Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

  • Ni Nzuri

    Votes: 205 58.4%
  • Ni Mbaya

    Votes: 147 41.9%

  • Total voters
    351
Naona speech ya Bwana Spika ingefaa ndio iwe ya Rais maana katumia dakika chini ya 10 lakini kaongea mambo mazito na yenye kuleta faraja kwa waTZ. Bora hii nchi iongozwe na Bunge chini ya spika kuliko Muungwana na Baraza lake la Mawaziri
 
Imerejesha Imani kwangu kwamba ufisadi utaendelea kutesa na wala hatujui tunapoelekea maana tumeshaanza kuchanganyikiwa wenyewe!
 
mwenzenu... nimeamua kurudi kuandika hadithi zangu na visa vya kufikirika; sidhani kama mimi na Kikwete tunaishi sayari moja.
 
Msanii ni msanii tu blah blah ndani ya msaa 3 na nusu kisha kaondoka zake.Huku nyuma katuachia mjadala mzito sana.
 
Nasema walau Raisi Mkapa alikuwa anatoa data za kumwezesha mtu kuchambua mambo. Hapa kwa masaa zaidi ya 3 porojo tuu!!! mtu utachambua lipi? maana hata aliyosema mwanzo mtu umeshasahau. Hii inasikitisha sana. Watanzania kazi tunayo, tena kubwa sana.

Tunahitaji mwelekeo mpya kabisa, ambao katika hii hotuba sijauona hata kidogo. Ndio Tunajua tumetoka wapi, Tulipo tunapajua (kwani machungu yake ni makubwa), sasa tuonyeshe wapi tunaelekea, hakuna kitu.

Jamani nasema huyu dereva wetu sio kwamba tu hajui njia ipi yakupita (ambalo ni tatizo dogo tu, akikubali kupokea ramani) bali hajui wapi tunapokwenda. Hivyo tatizo kwake sio njia bali ni wapi atupeleke. Huu ni muda muafaka wa kumwambia akae pembeni maana akifitufikisha pabaya hata ukimwondoa na gari tunaweza tusiwe nalo tena.

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake, waone ya kwamba dereva hafai ni wakubadilisha
 
wanacho fanya serekali kwenye issue ya maendeleo ni pale wanapo kuwa na maslahi binafsi, lakini nia binafsi au hatua binafsi hakuna, mfano suala la mafuta sio lazima tuingie opec, ili mradi hiyo reserve ya mafuta iwe economical viable, kuhusu chuo cha bugando nafikiri haikuwa vizuri kwa raisi mzima kusema, ukimsifia mtu unapewa, je watu wake wakimpa taarifa hiyo mwenye kuchangia, itakuwaje?

JMK ataweka sura yake wapi? si vizuri raisi wetu aonge mambo ya mtaani kwenye serious issue kama hizo.
 
mwenzenu... nimeamua kurudi kuandika hadithi zangu na visa vya kufikirika; sidhani kama mimi na Kikwete tunaishi sayari moja.

Mwanakijiji,

Can you read that speech again?unaweza kuna na nguvu kusoma mambo hayo?

makofi..kamaliza,hakutegemea kusema kiasi hiki,anasema amekuja kuwapa tarifa kule alikotoka na mpaka ha tulipo.mambo ambayo hajayazungumzia ni kama yafuatayo

1.Suala la RICHMOND,Je pesa za RICHMOND nani alilipwa na ripoti ya kamati ya kina mwakyembe walilipwa pesa nyingi ila hajaona effect yake.

2.Nafikiri sasa ,Lowasa anaweza kurudishwa madarakani ,Tuendelee kumpa ushirikiano

3.Suala la DOWANS,hajaelezea nini kifanyike.

4.Suala la Kamati ya Madini ya kina,Je nini kitafanyika na Ripoti alipewa na alimpa waziri wiki mbili alifanyie kazi na mapendekezo..muda ulishapita ila hatujaona chochote

Mungu mbariki Rais Wetu,Mbariki Jakaya kikwete.
 
Ngoja sasa tusikie mafisadi wa kilimo mana hela ndio hiyoo kwenye mikopo ya wakulima,sasa sitoshangaa kusikia fisadi akitokea kwenye sekta ya umwagiliaji wa vitunguu!
 
Dusikutegemea kabisa!alipoanza kuongelea EPA sauti ilikua inatoka kubwa/ya ukali flani hivi nikajua wa epa mwisho wao umefika!eh kutahamaki nikaishiwa nguvu yaani hakuna jipya zaidi ya kujifagilia tuuuuuuuu eti kimpira sasa tz ni kinyozi si kichwa cha mwendawazimu tena!yaani kaniboa kwa ufupi
sijaipenda hotuba yake 'ya mwezi huu'
 
Hakika sikuyaamini masikio yangu baada ya Hotuba ndefu ya Mr President iliyochukua takribani masaa manne 4 lakini ikiwa imebeba upupu. Hotuba hii imekuja kufunikwa na Hotuba ya Bwana spika iliyochukua chini ya dakika kumi ikiwa imebeba ujumbe mzito wenye matumaini.

I dont understand what type of this president we have na sijui kama tutaweza kuvuka katika dhahama hizi. Any way sijui wana JF mnamchukuliaje Mr president wenu
 
Back
Top Bottom