kumuombea msamaha yule mwanetu mpendwa wetu aruhusiwe kuingia Marekani, inasemekana kuwa sasa Watoto wa kike, wanaruhusiwa kufanya mapenzi wakiwa shuleni, na wale watakaopata ujauzito kwa bahati mbaya wataruhusiwa kuendelea na masomo katika shule Maalum za wanafunzi wamama.
Kama Wamerekani wametuingilia kisiasa, tukanyamaza, wakatuingilia kijamii, tumewapigia magoti, sasa wanaingilia Mhimili wa mahakama. Tunyamaze?. Tukiendelea kunyamaza hivi si hawa Wamarekani watatungilia kila sehemu inayoingilika hadi hata kutuingilia kinyume cha...kwa sehemu zisizo ingilika kama kuingilia mambo yetu ya ndani kwa kutuingilia katiba yetu, sheria zetu, taratibu zetu, na kanuni zetu tulizojiwekea? Si wanaweza kutuingilia hadi kumtoa mtu wetu na kutuwekea mtu wao?

Wajameni kama ilivyo demokrasia yetu, zilivyo siasa zetu, human rights records zetu, hukumu hii ndio mahakama zetu, hizi ndizo hukumu zetu na kwa upande wa haki, hizo ndizo haki zetu na huu ndio utoaji haki wetu nchini Tanzania.

Mungu Ibariki Tanzania.

Jumatano njema
P
 
Pascal Mayala huna lolote mnafiki mkubwa wewe, mbona huzungumzii mauchafu anayoyafanya Yohana na Paulo. Wameua, wamefunga watu wasio na hatia, wamewafilisi watu, wamewafunga wapinzani baada ya kuzidiwa hoja na kama haitoshi wamenunua wabunge na madiwani. Je, hayo huyaoni?

Kila mwenye akili timamu anajua kuwa sasa hivi mahakama zetu zinafanya kazi kwa kupokea maagizo kutoka kwa Yohana na siyo kutoka kwenye katiba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,
Pascal Mayalla. Kwa nchi masikini kama Tanzania zinazotegemea misaada, kwao sovereignty is just a term, juzi Kabudi kapeleka barua ya Rais Magufuli Marekani kwa Trump kuomba masamaha ili tupewe mkopo, Uhuru uko wapi hapo, sovereign state iko wapi hapo.

Kama Bashiru alivyosema CCM inatumia dola kubaki madarakani kwa advantage ya kuwa chama tawala, basi tukubali Marekani nayo inatumia advantage ya kuwa super power kuendesha na wakati mwingine kuingilia mambo ya ndani ya nchi zingine ili iendelee kuwa super power.
 
Pascal ujumbe umefika.

Yaan una ile indirect ya kufikisha ujumbe. Ngoja Kijani waje wakijua umesifia. Nimekuelewa hapo kwa Kabudi kasema hatupigiii magoti wale ma mbuzi meee na ile ya risasi kukata kona
 
Muendelezo wa unafiki wako,kama hatutaki kuingiliwa basi tujitegemee kwa kila kitu! Mimi naunga mkono Tz kuendelea kuingiliwa maana so far hayo wanayoingilia ni kwa manufaa ya watanzania,kwanini nikatae jambo jema? Yaani hata tunyanyasike kiasi gani basi tuwapinge mabeberu kuingilia kisa tu ni mambo yetu ya ndani, hell no!

Nasisitiza waendelee kuiingilia Tz maana kwa vyovyote vile wameonekana wana nia njema kabisa na watanzania!
Hatujiulizi kwanini enzi za JK tulikuwa hatuingiliwi kiasi hiki? Kwanini sasa?

Utasikia majuha eti kwasababu tumewabana kwenye madini, sasa kwani tukiwabana halafu tukawapa wananchi uhuru wao tunapungua nini? Tusijifiche kwenye vichaka vya hovyo hovyo, shubaamiti!
 
Pascal Mayalla, Mbona unahangaika sana mkuu? Hivi unawezaje kuwa mnafiki na ukaona uko sawa?
Haya mahakama ziko huru kwanini bandiko hili linakuja wakati kuna upepo mkubwa wa kisiasa kuhusu wapinzani waliohukumiwa jana?

Mahakama kuwa huru ulipaswa useme before issue inayotrend ili tujue haupo kwa ajili ya maslahi ya tumbo lako na kujipendekeza. Nchi hii ni yetu sote, usishabikie jambo linalomuumiza mwenzako kwakua hujui kesho yako itakuaje.
Alaf Pascal we ni mtu mzima bora hata ungekaa kimya tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulisoma fasihi enzi zako na ukaelewa vzr?


Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi huyu ni Pascal au kuna mtu ametumia akaunti yake! Uchwara mtupu. Yale ya Rwanda yalipotokea 1994, kilichofuata jumuiya ya mataifa ikiwa ni pamoja na kanisa katoliki walilalamikiwa kwa kukaa kimya! Pascal kwa ajili ya mapenzi/ushoga wake na utawala haoni tunakoelekea wala haja ya kukemea! Amani ya Nchi iko pembamba sana! Angalia ule umati uliofika Kisitu!
 
Back
Top Bottom