SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,843
- 1,841
Wana bodi nikiri ni miaka mingi nimepotea humu. Wale mlionimiss mniwie radhi. Mods pia acha kuunganisha uzi wangu na mingine isiyohusiana na maswala haya nayoyaongelea.
Turudi kwenye Mada:
Siku ya tarehe 24 March 2013 (Jumapili) Rais Xi Jinping aliwasili nchini Tanzania akitokea Urusi alikofanya ziara ya kwanza baada tu ya kuapishwa kuwa Kiongozi wa China, na kupokelewa kwa shangwe, vifijo, na mbwembwe za kila aina.
Kesho yake tarehe 25 March 2013, katika hafla iliyoandaliwa ikulu ilisainiwa mikataba 17 (KUMI NA SABA) kati ya Tanzania na China. Naomba nikiri kuwa sijawahi kuona mikataba mingi ikisainiwa kwa siku moja kati ya nchi mbili huru kabla ya hapo na hata baada ya hapo.
Katika mikataba hiyo, mmojawapo ulikuwa wa Bandari ya Bagamoyo, na Mingine hatuijui mpaka leo, na nikisema hatuijui namaanisha kwa ngazi ya wananchi walipa kodi wa Tanzania. Wachina watakuwa wanajua.
Wakati awamu ya Tano ikisitisha mkataba wa Bandari ya bagamoyo kwa sababu za masharti ya kinyonyaji hatukuambiwa kama mikataba iliyobaki 16 pia imesitishwa au inaendelea na masharti yake yalikuwa ni yapi.
Leo awamu ya sita imetuambia inarudisha Mkataba wa Bandari ya Bagamoyo, Pia hatujaambiwa ile mikatabamingine 16 inaendelea au ilisitishwa au imekufa au ipo.
Sasa ndugu zangu watanzania wakati tunajikita kwenye mkataba mmoja, ni vyema tukumbushane ile mingine 16 ilikuwa inahusu nini, utekelezaji wake ulikuaje, masharti yake pia yalikuwa yapi, na je mustakabari wake kwa taifa ni upi.
SUALA HAPA NI, tusijipumbaze na PAPA kwa sababu ndo huvuma baharini, bado kuna NYANGUMI hatumzungumzii.
Kabla ya kujikita katika mkataba mmoja SERIKALI tunaomba kwanza kufahamu ile mingine 16? hapa ndo kwenye Hoja