Naomba hesabu ya kukokotoa kiinua mgongo

makronu306

New Member
Jan 16, 2019
4
4
Hallo wapendwa naombeni msaada namna ya ku culculate kiinua mgongo, mimi nipo kampuni binafsi kwa miaka 8 sasa, hii 2024 nmeanza wa tisa
1. Calculations ya kiinua mgongo
2. Je ukiacha kazi mwenyewe una haki ya kupata kiinua mgongo?
3.Kabla ya kuacha kazi mwenyewe kabla ya mkataba kuisha nini cha kuzingatia

Asantenii!!
 
2. Kuacha kazi mwenyewe kuna haki unazipoteza automatically ikiwepo Kiinua mgongo (Severance Pay)
Lakini pia kiinua mgongo hupatiwa mfanyakazi mwenye mkataba wa kidumu au kuanzia miaka mitatu kwa pamoja sio uwe umefanya kazi miaka 8 ila ulikuwa unapatiwa mkataba wa miezi 6 hadi inafika hiyo 8.

1. Kikokotoo cha Kiinua mgongo ni uchukue kiasi unacholipwa kwa siku zidisha siku 7 kwa mwaka mmoja yaani unalipwa 20,000×7 unachopata ni thamani ya Kiinua mgongo cha mwaka mmoja
Kwahiyo ukiwa umetimiza masharti ya kupatiwa kiinua mgongo kwa miaka 8 hiyo chukua 20,000×56=(kiinua mgongo)

3. Kabla ya kuacha kazi mwenyewe unatakiwa kujitathmini maisha yako nje ya kazi uliyofanya kwa miaka 8 mfululizo unaweza kusurvive vipi, pia tambua unasurrender haki zako ikiwepo kiinua mgongo,mshahara wa mwezi mmoja umlipe mwajiri wako (Notisi), NSSF hutopatiwa na nauli hadi ulipoajiriwa


Inatosha kwa leo, weekend njema
 
Back
Top Bottom