Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,498
- 40,045
mzee mwanakijiji na wengine humu forum,
kuna uwezekano wowote wa kuipata hii hotuba live?
Nina mpango wa kuirusha live...
mzee mwanakijiji na wengine humu forum,
kuna uwezekano wowote wa kuipata hii hotuba live?
Jamani hebu semeni muda na sisi tuliko mbali tusikilize. J
Sasa hii source yako ya habari mbona ime-base kwenye sehemu moja tuu, nashindwa kushawishika kwamba muungwana ataongelea swala moja tuu, halafu kama nitakuwa sikosei hotuba hiyo source wako amekupa kwenye copy iwe soft au hard kwa kuwa haiwezekani katika chit-chat ukawa na uwezo wa kukumbuka takwimu zote hizo, sasa kama ni hivyo basi imwage hiyo hotuba janvini, waungwana waione na waijadili........kama tarehe imekosewa wasiliana na Mwanakijiji.
Itaanza muda mnfupi baada ya saa 4 kamili kwa saa za afrika mashariki
Pole sana Kijunjwe hivi ulishawahi kumwona rais wako akiwa serious? Au haya yanayofanyika ndo unayaona kuwa ni seriousness.................kwa mtazamo wa haraka, nadhani source yake iko katika mchango waliopeleka TAKUKURU Ikulu kwa ajili ya hotuba. Haingii kichwani hotuba yote ikajaa taasisi moja tu.
...pili sitaki kuamini kuwa JK hatakuwa makini kiasi hicho cha kwenda kuhutumbia bunge na Taifa kwa ujumla juu ya TAKUKURU tu.
Where do we go to subscribe?
Mambo Jambo huyu jamaa amejivua nguo kuwa ni mtu wa ndani ya TAKUKURU tena ngazi ya Ukurugenzi, kwa kuwa amehusika katika kupitisha takwimu zilizotakiwa na IKULU katika draft speech yao, ambayo si lazima wazitumie katika kuandika speech. Angekuwa makini kidogo angefanya uchambuzi hata wa EPA ili angalao kuonyesha kwamba hatoko TAKUKURU.
Mhusika huyu mwenzetu hapa JF, amekuwa na mchango mzuri sana katika kutoa taarifa za kusaidia mapambano dhidi ya ufisadi ikiwa ni pamoja na ile taarifa ya ununuzi wa nyumba ya Mkurugenzi Mkuu wake, Edward Hosea, lakini pia alichemsha kwa kushindwa kuficha nyayo zake hadi akajulikana.
Awe anawasiliana na watu kama kina invisible ama mwanakijiji kabla ya kupost ili wamsaidie kuweka bila kuacha nyayo.
Kwa taarifa ni kwamba KESHO KUNA KISHINDO
KLHN inatarajia kurusha matangazo ya hotuba ya Rais "Live" kutoka Dodoma kwa subscibers na wachangiaji tu . To offset gharama ya matangazo hayo ya muda mrefu tunalazimika kufanya hivyo. Kwa wengine wataweza kuisikia vipande vyake baada ya kuirekodi na kuihariri.
Tuko pamoja.
Hapana ingia pale kwenye klhnews.com kuna mahali panasema "Support KLHN"... NN.. haka kajarida tu leo kameshusha site kwa sekunde chache.. sasa hotuba ya Rais ambayo anaweza kuvunja Bunge na kurudi kwa wananchi kupata new mandate na viongozi wapya kabisa si ndio itakuwa kasheshe..?
Mwanakijiji,
..hivi Raisi wa Comoro hayuko ktk msafara wa kulihutubia Bunge?
..huyo nadhani atatupotezea muda wa kujadili masuala ya taifa letu.
..kama anataka kushukuru mchango wetu bora angezungumza na maofisa na wapiganaji wa JWTZ sehemu kama Lugalo au Uwanja wa Taifa.
Kikwete hana pengine kwa kwenda isipokuwa juu!