Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,169
- 10,787
"Hii ni ndoto ya mchana"- BWM
Afadhali una uwezo huo wa kuona kuwa ni ya mchana inawezekana ikawa sindoto kwa sababu ni mchana ,yanaweza yakawa maono!!!
"Hii ni ndoto ya mchana"- BWM
Nilishaongea hapa kwamba mabadiliko ya kitaasisi (katiba, kukua kwa utawala wa sheria, utamaduni wa ufuatiliaji kwa watu wote etc) ni muhimu kuliko mabadiliko ya watawala. Kama anakuja rais mwingine akakuta katiba ya sasa ambayo inamfanya rais kuwa mungu mtu fulani, ukweli utabaki kuwa kama hatatumia vibaya nguvu hizo atakuwa anatufanyia hisani tu.
Dawa ya kuondokana na uwezekano wa kukutwa na urais wa Kikwete mwingine ni kuwa na taasisi zenye misingi madhubuti katika utawala wa sheria. Najua hili linaweza kuwa ni lengo la muda mrefu na kwa muda mfupi tunaweza kutaka kumuondoa Kikwete tu, lakini vile vile tuangalie Kikwete anaendesha mambo yake katika mfumo na utamaduni gani, tukiweza kuuondoa huu mfumo wa "top down" na utamaduni wa kuogopana tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana.