Tanzania na tishio la migomo

Thank you so much.

Everything confirmed. Education .... may be ok; but political leadership experience... almost NILL. She needed to become at least a DC and not even a deputy minister! May be mambo jambo came to work in this case... That's Bongo; kila kitu kinawezekana. Hata kenge anaweza kuwaongoza mamba!!

Unless we are ready to face up na kukubali kwamba education level in Tanzania is NIL hatutaendelea. Watu wanaendea vyuo vikuu na kupata hata Masters lakini hawana chochote cha maana wanachokijua na kukifanya.
We have neglected our higher learning institutions for too long na hivi sasa they are on the verge of collapse. Mtu akitoka na digrii UDSM kwa kweli anatoka na ujuzi mdogo sana, and it is not the students fault. Ujinga ni kwamba people cannot afford to go abroad to study and to seek more education elsewhere so we have to strengthen our public education system....
On the other hand we have to be fair toward Mzumbe. Huyu waziri ni plain ignorant hata angesoma Harvard (kama akina Chenge) bado ujinga wake usingepungua maana ile ni mater of intelligence that is nature not nurture!
Arguments zake Waziri ni weak, unprepared and populist using rhetoric from the past century which cannot and will not work.
 
Serikali: Migomo inafadhiliwa na Wazungu

Waziri Kombani alitumia pia wasaa huo kulaani na kuwatunishia misuli walimu kupitia Rais wao wa Chama cha Walimu nchini(CWT) Gratian Mukoba, juu ya msimamo wao wa kuendeleza migomo leo.

Alisema serikali ikichoshwa na migomo hiyo ya walimu, itaanza kuwapandisha kizimbani mwalimu mmoja baada ya mwingine kujibu mashitaka ya kushiriki mgomo.

“Walimu wasidanganyike kuendesha migomo, tutawafikisha mahakamani kujibu mashitaka na wala hatutakishitaki chama cha walimu,” alisema.

Jana katika jiji la Dar es salaam wanafunzi wa shule za msingi waliandamana mpaka ofisini kwa mkuu wa mkoa ili kushinikiza walimu wao walipwe mdai wanayoidai serikari.....halafu waziri wetu anakuja na hadithi za aina hii....hivi wajukuu zake atawaambia nini?..
 
May be misquoted she is one of the best ministers in jk cabinet

Why do you say she is the best? What has she done so far? .

She might have been considered so because she used not to speak in public for sensitives national issues like these.

Which is worse….saying something and wishing you hadn’t or saying nothing and wishing you had? In most cases, silence hides someone's low levels of IQ!
 
This nation is almost collapsing! Nothing is happening, everything has come to a stand still.

Mawaziri hawajui la kufanya kwa kuwa mkubwa wao wa kazi naye hajui la kufanya!
 
Mama kombani si mtu wa majukwaa wala midahalo, huo ndio ukweli usiopingika. Ni product ya vita ya mkapa na matajiri wa morogoro, maana tangu 2000 na 2005 mkapa aliwaumiza matajiri wote walionyemelea ubunge mkoani morogoro akianzia na abood, mwarabu yule wa mikumi na kimetule aliyeshinda kura za maoni ulanga mashariki 2005 lakini akapitishwa mama kombani, ujio wake ktk siasa na hasa hizi kubwa ulichagizwa sana na mjumbe wa nec by then na makapa akaafiki mapendekezo ya kada mwenzake.

Lakini ni mwenyeji wa vikao vya suwasa ambavyo dkt. Nchimbi na kamara waliviendesha pale kumjenga muungwana.

She is well connected na utawala huu na ndiyo kisa cha kupaa kwake kwa kasi ktk siasa za nchi.

Msisahau kuwa chief of protocol wa sasa na yeye ni wamoja hasa.

Upungufu uliojitokeza ni kile nilichosema kuwa mama yangu kombani si mtu wa majukwaa kama waliomleta ktk siasa, lakini pia wasaidizi wake hawakuwajibika ktk kumshauri mambo ya muhimu ktk " do & don'ts"

she is a good woman, leader and ccm.

Kaya kumhera mhaja wangu.
 
tunategemea 40% ya bajeti yetu kutoka kwa wazungu,ndio maana kisura kila siku kiguu na njia kuomba omba kwa hao wazungu.labda baada ya kikao cha nec sera imebadilika sina hakika.

watanzania wa leo sio wale wa mwaka 47,ni watu wenye akili zao na upeo mkubwa wa kuelewa mambo.hasifikiri kwenda kusemea geita akadhani habari hii haita julikana basi kaliwa wa chuya.

celina bora sasa upumzike watanzania hasikilizi hadithi bali wanataka vitendo.
 
CV yake huyo Kombani ni ya kawaida sana. Kwanza kwa wale mliosoma nae hizo diploma na masters alipata grade gani with hons or kwa mitulinga???? Mimi si mind sana mtu amesoma ana degree au masters kama hizo amezipata kwa kukremu. Unajua watu waliokubuhu kwa creaming ikipita siku au masaa wanasahau kila kitu!!!!! Ndo maana philosophers wanakuambia kitu ulichofundishwa miaka hiyo since seven years till say level of Phd kile unachokumbuka tu kwa leo ndicho ulichoelewa!!!! Ni wangapi tuseme wakiletewa mitihani ile ile uliyofanya first degree ukapat A leo ukifanya utapata D??? Fahamu hiyo D ya sasa ndicho ulichoelewa wakati ule na mengine ulicream wakati ule ili ufaulu mitihani!!!!!

Sioni kama huyu mama alipata post aliyo nayo kwa kuwa ati ame excel sana kielimu!!! Serikali ya sasa imebeba maswahiba na close relations za maswahiba na si watendaji so sishangai still speeches of this nature? How can someone anaweza sema ati migomo inafadhiliwa??? Bila kuona the reality ili aweze kumshauri vema Rais wake? Hapo wengi wanataka kujipendekeza ili aonekane mwenzetu bila kukubali hali halisi. viongozi kama hao ni wanafiki sana, tena wasaliti.

Tafadhali awe specific with evidence kuwa wazungu wanafadhili migomo ili waweze kumfungulia mashitaki. Anawadhalilisha wazungu wakati mkuu wao anazunguka na bakuli la kuomba misaada nje kila siku ambayo sijui inakwenda wapi wakati wananchi wana starve? Au ni za maandalizi ya campaign 2010? Pengine ameshapata za kutosha ndo maana hata maswahiba wa EPA waliomuweka madarakani anawafunga sasa au tuseme amewaabisha? Na kwa mantiki ya kupata enougn resources in the Bakulu to finance 2010 elections hajali tena!!!! Hii ni my personal view and analysis!!!!

Anyway, 2009 kampeni rasmi zinaanza kwa speed ya 60, early 2010 speed ya 80, and mid 2010 mpaka uchaguzi speed ya 160. Yangu ni macho na masikio!!!! Wengine watakuwa speed 0-59, poor them!!!
 
Mkuu sikubaliani na wewe kwa asilimia 100.Hivi kwanini watu wanapenda kumtathmini mtu kwa jinsi alivyofaulu darasani.kwa mfumo wetu wa elimu,ambao unamfanya mwanafunzi afurahie alama za darasani badala ya jinsi alivyoelewa na kufainyia kazi hiyo elimu ndiyo hapo tunazalisha mafisadixmafisadiXmafisadi.Sidhani kama huu utumwa wa kumjaji kiongozi kwa elimu yetu ya kimangaribi ndiyo utakao tukomboa.hapo waziri kachemka kamchemka tu au ni mambo ya kisiasa zaidi kuliko tunavyo hukumu hapa.
 
Mama kombani si mtu wa majukwaa wala midahalo, huo ndio ukweli usiopingika. Ni product ya vita ya mkapa na matajiri wa morogoro, maana tangu 2000 na 2005 mkapa aliwaumiza matajiri wote walionyemelea ubunge mkoani morogoro akianzia na abood, mwarabu yule wa mikumi na kimetule aliyeshinda kura za maoni ulanga mashariki 2005 lakini akapitishwa mama kombani, ujio wake ktk siasa na hasa hizi kubwa ulichagizwa sana na mjumbe wa nec by then na mkapa akaafiki mapendekezo ya kada mwenzake.

Lakini ni mwenyeji wa vikao vya suwasa ambavyo dkt. Nchimbi na kamara waliviendesha pale kumjenga muungwana.

She is well connected na utawala huu na ndiyo kisa cha kupaa kwake kwa kasi ktk siasa za nchi.

Msisahau kuwa chief of protocol wa sasa na yeye ni wamoja hasa.

Upungufu uliojitokeza ni kile nilichosema kuwa mama yangu kombani si mtu wa majukwaa kama waliomleta ktk siasa, lakini pia wasaidizi wake hawakuwajibika ktk kumshauri mambo ya muhimu ktk " do & don'ts"

she is a good woman, leader and ccm.

Kaya kumhera mhaja wangu.
 
Mkuu sikubaliani na wewe kwa asilimia 100.Hivi kwanini watu wanapenda kumtathmini mtu kwa jinsi alivyofaulu darasani.kwa mfumo wetu wa elimu,ambao unamfanya mwanafunzi afurahie alama za darasani badala ya jinsi alivyoelewa na kufainyia kazi hiyo elimu ndiyo hapo tunazalisha mafisadixmafisadiXmafisadi.Sidhani kama huu utumwa wa kumjaji kiongozi kwa elimu yetu ya kimangaribi ndiyo utakao tukomboa.hapo waziri kachemka kamchemka tu au ni mambo ya kisiasa zaidi kuliko tunavyo hukumu hapa.

Uwezo wa mama Selina Kombani, ni Mdogo sana hili halina ubishi... ukifatilia alipokuwa Kilosa na hata SUA kama afisa utawala utapata jibu. Alipogombea ubunge alikuwa alishindwe lakini Muungwana alimsaidia sana kwenye kampeni kule Mahenge maana alienda kabisa na kubadili upepo wa kisiasa na jimbo kubaki CCM.

Alipochaguliwa waziri tunaomjua tulihisi kumbe waziri mtu yeyote anaweza kuteuliwa hiyo nafasi hata kama ni mgonjwa wa akili, Tanzania inawezekana. Kama mnakumbuka Muungwana alisema hakuna sehemu watu husomea uwaziri mmoja wa walengwa alikuwa huyu mama. Ni heri angeendelea kukaa kimya kuficha uwezo wake. Akianza kupanda mimbali basi kila kitu kitakuwa wazi.

Kwenye jimbo lake amejiimalisha sana amefungua shule na kuipa jina lake, pia amedanganya wananchi kuwajengea daraja kwenye kivuko cha Kilombero, ahadi ambayo haitekelezeki, huyu mama ameanza kuwa mfisadi na yeye. Kuna kipindi alifiwa na ndugu yake wa karibu alichukua magari ya serikali kama 8 kukiwa na ambulance za Temeke na Ilala kupeleka Msiba Mahenge, sasa wakina mama na wagonjwa waliohitaji msaada wa dharura ingekuwaje? Hawa ni mawaziri wa Tanzania. Siwezi Kushangaa kauli kama hizi kutoka kwa Selina ndivyo alivyo

Ushi wa Rombo
 
ccm wameshikwa pabaya..Kumbe ni kweli wanataka wananchi wabaki masikini na viongozi na tabaka jingine la matajiri kwa kupitia mgongo wa masikini?
Kwa hiyo wakifukuzwa ndio hawatakiwi kupewa lifti? Ni kizazi gani hawa watu wanajenga kama si cha kitumwa?
Siasa za copy and paste ccm wameziendekeza na sasa zinawatokea puani...Badala ya viongozi hao kufanya maamuzi kutokana na wakati wao wanaingia kupekuwa makabrasha na kuangalia Christian Kisanji ama Chediel Mgonja(RIP) walifanya nini wakati ule wa utawala wa mwalimu na Mwinyi...Wanarudia yale yale..Sasa masikini nani amsaidie? Fisadi? Kiutaratibu fisadi hugawa pilao na fulana na kofia, maendeleo hupati...Na sasa wameshikwa pabaya wanalia.."Mzungu, Mzungu" Hakuna atakayewasikiliza kwasababu hata EPA kama si mzungu huyo si mlitaka kutupiga bao?
Na bado si inaelekea mnataka kufanya hivyo? Kama sivyo wanafunzi mnawanyanyasa kwasababu gani?
Nawaunga mkono wanafunzi na walimu waendeleze libeneke mpaka kieleweke kwasababu huko ndiko mageuzi ya kweli yatakapoanzia, kama wale wenye kwenda shule wasipobadilika na kuwauliza viongozi wetu wanachoifanyia nchi basi hata wale wasiokwenda shule hawataweza kubadilika.
Walimu wasipolipwa mishahara yao matatizo waliyonayo hasira wanawamalizia wanafunzi..Hili ni suala la kisaikolojia, sasa wakitokea wananchi wanawaorganize kudai haki zao nyie mnaanza kulia na wazungu..Haya tuone mnakotaka kutupeleka sasa maana mmeshakuwa wakoloni wabaya sana.
 
Mfa maji haishi kutapatapa.....Mara migomo ya vyuo vikuu inachochewa na CHADEMA mara migomo nchini inachochewa na Wazungu. Ukiwaambia watoe ushahidi wa kuthibitisha tuhuma zao wanang'aa macho. Wanatafuta mtu wa kumbabikia lawama ili wao waendelee kupeta. Bahati mbaya Watanzania wameshaanza kufunua macho na kujua ukweli umelalia wapi.
 
Hao wazungu anaosema wanachangia migomo na wao wakigoma kuleta midola yao kuwafanya wao wanazunguka nchi nzima kuwahadaa wananchi huku wakiwa kwenye magari ya nguvu kuliko wanayo tembelea hao wazungu wanao waletea midola hiyo si itakuwa balaa.....
 
By the way, hii habari ni ya kutoka gazetini angalia inavyogenerate traffick hapa JF. Hii inaonyesha wengi hupenda kufuatilia na kuzijadili habari za magazetini hapa JF, lakini wengine wanazipiga vita!!!! Mwe! ama kweli kwenye wengi kuna mengi!
 
Thank you so much.

Everything confirmed. Education .... may be ok; but political leadership experience... almost NILL. She needed to become at least a DC and not even a deputy minister! May be mambo jambo came to work in this case... That's Bongo; kila kitu kinawezekana. Hata kenge anaweza kuwaongoza mamba!!

Hapa kuanzia elimu mpaka experience ni zero. Hivi Diploma na Masters ya mzumbe nayo unaihesabu kama ni academic certificate?. Hii inapaswa kuwa Certificate of attendance. Huyu Mama ni empty
 
Unless we are ready to face up na kukubali kwamba education level in Tanzania is NIL hatutaendelea. Watu wanaendea vyuo vikuu na kupata hata Masters lakini hawana chochote cha maana wanachokijua na kukifanya.
We have neglected our higher learning institutions for too long na hivi sasa they are on the verge of collapse. Mtu akitoka na digrii UDSM kwa kweli anatoka na ujuzi mdogo sana, and it is not the students fault. Ujinga ni kwamba people cannot afford to go abroad to study and to seek more education elsewhere so we have to strengthen our public education system....
On the other hand we have to be fair toward Mzumbe. Huyu waziri ni plain ignorant hata angesoma Harvard (kama akina Chenge) bado ujinga wake usingepungua maana ile ni mater of intelligence that is nature not nurture!
Arguments zake Waziri ni weak, unprepared and populist using rhetoric from the past century which cannot and will not work.

Sure! Ila hao wanafunzi, leo wanachokipigia kelele ni maisha bora kwa kila mwanafunzi. Kuna siku watu hapa jamvini walilalamikia wanafunzi wa chuo kwa kutojali. Tizama mambo yanayowafanya waandamane, halafu oanisha na yale ungetegemea wangeshiriki kikamilifu kupinga kwa nguvu zao zote. Sina hakika, elimu bora iko kwenye number gani kwenye priority list zao.

.
 
Kufuatia taarifa kwamba DIT wamegoma (Tz daima), wakidai wale wanafunzi waliofukuzwa warudishe, ni kitendo cha kishujaa kufanywa na wanafunzi. Natamani mlipuko huu wa mgomo uambukize vyuo vingine, halafu sekondari na walimu wao, tutamalizia na wanafunzi wa shule ya msingi. Mgomo utaendelea kwa wafanyakazi wa mashirika fulani wakiunga mkono waalimu,TRL, NMB... Hatimaye mgomo uwe nchi nzima, ikiwezekana mpaka wafanyakazi wa ikulu wenyewe. Usalama wa taifa na polisi nao watagoma, hakuna FFU wa kuzuia migomo na maandamano. Manesi na madaktari wataendelea na kazi yao kama kawaida huku wakiunga mkono hatua itakayofanywa na wenzao katika idara na taasisi zote.

Tutaona watu wakielekea ikulu, tutaona rais aliye waangusha watanzania kwa kujiangusha mwenyewe akitoka ikulu. Tutashuhudia nchi inapita kipindi cha mpito. Tutaona mabadiliko ya amani , hakutakuwa na vifo wala watu kuzimia, ambayo yatakuwa simulizi na fundisho kwa vizazi vijavyo.

Kutakuwa na mjadala wa taifa kuhusu mabadiliko ya katiba, yatakayotoa fursa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa kuwa kila chama kitapata nafasi serikalini kulingana na kura walizopata.

Tutaona Tanzania mpya, ambayo siku zote ni nzuri inayoharibiwa na watu wachache kwa uroho wao, kisa kwa sababu ya upole na uungwana wa watanzania. Tutaona nchi iliyobarikiwa kwa mali asili ikifaidi matunda ya uumbaji wake, kwa kila raia kufaidikia na matunda yake.Tutajua vizazi vijavyo jinsi vitakavyokuja kuisifu tanzania ya sasa kwa maamuzi haya mazito. Huku wenyewe tukifanya kazi kwa bidii kila siku pasi kuwa na chembe ya ufisadi.

Nguvu kidogo tu inahitajika sasa, kama hali ni hii migomo nchini kila mahali wataalamu mko wapi, JF je?

wakatabahu!
 
Mhadhiri asema migomo nchini Tanzania ishara ya wananchi kuzinduka
Na Geofrey Nyang'oro

MHADHIRI Msaidizi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Duce), Haruna Makandi amesema migomo inayoendelea nchini inadhihirisha kuwa amani iliyodumu tangu uhuru ilitokana na watu kunyimwa haki ya kuzungumza.

Makandi alisema hayo alipokuwa akizungumza na Mwananchi nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam alipokwenda kushuhudia maandamano ya wanafunzi wa shule tatu za msingi waliofika ofisini hapo kuishinikiza serikali iwalipe walimu madai yao.

Wanafunzi hao walisema kutokana na serikali kushindwa kuwalipa madai yao, walimu hao wamegoma kuingia darasani na kuwafanya kukosa haki ya kupata elimu waliyoifuata.

Alisema licha ya kutambua athari zitokanazo na migomo pamoja na njia mbadala za watu kutaka kuwasilisha madai yao baada ya njia za kawaida kushindikana, migomo iliyopo inaonyesha kukua kwa demokrasia.

"Watu wamechoka kuonewa wamekaa kimya kwa muda mrefu, lakini sasa wameamua kutumia njia mbadala kuwasilisha madai yao. Hali hii kitaalamu tunaiita (popular democracy) yaani demokrasia ya wengi ambayo huibuka ghafla na hudumu kwa muda mfupi, lakini huacha mabadiliko makubwa katika jamii," alisema Makandi.

Makandi alitolea mfano nchi ya Uphilipino ambayo alisema wananchi walipochoshwa na utawala uliokuwapo madarakani waliandamana na hawakujali mauaji yaliyofanywa na polisi waliokuwa Ikulu hadi walipokamilisha madai yao.

Aliitahadharisha serikali kama haitakuwa makini katika kushughulikia hali hii watu, wataendelea na maadnamano hayo mpaka bungeni na baadaye Ikulu hivyo kuondoa kabisa hali ya utulivu na amani iliyopo.

"Migomo inaonyesha wazi kuwa watu wamechoka kukaa kimya huku wakinyimwa haki zao, watu wamekuwa wakikosa nafasi ya kutoa malalamiko yao na pia wamekuwa wakikosa fursa za kusikilizwa, hali hiyo ya watu kutafuta njia mbadala ya kusikilizwa hudumu kwa muda mfupi, lakini huleta mabadiliko makubwa kwenye nyanja za utawala," alisema.

Alisema jibu pekee la kuituliza migomo hii inayoendelea hapa nchini ni kwa serikali kuwapa watu haki zao kadiri ya makubaliano waliyoafikiana.

Alitoa mfano wa mgomo wa walimu ulioanza juzi kwa nchi nzima wenye lengo la kuishinika serikali kuwalipa malimbikizo ya madai yao kwamba, kama serikali hatafanya hivyo mgomo huo hautatulia mpaka walimu walipwe haki zao.

Alisema kwa sasa vitisho siyo wakati wake kwa sababu dhana hiyo ya mabavu ni sehemu ya kuwashinikiza watu kukubaliana na matakwa ya serikali hata inapokwenda kinyume na haki zao.

Makandi alisisitiza kuwa, walimu hao wanaoendelea na mgomo hivi sasa inaonyesha wazi kuwa watu wamechoshwa na uonevu pamoja na vitisho na kwamba, kinachotakiwa kufanywa na serikali ni kuwalipa madai hayo haraka.

.........e&p...2008/11/18
 
By the way, hii habari ni ya kutoka gazetini angalia inavyogenerate traffick hapa JF. Hii inaonyesha wengi hupenda kufuatilia na kuzijadili habari za magazetini hapa JF, lakini wengine wanazipiga vita!!!! Mwe! ama kweli kwenye wengi kuna mengi!

ndugu yangu habari ni habari, cha muhimu habari iwe habari kweli na sio kujali kama iko radioni au gazetini. Vitu vya hapa JF ni makini zaidi kuliko magazetini kwa sababu source za habari zinatoa direct hapa na sio kutupa habari kupitia waandishi wa habari ambao wengine ni wachovu kwelikweli.
Lakini ukweli kama hiyo kauli imietolewa na waziri, ni jambo la kusikitisha sana, ingekuwa kwenye nchi "staarabu" kama asingetakiwa kujiuzulu basi angeona hata aibu kutonesha sura yake mbele ya watu. Kwa sababu hiyo point ni ya kitoto hata kuliko ya mtoto.
Anaposema wazungu siji maana yake nini? Na sijui kama mgomo wa walimu ulifadhiliwa na hao anaowaita wazungu. Hii inaonesha kwa upande fulani uwezo wake kiuongozi.
 
Back
Top Bottom