Kutoka daily news:
Serikali ya Tanzania itapata dola zisizopungua milioni 24 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 24) katika miaka mitatu ijayo kwa kuwa bandari ya Dar es Salaam itatumika kusafirisha salfa inayopelekwa katika migodi ya shaba Zambia.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Grindrod Tanzania, Peter Buchholz, aliwaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa kampuni hiyo inasimamia usafirishaji wa salfa inayotoka Saudi Arabia kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwa njia ya reli kuipeleka Zambia kwa makubaliano na wanunuzi.
Kwa mujibu wa Buchholz, kampuni hiyo imeingia mkataba na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) kwa ajili ya kusafirisha salfa hiyo inayotumika katika mchakato wa kutengeneza shaba.
Alisema mahitaji ya salfa yamekuwa yakiongezeka Zambia na kwamba, kama miundombinu itaboreshwa, kutakuwa na ongezeko la malighafi hiyo itakayopelekwa nchini humo hivyo kuongeza mapato ya serikali kwa kuwa shaba inayozalishwa huko pia inapitishwa Tanzania kwenda maeneo mbalimbali.
Buchholz alisema hadi sasa kampuni hiyo iliyosajiliwa Agosti mwaka jana, imesafirisha tani 30,000 za salfa kwenda Zambia, na kwamba, tani 70,000 zitasafirishwa kila mwaka kwenda huko.
.....
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=9438