Uamuzi wa Mahakama kuhusu DP World umethibitisha mahakama zetu haziko huru

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Ukiona mahakama inatumia katiba ya Falme za Kiarabu kuhalalisha Dubai ni nchi inayostahili kunufaika na sheria za mikataba ya kimataifa badala ya kujikita kwenye Lome & Geneva Conventions ujue hatuna mahakama.

Uhalali wa Dubai na DP WORLD kuingia mikataba ya kimataifa inabidi utokane na Geneva & Lome Conventions siyo katiba za nchi husika. Uamuzi huu unamaanisha Zanzibar kwa vile katiba yake nayo inajiita ni nchi basi inaweza kuingia mikataba ya kimataifa na kulindwa na makubaliano ya Geneva & Lome Conventions jambo ambalo ni batili.

Msimamo sahihi wa kisheria

Mahakama ilipaswa ichunguze kama Dubai na DP WORLD ni wanachama wa Geneva na Lome Conventions ili waweze kunufaika na nafuu za mikataba ya kimataifa. Vinginevyo sheria zetu zilipaswa kutumika kubatilisha mkataba na azimio la kibunge liloridhia uwekezaji wa DP WORLD.

Inapokuja DP WORLD kukidhi mahitaji ya kisheria ya kuingia mkataba kwa sheria zetu wanasema sheria za mikataba haziwahusu bali zitawahusu baadaye. What kind of nonsense is this? Aidha kama haiwahusu sasa basi hata baadaye haitawahusu au kinyume chake.

Ukiona mahakama inaikana katiba yetu na sheria zake kuwa hazihusiki na usimamizi wa mali za umma bali ni makubaliano ya mezani kati ya watawala wa pande mbili za mkataba ujue hatuna mahakama bali tuna viwavi jeshi.

Ukiona mahakama wanarudiarudia kwenye maamuzi yake misimamo ya serikali iliyoko majukwaani kuwa ndiyo sheria ujue hatuna mahakama

Ukiona mahakama zinaona sawa kampuni binafsi ya DP World kuwa sehemu ya mkataba wa kimataifa kwa kukebehi sheria zetu za manunuzi na mikataba bila ya kujikita ni ibara zipi za Geneva na Lome Conventions zimeruhusu hayo basi ujue hatuna mahakama.

Ukiona maamuzi yanaahirishwa ahirishwa kwa visingizio waheshimiwa wana udhuru wakati hata Msajili anaweza kuyasoma maamuzi yao basi ujue hatuna mahakama maana kuna mambo ya kichinichini yanaendelea. Ni mgao unasubiriwa kabla ya uamuzi kusomwa kama hautoki wana uamuzi kinzani upo kwapani

Ukiona mahakama inazikana baadhi ya sheria kwa vile zina makatazo na kubatilisha mkataba huku baadhi zisizo na athari tajwa wanazifanyia kazi na hivyo kujipinga pinga wenyewe basi ujue hatuna mahakama. Aidha sheria zote zahusika au hazihusiki. Huwezi kuamua za manunuzi na mikataba haziwahusu lakini za maliasili zinawahusu bila kuanisha hiyo migongano inahalalishwa na sheria zipi au maamuzi yapi ya kisheriabunge.

Ukiona mahakama inaoni juu ya nafasi ya maoni ya wananchi kuwa hata kama yangetolewa Bunge haliwajibiki kuyazingatia kinyume na kanuni za haki ya kiasili hesabu huna mahakama.

Ukiona mahakama haioni batili sisi tubebeshwe majukumu tu bila haki yoyote ujue huna mahakama. Wajibu bila haki mi utumwa. Kama mikataba midogo midogo itamaliza huo ubishi kwanini wajibu mbele ma haki baadaye? Kwanini wajibu na haki usiwemo kwenye makubaliano zije kuwekwa zote baadaye?


Ukiona mahakama inatumia kitabu (porojo) cha kada nguli wa chama tawala Pius Msekwa kubatilisha ibara ya 8 ya katiba inayosema mamlaka zote zinatoka kwa wananchi wa JMT basi ujue idara ya mahakama sasa ni dawati la dhuluma la chama tawala.

Ukiona Rais anamwongezea muda usiyo ma kikomo Jaji Mkuu ili ateue majaji wanaoegemea watawala ujue lazima ukiri kutoka sakafu ya moyo wako idara ya mahakama ni dawati la dhuluma la chama tawala.

Ukiona standing orders za bunge zinatengua ibara ya 8 katiba kwenye uamuzi wa kimahakama basi ujue huna mahakama wewe bali una kijiwe cha kulangua haki za wanyonge

Kwanini uamuzi wa Mahakama Kuu Mbeya umekiuka katiba yetu na Geneva & Lome Conventions.

Wadau kwa vile hampendi sana udadavuaji unaenda ndani sana basi tutawakilisha hoja zetu kiujumla tu.

Baada ya kuutafakarinkwa ndani uamuzi wa kimahakama kuhusiana na azimio la kibunge liloridhia uwekezaji wa DP WORLD tungependa kuainisha uamuzi wa Mahakama kuu Mbeya haukujibu khoja za walalamikaji.

Aidha kwa ujanja ujanja walizipiga chenga na kuhalalisha sheria za nchi zetu kukiukwa hususani katiba yetu, sheria zake na yaliyomo na mantiki zake za matakwa ya mikataba ya kimataifa.

Kwanza, Mahakama Kuu Mbeya imebeza na kudhihaki matakwa ya kikatiba ya misingi ya uwazi, haki na ushindani ambayo imewekwa na kishinikizwa na sheria za manunuzi, makampuni, maliasili na haki za kusikilizwa.

Uamuzi unasema sheria zetu hazitumiki katika mikataba ya kimataifa bila kutoa majibu sahihi kama pamoja ma mkataba husika siyo mkataba wa kimataifa kama tutakavyofafanua baadaye.

Uamuzi kughairi kutoa majibu kama ni sahihi kwa Kampuni binafsi kama Dubai kuwa sehemu ya mkataba wa kimataifa chini ya Geneva na Lome Conventions. Hakuna mahali popote pale

Dhdhdhdhd…..

Pili, katika hali ya kusikitisha uamuzi umetathmini katiba ya Falme za Kiarabu ili kuamua kama Dubai inaweza kuingia mikataba sahihi wakati utaratibu sahihi wa kisheria ni kutathmini kama Dubai ina sifa zilizoanishwa na sheria za kimataifa ina wasifu wa kuingia mikataba ya kimataifa na hivyo kuwa na sifa ya kunufaika na haki zilizobainishwa kwenye mikataba hiyo.

Tatu, uamuzi ulizisigina sheria za manunuzi kuwa hazitumiki kwenye mikataba ya kimataifa lakini ilipokuja sheria za maliasili waliona zinahusika na kuzichambua. Maamuzi ya kimahakama yanapaswa yawe yanazingatia kanuni moja hayawezi yakawa yana migongano kama tuliyoiona hapo. Aidha sheria zote zinahusika kwenye mikataba ya kimataifa au hazihusiki haiwezekani sheria zetu zikawa zinahusika nusunusu.

Nne, hii hoja ni mwendelezo wa khoja ya tatu hapo juu. Katika kuihalalisha kampuni ya Dubai kuwa sehemu ya mkataba mahakama kuu Mbeya ilibidi iitengue sheria ya manunuzi ambayo imeweka bayana upatikanaji wa huduma na bidhaa kwa matumizi ya serikali kuhakikisha misingi iliyomo kwenye katiba ya usawa, uwazi, ushindani na uwajibikaji izingatiwe. Mahakama Kuu Mbeya kwa kuibeza sheria ya manunuzi ambayo imepitishwa na Bunge ili kuhakikisha Katiba yetu inazingatiwa inaufanya uamuzi wake kukiuka katiba yetu ambayo wanapaswa kuilinda kulingana ma sheria zetu.

Tano, uamuzi uiikana sheria ya mikataba na kudai haihusiki wakati wanakiri mikataba midogo midogo inayojulikana kama HGAs itahusika. Sheria ya mikataba yetu inabatilisha Dubai kuingia aina yoyote ya mikataba lakini kama tulivyoona kwenye sheria ya manunuzi pale sheria zetu zikikataza Mahakama Kuu Mbeya ilizifuta na kusema hazihusiki.

Sita, uamuzi ulitengua kanuni za haki ya kisikilizwa ambazo zinakataza kuhisia maamuzi ambayo hayajafanyika lakini uamuzi huu ulidiriki kudai mapungufu ya ushirikishwaji wa wananchi yasingetengua azimio la kibunge. Hizi ni hisia ya kimahakama na hakuna mahali popote kwenye uamuzi wao ambapo walitoa ushahidi wao kuthibitisha maoni yao kuwa utaratibu wa kusikilizwa usingebadili.misimamo ya bunge juu ya azimio lao.

Saba, uamuzi ulijikita mno kwenye maamuzi ambayo yanahalalisha bunge kutowajibika kwa wananchi wake na maamuzi waliyoyatumia ni hasa ya India, Uingereza na Afrika ya Kusini bila ya kufanya jitihada yoyote ya kuona kama katiba zao zina Ibara za uwajibikaji wa bunge kwa wananchi kama zetu. Mfano uingereza wanazo sheria zinazohitaji kura ya maoni kama kujitoa EU na yapo maamuzi kwenye hilp sisi hatuna sheria ya maoni kama hiyo, India ni nchi inayoendeshwa na majimbo na kuongezwa ushirikishwaji kinyume ma sheria zetu. Pia Afrika ya Kusini ni kama India. Hivyo, haikuwa sahihi kwa Mahakama Kuu Mbeya kudabua maamuzi ya mahakama ya nchi tajwa nila ya kujihakikishia mazingira yao kweli kiuhalisia yanashabihiana na ya kwetu

Nane, uamuzi haukufanyia kazi misingi ya haki, utu, ushirikishwaji, ushindani, uwazi, uwajibikaji na usawa iliyomo kwenye makubaliano ya Kimataifa ya Geneva na Lome.na ulichukulia kijuujuu tu kuwa ilifuatwa jambo lilichangia sana kupindisha haki.

TUONAVYO.

Uamuzi huu umeonyesha mahakama zetu haziko huru maamuzi yake kila wakati hupendelea serikali.

Haya ni matatizo ya kimfumo ambao umehakikisha unayemshtaki kwa kukiuka haki zako ndiye anateua majaji kwa vigezo ambavyo jamii haivijui na huchagua ni majaji wapi wasikilize shauri lako kupitia Jaji Mkuu ambaye jamii hata haijui alipatikanaje.

Matokeo yake pamoja na katiba kuwapa raia haki za kuwajibisha serikali yao lakini katiba hiyo hiyo imewapa watawala mamlaka ya kufanya watakavyo


 
Tanzania hakuna mahakama.... evidence:: hakuna tajiri utamkuta selo au gerezani
Ukiangalia jinsi zinavyotafuna hela yetu na kazi hovyo hovyo namna hii ndiyo maana kwenye umasikini hatutoki.


Tutaimba kuutokomeza umasikini lakini kwa huu upeo hatutoboi tutabaki hapa hapa tulipo au hata kurudi nyuma
 
Mahakama Ile na majaji wale ni machoko hovyo kabisa
Sijawahi kuona uamuzi wa mashauri ya kikatiba unaokiuka katiba yetu kama huu.

Inaelekea uwezo wa mahakama kuu kuyaamua mashauri ya kikatiba umepungua mno.

Nilitarajia kubatilisha sheria zetu wangelitumia katiba yetu lakini wao wameikweza katiba ya Falme za Kiarabu ikawa juu ya katiba yetu na sheria zake na ikawa juu ya matakwa ya mikataba ya kimataifa kinyume na sheria na isivyo halali
 
Wewe mpuuzi Hayati Mchungaji Mtikila alishinda nini? Usidhani kila mtu ni mjinga mjinga kuburuzwa na nyie wazee wa pinga kila kitu
Kama Mtikila angelishinda kitu mgombea binafsi yuko wapi?

Ninashukuru nimeanza polepole kuelewa uzezeta wako kwenye fani ya sheria
 
Wabongo wanawaza haya

Screenshot_2023-08-08-11-20-10-1.jpg
 
Back
Top Bottom