Ukiachana na ujinga, maradhi, na umasikini, Unafiki ndio tishio zaidi Tanzania kwa sasa

Youngblood

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
18,959
55,054
Mwalimu Nyerere alianzisha vita dhidi ya maadui watatu; ujinga, maradhi na umaskini. Alikuwa na maana kwamba ikiwa Tanzania itaweza kupigana na maadui hao watatu kwa mafanikio, basi nchi hii ingeligeuka kuwa kisiwa cha maendeleo na maisha ya hadhi ya juu sana duniani.

Lakini tofauti na matarajio yake hata kabla hatujafika mbali ameongezeka adui namba nne( 4) UNAFIKI

Mwalimu alisema,UTII ukizidi unakuwa UOGA,uoga huzaa UNAFIKI na Kujipendekeza.

UNAFIKI- ni tabia ya mtu kujivika sura mbili tofauti kwa nyakati moja lakini kwa mahali tofauti tofauti kulingana na muktadha (context) husika. Lengo kuu la kufanya hivyo ni kutaka kuharibu uhalisia wa jambo fulani kwa kificho,lakini aonekane mwema mbele za watu

Wasomi kibao tunao ,tena wengine wameishi na kusoma nje ya nchi hii lakini wanayofanya ni matatizo matupu, sababu kubwa ni kujipendekeza na unafiki

Ujinga unaweza kuchangia umaskini na maradhi kwa mfano,Ukosefu wa ufikiaji wa elimu na habari unaweza kuzuia uwezo wa watu kupata kazi zinazolipa vizuri na kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kiafya

Vivyo hivyo kwa Unafiki, unafanya hata mapambano dhidi ya maadui hawa watatu usifanikiwe kabisa, kwasababu watu wanakuwa waoga kutoa mawazo yao,wanajipendekeza ili wapate nafasi za uongozi,wakipata watashindwa kufanya maamuzi au kuweka sheria zenye maslahi mapana kwa nchi sababu ya uoga wabkutolewa katika nafasi walizopo.

Viongozi wanafiki wanashindwa kufanya mambo kwa kuogopa kuonekana wabaya,au kuonekana wapo tofauti na wengine,hii husababisha watu kufanya kazi bila morali au bora liende.

Mafisadi wanakula pesa za nchi lakini wanashindwa kuwajibishwa sababu ya unafiki na kuoneana huruma.

Wafanyakazi wanashindwa kudai maslahi yao kwa kukataa kuonekana vimbelembele,rejea kipindi chwendazake, wafanyakazi waliteseka kwa kupindi cha miaka sita bila kutoa neno lolote.

Viongozi wa vyama vya upinzani wanajua kabisa tatizo lililopo katika sheria za uchaguzi lakini bado wanashiriki, kwasababu ya maslahi yao binafsi.

Viongozi waliopo serikalini wanaona kabisa shida iliyopo katika katiba yetu lakini hawataki ifanyiwe marekebisho kwasababu inawanufaisha wao binafsi.!



Ciao . Weekend njema.
 
Back
Top Bottom