Tanzania na tishio la migomo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania na tishio la migomo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mhache, Sep 9, 2008.

 1. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Serikali ya awamu ya nne imepata misukosuko mingi sana. Sina maana kwamba serikali zilizotangulia hazikuwa na misukosuko kama hiyo. Ilikuwepo kwa kiwango chake. Maamuzi yanayogusa maisha ya watu yanafanywa bila kufanyika kwa utafiti wa kina. Kwa mfano wafanyakazi wanatakiwa kupandishwa vyeo ambavyo vyeo hivyo hutakiwa kufuatwa na fedha kiasi fulani. Ni kwa nini kitengo kinachohusika kisiwe na maandalizi ya kutosha ili kukwepa matatizo yanayoweza kujitokeza likwepo suala la migoma isiyokuwa na tija.

  Migomo imekua kila kukicha ikiwa ni suluhisho la wahusika kupata ufumbuzi wa matatizo yao. Kwa mfano tishio la walimu kugoma. Zoezi hili limewezesha walimu kadhaa japo sio wote kupata haki yao. Muhimbili wametishia kugoma, jana serikali imetoa tamko tarehe ya kuwalipa madai yao 23/09/2009. Je tumekuwa kama kichwa cha wenda wazimu? Serikali ni lazima iamshwe kwa matishio ya migomo ndio haki itoke.
   
 2. m

  mwalimu Jr. Member

  #2
  Nov 17, 2008
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  DAWA YA MIGOMO sio kwenda mahakamani au kuwafukuza wanafunzi shule au vyuoni bali ni kutafuta na kushughulikia vyanzo vya migomo kwa mazungumzo, mipango, mikakati na hatua za dharura.

  Kinachoonekana Tanzania hivi sasa ni kwamba Mawaziri, Makatibu wakuu,Wakurugenzi mbalimbali na wakuu wa vyuo wameshindwa kumsaidia Rais na serikali yake 'to nip in the bud' through just and desirable outcomes' matatizo mbalimbali yanayowakabili wafanyakazi na wanafunzi Tanzania.

  Au kuna mkono wa mtu au hujuma kwa maneno mengine dhidi ya Rais aliyeko madarakani. Na huyo anayehujumu anafanya hivyo kwa faida ya nani. Maana watu wameanza kusikika wakisema watahakikisha Kikwete aendelee kuwa Rais baada ya 2010!!

  Bila shaka kinachofanyika sasa ni bidii na juhudi ya kuonesha kwamba serikali iliyopo madarakani imeshindwa kazi. Je, ni kweli serikali ya awamu ya nne imeshindwa kazi. Wenyewe wanasemaje.

  Na vyombo vya habari vinaposhabikia migomo hii je, navyo vinashabikia hivyo kwa faida ya nani?

  Tuombe madaktari, manesi, polisi na jeshi nao wasije kugoma.
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi nao wagoma. Wanafunzi wamefanya fujo na kuvunja baadhi ya madarasa na samani za shule.
   
 4. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Siku za karibuni mogomo imeonekana kuwa dili na ndio njia ya pekee kudai haki yako maana hata hizo nchi tunazoziona zina maendeleo hayakuja hivi hivi ila ni kwa revolutions na kitu wanafunzi wanachofanya hivi sasa ni "REVOLUTIONISING POOR EDUCATON REFORMS".
  Tanzania tuna haki ila haupati bure ila lazima ujitume kidogo!
   
 5. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hadi walinzi wa Ikulu wakigoma ndio watashtuka an kuamka usingizini.
  That is my thinking BUT anyway they say CCM is chama safi na kimekuwa na historia safi.
   
 6. b

  bgmy Member

  #6
  Nov 17, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ndiyo ARI MPYA,KASI MPYA NA NGUVU MPYA tusishangae sana kuona hali hii ikitokea sasa kwa taarifa ni kuwa migomo itakuwa nchi nzima kuanzia chini kabisa mpaja juu kwamaana hata wananchi sasa tutaendesha mgomo kuwa hatumtaki rais wetu kwamaana ametudanganya wakati akiomba kula zetu na hakuna alichotusaidia zaidi ya kutuweka katika mazingira magumu sana kimaisha...................sasa wananchi tunatakiwa kuweka nguvu pamoja ili tujikomboe..............
   
 7. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Anayegomewa wajiwajibishwe/au ajiwajibishe kama yeye ndo kashika makali

  vinginevyo tunakoenda hadi Rais atagoma na ikitoka hapo ni kwa wanajeshi wote nao watagoma ili nchi inoge zaidi.
   
 8. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Serikali: Migomo inafadhiliwa na Wazungu  SERIKALI imetoa siri ya kuwapo kwa migomo nchini kwamba imekuwa ikiandaliwa na kufadhiliwa na Wazungu.

  Kauli hiyo imetolewa juzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selina Kombani.

  Bila kutaja majina ya Wazungu hao, Kombani alisisitiza kuwa ufadhili wa raia hawa wa Kizungu katika migomo hiyo, umelenga kulipunguzia uwezo taifa na kutaka kurudisha utawala wa kikoloni kwa Watanzania.

  Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Geita mkoani Mwanza, baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya katika Kata ya Katoro, wilayani humo, Waziri Kombaini alisema serikali inasikitishwa na kukasirishwa mno na ufadhili huo wa migomo.

  Alisema kutokana na hali hiyo kamwe Serikali ya Tanzania haitavumilia vitendo hivyo vya uchochezi na kuahidi kuwachukulia hatua wahusika.

  Akitolea mfano wa uthibitisho juu ya hilo, Kombani alisema wiki iliyopita wanafunzi wa Chuo Kikuu sehemu ya Mlimani waligoma, kisha kufukuzwa chuoni lakini wafadhili wa migomo hiyo waliwapelekea usafriri wa magari kwa ajili ya kuwarejesha makwao.

  “Wapo watu wanaochochea vitu hivi vya kijinga vya migomo wakiwemo Wazungu.

  “Mlishaona wapi Wazungu wakishiriki maandamano, lakini hapa nchini, Wazungu wamekuwa wakishiriki maandamano na hawa ndio wafadhili wa yote haya,” alisema Kombani.

  Waziri Kombani alitumia pia wasaa huo kulaani na kuwatunishia misuli walimu kupitia Rais wao wa Chama cha Walimu nchini(CWT) Gratian Mukoba, juu ya msimamo wao wa kuendeleza migomo leo.

  Alisema serikali ikichoshwa na migomo hiyo ya walimu, itaanza kuwapandisha kizimbani mwalimu mmoja baada ya mwingine kujibu mashitaka ya kushiriki mgomo.

  “Walimu wasidanganyike kuendesha migomo, tutawafikisha mahakamani kujibu mashitaka na wala hatutakishitaki chama cha walimu,” alisema.

  Kwa mujibu wa Kombani, serikali ilishaandaa malipo ya madai yao na kwamba itawalipa wale tu wanaodai kihalali na si walioghushi vyeti na wasio na uhalali wa kulipwa fedha hizo.

  Wiki iliyopita Rais wa CWT nchini, Mukoba, alitangaza mgomo wa walimu nchi nzima ambao unaanza leo licha ya serikali kuzuia mgomo huo na kukimbilia mahakamani kama ilivyofanya hapo awali.

  Kuhusu mafisadi wa EPA, Waziri Kombani alimtetea Rais Jakaya Kikwete kwamba amejitahidi hadi kufanikisha kuwafikisha mahakamani.

  Waziri Kombani alisema serikali haiwezi kuona na kufumbia macho watu wanaoligharimu taifa kwa kuchota fedha za umma kwa manufaa yao binafsi.

  Alisema fedha nyingi zilizoibwa katika Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje (EPA), zimeanza kurejeshwa na tayari zimeanza kutumika kwa ajili ya maendeleo ya taifa, ikiwemo ununuzi wa pembejeo na dawa kwa wakulima.

  “Vijesenti vilivyoibwa na hawa mafisadi vimeshaanza kurudishwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na tayari watuhumiwa wameshaanza kufikishwa mahakamani,” alisema.

  Kombani alisema wanaopuuza na kudharau hatua iliyofikiwa na serikali chini ya Kikwete ya kuwaburuza mahakamani mafisadi hao, wana ajenda ya siri na kwamba ni vema watu hao wakapingwa kwa nguvu zote kwa mawazo na ushawishi wao.

  Kwa upande mwingine, Kombani aliwataka watumishi wa serikali za mitaa kutoendekeza vitendo vya ulevi kazini kwani serikali itaanza kuwachukulia hatua watakaobainika kuendekeza vitendo hivyo.

  Alisema Tanzania haiwezi kugeuzwa kuwa kiwanda cha bia kwa watumishi wake kuendekeza vitendo vya ulevi na kusisitiza kuwa mtumishi atakayebainika, ajiondoe mwenyewe ili akaungane na walevi wenzake.

  “Serikali yetu haiwezi kuvumilia vitendo vya kilevi vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri na Serikali za mitaa, yeyote anayeona hali hiyo inamfaa, aache kazi akajiunge na walevi wenzake, hatuwezi kukubali Tanzania igeuzwe kuwa kisiwa cha walevi,” alisema.

  Aliwataka madiwani kuepuka migongano na migogoro inayohatarisha maendeleo ya nchi na kutolea mfano wa madiwani wa Geita kwamba wamekuwa na mshikamano na ndiyo wilaya inayopata mafanikio kwa kasi.


  By:-
  Tanzania Daima

  My Take:-

  Kauli hizi za mawaziri wetu zinanifanya nijiulize maswali mengi, labda umefika wakati wa kutangaza kazi za uwaziri, naibu waziri na makatibu wakuu wa wizara kwenye magazeti ili watanzania walio na vigezo waweze ku-apply na kupewa kazi hizo, haya mambo ya kupeana peana ndiyo yanasababisha mambo ya ajabu ajabu kama haya, inasikitisha kwa waziri kutoa hotuba kama hii...

  Geita/Tanzania stand-up!
   
 9. M

  Mama JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  hata hizo nafasi zikatangazwa, nani atasimamia usaili? si watakuwa wale wale?
   
 10. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #10
  Nov 18, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Huyo hana sifa za kuwa waziri kwanini anatoa kauli kama hizi na kukimbilia mafichoni anakata simu hataki kuongelea kauli hizo anazozitoa ? Kwani wale wazungu sio wanafunzi ? Sio watanzania ? Au hakuna wazungu watanzania ?
   
 11. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  style ya Mugabe hii, duh! hata watawala wa bongo wameamua kutumia visingizio anavyotumia Mugabe. Huyu Mama huwa anaonekana ni makini sana naona 'unga wa ndele' aka ulevi wa madaraka unamuelemea.
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Nov 18, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Eehh! makubwa huyu ni waziri anaongea hivi????????? and we keep wondering kwa nini nchi haijaendelea mpaka leo???????
   
 13. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Ukisikia kuweweseka kwa serikali ndo huku! yaani alo yasema hata mtoto wa darsa la saba aweza kutoa maelezo bora zaidi kuliko haya!

  Wazungu kutoa usafiri wa wanafunzi walio fukuzwa UDSM? halafu wakawapeleka wapi? kwani hao wanafunzi ni wa mji mmoja? uongo mwingine hauna hata maana! sana sana ni kuzidi kujidhalilisha badala ya kujikosha!
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Can anyone please post her CV? We might be dealing with another Kihiyo here! If not, may be she is among those who just went to politics to look for a job. ... I won't be surprised!!
   
 15. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Delloitte and Touche/Pricewaters...Lol!
   
 16. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mama kuna msemo unasema" kama noma na iwe noma" yaani hapo mbwa kala mbwa....tunatangaza nafasi za kazi kwenye magazeti, mtandaoni na sehemu zote....na post zenyewe ni UWAZIRI, NAIBU WAZIRI, MAKATIBU WA KUU WA WIZARA NA WAKURUGENZI NDANI YA WIZARA, baada ya hapo tunakusanya CV's zote nakufanya usaili, kama vipi tunawapa mawakala wa shughuli hizo, kama KPMG, PriceWaterHouseCo, Delloite, n.k haya mambo yakupeana positioni muhimu kama hizi kwa kujuana ni hatari sana kwa taifa letu...
   
 17. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  EDUCATION
  School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
  Institute of Development Management, Mzumbe M.A in Public Administration 1992 1994 MASTERS DEGREE
  Institute of Development Management, Mzumbe Diploma 1982 1985 ADV DIPLOMA
  Tabora Girls' Secondary School A-Level Education 1979 1981 HIGH SCHOOL
  Kilakala Secondary School O-Level Education 1975 1978 SECONDARY
  Kwiro Primary School Primary Education 1968 1975 PRIMARY

  --------------------------------------------------------------------------------
  CERTIFICATIONS
  Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
  No items on list

  --------------------------------------------------------------------------------
  EMPLOYMENT HISTORY
  Company Name Position From Date To Date
  Prime Minister's Office (Regional Admin & Local Govt.) Minister 5/12/2008
  Prime Minister's Office (Regional Admin & Local Govt.) Deputy Minister 2006 5/12/2008
  Sokoine University of Agriculture Principal Administration Officer 1995 2005
  Morogoro Canvas Mill Manager 1994 1995
  Kilosa District Council Officer 1985 1992

  --------------------------------------------------------------------------------
  POLITICAL EXPERIENCE
  Ministry/Political Party/Location Position From To
  Chama Cha Mapinduzi - CCM UWT Chairperson (Morogoro District) 2002 2005
  Chama Cha Mapinduzi - CCM UWT Implementation Committee Member - Kilosa 1987 1992  PUBLICATIONS
  Description
  Published Date
  No items on list

  --------------------------------------------------------------------------------
  SPECIAL SKILLS
  Skill Name or Description Years Experience Acquired Through Skill Level
  No items on list
   
 18. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #18
  Nov 18, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kuhusu mafisadi wa EPA, Waziri Kombani alimtetea Rais Jakaya Kikwete kwamba amejitahidi hadi kufanikisha kuwafikisha mahakamani.

  Waziri Kombani alisema serikali haiwezi kuona na kufumbia macho watu wanaoligharimu taifa kwa kuchota fedha za umma kwa manufaa yao binafsi.  “Mkulo asema fedha za epa hazikuwa za Serikali wala BoT” - Gazeti la Mwananchi na Habari Leo, Jumamosi tarehe 21.06.2008),

  Hawa ndiyo mawaziri wetu.
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Nov 18, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Thank you so much.

  Everything confirmed. Education .... may be ok; but political leadership experience... almost NILL. She needed to become at least a DC and not even a deputy minister! May be mambo jambo came to work in this case... That's Bongo; kila kitu kinawezekana. Hata kenge anaweza kuwaongoza mamba!!
   
 20. M

  Mama JF-Expert Member

  #20
  Nov 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  hao ni kina nani watakaofanya? jibu ni wale wale! Unless mageuzi ya haraka yatokee.
   
Loading...