Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Naomba kuuliza, Kuhusiana na Swala la ugonjwa...

Nimeona Siku 63 za mwanzo----Mshahara mzima.
Siku 63 zinazofuata, Msahara nusu.

Sasa swali ni je; """Mfanyakazi huyu akiugua zaidi ya Miezi 10"" ataendelea kupokea Mshahara ama?????

Ukishamaliza mzunguka wa likizo yako ya ugonjwa kama ulivyoainisha hapo juu, na ukawa bado haujapona kuweza kuendelea na kazi, basi mwajiri anaweza kuangalia kama una likizo za aina ingine ambazo haujachukua (mfano zile annual leave za siku 28), ikiwa nazo ulishamaliza, basi ktk good practice wewe mtakaa na mwajiri wako mshauriane aidha ustaafu mapema zaid (early retirement) ama pia anaruhusiwa kusitisha ajira yako kutokana na sababu za ugonjwa (termination on medical grounds).
 
Wakuu, shukrani kwa uzii huu mujarabu.

Wadau naomba Mnisaidie kuhusu,

PESA YA LIKIZO (tofauti na mshahara wa mwezi)

a) Kwenye sekta binafsi
huwa inalipwa?
b) Kama inalipwa huwa inakokotolewaje? Kwenye (sekta binafsi)
 
TUNASHUKURU SANA KWA MAELEZO YAKO, SASA NDUGU YANGU , NISAIDIE HAPA UKO KWENYE KAMPUNI BINAFISI UNAPEWA MKATABA MFANO WA MWAKA MMOJA BAADA YA MKATABA KUISHA MWAJILI ANASEMA ATAKUPATIA MKATABA MWINGINE SIKU ZINAZIDI KWENDA MPAKA LABDA MIEZI 6 AFU ANAKUJA KUKUSIMAMISHA KAZI NA ANADAI MKATABA WAKO ULIKUWA UMEISHA JE KATIKA MAZINGIRA HAYO HAKI ZAKO NI ZIPI HAPO
 
Villky_J,
hii nimetoa kwenye nyaraka zangu ambazo nimezisave kwenye pc kwa ajili ya kazi na hizi tunaandaa kutokana na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya Mwaka 2004 na Sheria ya Taasisi za Ajira Namba 7 ya Mwaka 2004 na kutokana na maazimio mbalimbali ya ILO na miongozo ya wizara.

in short mimi hizi ndo kazi zangu za kila siku chief kama Labour Officer (Ofisa wa Kazi)
Unaptikana wapi mkuu kwa dare esalaam office yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu, naomba kujuzwa Sheria ya Kazi inavyosema kuhusiana na mambo yafuatayo:

1. Masaa ya kufanya kazi kwa juma.

2. Mfanyakazi kufungiwa nje baada ya kuchelewa kufika kazini.

3. Mfanyakazi kupangiwa kazi siku za wikendi.

Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi naomba nichangie kwa kupitia haya maswali yako

1. Masaa ya kufanya kazi kwa juma.

2. Mfanyakazi kufungiwa nje baada ya kuchelewa kufika kazini.

3. Mfanyakazi kupangiwa kazi siku za wikendi.

Tutatumia sheria zifuatazo kujadili ili sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004, kanuni za ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2007 na Minimum wage order 2013

sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 15 (1)
kinaweka wazi kwamba mkataba unatakiwa kuanisha masaa ya kufanya kazi

sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 19 (2)
kinachanganua suala la masaa ya kazi inatakiwa kwa wiki ni siku 6 na masaa 45 kwa wiki yote sasa

Sasa ikitokea muajiri anamtaka mfanyakazi aafanye kazi masaa ya ziada sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 19 (5) anatakiwa kukulipa sio chini ya 1 na nusu ya mshahara wa siku moja kwa masaa ya ziada na pia sio lazima ni makubaliano baina ya pande zote mbili

Mfanyakazi kupangiwa kazi siku za weekend mfano jumamosi na jumapili kwa jumamosi ile nusu siku tunahesabu kama siku ya kawaida ila yakivuka masaa yale ya nusu siku tunaanza kuhesabu kama ni masaa ya ziada na kwa jumapili huwa tunahesabu ni siku nzima kama kama siku ya ziada na huesabiwa masaa 8

cha kuangalia hapo je mmweweka makubaliano ya aina ipi kwenye malipo ila inategemea sana unafanya kazi ya aina gani ila ni vyema kujua iyo kazi je kisheria mshara wake wa kima cha chini sasa hapa unatumia minimum wage oder ya 2013 kujua kima cha chini cha mshara kw a sekta uliyopo

Kilimo 100,000
Afya 132,000
Mawasiliano 400,000
ulinzi kuna 150,000 na 100,000
ujenzi 250,000 mpaka 325,000
mining hapa inategemea lesseni ila ni 200,000 mpaka 400,000
elimu 140,000
sekta ya fedha 400,000


hizo ni baadhi tu itakusaidia kufahamu

Mfanyakazi kufungiwa nje baada ya kuchelewa kufika kazini. kwenye ili wapo sahihi kama tu utaratibu na sheria mlisomewa kwamba ukichelewa baada ya muda fulani wanafunga geti hili wameweka ili kupata urahisi wa mienendo mibaya ya wafanyakazi haswa swala la nidhamu kama KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI YA MWAKA 2007 inavyohitaji muajiri kukabiliana na muenendo mbaya wa mfanyakzi kwa kuweka taratatibu nasheria na kuhakikisha mfanyakzi anazijua na anazifuata na nini kitatokea zikivunjwa
 
mm naomba kufahamu juu ya hii case yangu nitaweza kusolve vipi, nilipata kazi kwenye kampuni Fulani inaendeshwa na wahindi lakini ni zaidi ya miaka miwili sijapatiwa mkataba wa kudumu na hata malipo ninayoyapata hayaendani na viwango kisheria Nina bachelor degree lakini nalipwa chini ya laki 6, mshahara naweza nisiangalie sana lakini nakosa haki za msingi mfano likizo sipati, sipo kwenye mifuko ya kijamii hata Ikitokea nafukuzwa kazi sina cha kujitetea lakini kabla ya hayo yote kutokea naomba nipate darasa nini nifanye ili miaka yangu miwili ya kuwatumikia hawa watu isipotee bure, na sio kwangu tu ninawafanyakaz wenzangu pia wanatatizo kama hili.

don't waste your time on lecturing me, this is 2020
 
Naomba msaada wakisheria please, mnapo sainishana mkataba na mwajiri najua haya nimakubaliano kati ya mwajiri najua mwajiriwa.

Kwa mfano ndani ya mkataba kuna kipengere cha Medical Insurance, ambayo inamutaka mwajiriwa achangie 3% na mwajiri nayeye achangie 3%, mwisho wa siku mwajiri anasema ameshindwa kumuhudumia mfanyakazi kwenye huduma hiyo ya Medical Insurance wakati mkataba unaonyesha kwamba mwajiri atapata matibabu kwa mjibu wa mkataba.

Je hapa sheria inasemaje baada ya mwajiri kuvunja vifungu vya mkataba..!!?

Naomba msaada tafadhali
 
Naomba kufahamu juu ya PER-DIEM hivi nikweli PER-DIEM inaondoa uharali wakulipwa masaa ya ziada yani (OVERTIME) Mwajiri wangu ananiambia kwamba kama ananilipa PER-DIEM hawezi kunilipa overtimes, kituo changu cha kazi ni DSM, ila kampuni imepata kazi huku Mbeya, hivyo nimeondoka sehemu yakituo changu kwa ajiri ya hii kazi na ninafanya masaa zaidi ya nane kila siku iendayo kwa Mungu bila kupumunzika, je nisasa kutokulipwa overtime kisa mwajiri ananipa PER-DIEM...!!?

Naomba kusaidiwa hapo tafadhali.
 
Kusimamishwa kazi bila kuchukuliwa maelezo ya awali ni sahihi kwa mjibu wa sheria za kazi...!!? Au barua yakusimamishwa kazi na kuchukuliwa maelezo kipi huanza kati ya hivyo viwili.
 
Naomba msaada wakisheria please, mnapo sainishana mkataba na mwajiri najua haya nimakubaliano kati ya mwajiri najua mwajiriwa...
Kwa mfano ndani ya mkataba kuna kipengere cha Medical Insurance, ambayo inamutaka mwajiriwa achangie 3% na mwajiri nayeye achangie 3%, mwisho wa siku mwajiri anasema ameshindwa kumuhudumia mfanyakazi kwenye huduma hiyo ya Medical Insurance wakati mkataba unaonyesha kwamba mwajiri atapata matibabu kwa mjibu wa mkataba.
Je hapa sheria inasemaje baada ya mwajiri kuvunja vifungu vya mkataba..!!?

Naomba msaada tafadhali
Mimi siyo bingwa lakini nadhani suala la medical insurance limekaa kama privilege ambazo zinatokana na collective bargaining kupitia trade union.

Sioni kama kuna room ya kumshataki na kumshinda Mwajiri kwa kushindwa ku-provide. Yaweza kuwa amefikia kipindi kigumu cha uzalishaji ambapo any prudent employer will do cost reduction.

Before the law inaweza ikawa siyo enforceable kwa kuwa employers hawabanwi kama wanavyonanwa kwenye statutory deductions such as social security, service development levy au PAYE.
 
Naomba kufahamu juu ya PER-DIEM hivi nikweli PER-DIEM inaondoa uharali wakulipwa masaa ya ziada yani (OVERTIME) Mwajiri wangu ananiambia kwamba kama ananilipa PER-DIEM hawezi kunilipa overtimes, kituo changu cha kazi ni DSM, ila kampuni imepata kazi huku Mbeya, hivyo nimeondoka sehemu yakituo changu kwa ajiri ya hii kazi na ninafanya masaa zaidi ya nane kila siku iendayo kwa Mungu bila kupumunzika, je nisasa kutokulipwa overtime kisa mwajiri ananipa PER-DIEM...!!?

Naomba kusaidiwa hapo tafadhali.
Mwajiri yuko sawa. Kama umesafiri nje ya kitu hauko entitled ku claim overtime. Kila kitu kiko covered kwenye PerDiem.

Akikulipa itakuwa ni nurgatory expenditure na anatengeneza audit query. Looks like double payment
 
Back
Top Bottom