Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Hii ni masuala ya misconduct na Standing Orders itakuwa imeeleza vizuri mkuu, hebu ipitie, naamini wewe ni mtumishi wa Umma hivyo utakuwa unaijua hii
Mkuu asante kwa maelezo yako mazuri. Naomba kupata ufafanuzi kidogo, endapo ukiamishwa na mwajiri wako kutoka eneo moja kwenda eneo lingine ndani ya halmashauri ile ile, je nastahili kulipwa stahiki zipi?
 
Brother samahan mimi ni Hassan daudi uliyekuwa umenisaidia kipindi kile nipo songea naomba msaada wako tena kuna vitu bado vinanitatiza kwa kunikumbuka zaid nakutumia picha nilizokuwa nimevunjika
Kaka deonova habar za majukumu na pole kwa usumbufu
FB_IMG_15420284460465607.jpeg
FB_IMG_15420284673645262.jpeg
 
Muda wa kuchukua likizo hukokotolewa kwa pro rata ama unaangalia pale muda wa kuchukua likizo ulipofikia? Mimi kwa uelewa wangu kama mtumishi ameanza kazi lets say mwezi wa pili, 2017 ina maana likizo yake itaiva kwenye mwaka wa fedha unaofuata yaani 2017/2018 somewhere July kama anafuata ELRA, 2006 au September kama anafuata Public Service Regulations, 2003.
 
Kama hujapewa notis ya miezi mitatu na umeshtukizwa siku moja kabla ukapewa barua ya kuachishwa kazi inakuwaje haki za msingi mimi nimeshtukizwa hata sijapewa barua ya miezi mitatu na wamenipa hela ya miaka miwili je ni haki nikipewa hizo za mahesabu ya siku saba ya mwaka mzima?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hujapewa notis ya miezi mitatu na umeshtukizwa siku moja kabla ukapewa barua ya kuachishwa kazi inakuwaje haki za msingi mimi nimeshtukizwa hata sijapewa barua ya miezi mitatu na wamenipa hela ya miaka miwili je ni haki nikipewa hizo za mahesabu ya siku saba ya mwaka mzima?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ya kuzingatia hapa ni;

1. Je mkataba wako wa ajira umetaja kipindi cha notice period ni miezi mingapi pale ambapo upande wowote unataka kusitisha makubaliano ya mkataba? kama ni miezi mitatu kama ulivyotaja hapo juu, na ukaondolewa kazini pasina kupewa muda wa notice uliotajwa kwenye mkataba, basi mwajiri analazimika kukulipa mshahara wa muda ambao ungeendelea kuhudumia ukiwa kwenye notice period (miezi 3)........i.e payments in liue of notice

2. Umesema umedumu kazini kwa muda wa miaka miwili; basi utastahili tena kudai malipo ya kiinua mgongo ambao
unakokotolewa mshahara wa SIKU 7 kwa kila mwaka uliokamilika (Formula hii hutumika pale ambapo mkataba haujataja njia nyingine bora zaidi ya ukokotoaji wa kiinua mgongo eg. kwa asilimia/gratuity)

NB: Stahiki zako kama una mashaka nazo kwamba hazikuchanganuliwa kwa usahihi, ama umenyimwa stahiki zako; inafaa kufungua kesi ya madai ktk Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ktk kipindi kisichozidi siku 30 kuanzia tarehe uliposimamishiwa ajira yako. Aidha unaweza kuwasilisha madai yako ukisimamiwa na Wakili utakayemchagua ambaye pia atakuongoza ktk kudraft madai yako kupitia form maalumu, au unaweza kutumia Chama cha Wafanyakazi ktk kusimamia kesi yako (kama wewe ni mwanachama), vyama ninavyozungumzia hapa ni kama TALGWU, TUGHE, TUICO, CHODAWU, COTWU (T), RAAWU, TAMICO, CWT, TEWUTA, etc. Kama hukuwa mwanachama wao bado unaweza kuwatumia (ingawa utachajiwa gharama za kusimamia kesi yako maana wewe sio mwanachama wao)
 
Mkataba wangu kwanza ni wakudumu hivyo haki zangu hazijafafabuliwa sawasawa kuna kipengele kimoja kimeandika kuwa (a)mshahara wa mwajiriwa kabla ya makato ya ppf,nssf na paye havijaandikwa ni shilingi ngapi hivyo hiyo ni moja ya utapeli
(b)Na vipengele vingine ni kuhusu saa za kazi hakuna maelezo meengi kama mikataba ya kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom