Tanzania kupata billion 24

Masaka

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
437
1
Kutoka daily news:

Serikali ya Tanzania itapata dola zisizopungua milioni 24 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 24) katika miaka mitatu ijayo kwa kuwa bandari ya Dar es Salaam itatumika kusafirisha salfa inayopelekwa katika migodi ya shaba Zambia.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Grindrod Tanzania, Peter Buchholz, aliwaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa kampuni hiyo inasimamia usafirishaji wa salfa inayotoka Saudi Arabia kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwa njia ya reli kuipeleka Zambia kwa makubaliano na wanunuzi.

Kwa mujibu wa Buchholz, kampuni hiyo imeingia mkataba na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) kwa ajili ya kusafirisha salfa hiyo inayotumika katika mchakato wa kutengeneza shaba.

Alisema mahitaji ya salfa yamekuwa yakiongezeka Zambia na kwamba, kama miundombinu itaboreshwa, kutakuwa na ongezeko la malighafi hiyo itakayopelekwa nchini humo hivyo kuongeza mapato ya serikali kwa kuwa shaba inayozalishwa huko pia inapitishwa Tanzania kwenda maeneo mbalimbali.

Buchholz alisema hadi sasa kampuni hiyo iliyosajiliwa Agosti mwaka jana, imesafirisha tani 30,000 za salfa kwenda Zambia, na kwamba, tani 70,000 zitasafirishwa kila mwaka kwenda huko.

.....

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=9438
 
This is ain't S H I T ! Yes I said it just like how Jasusi said it!

3 years collecting mere US $ 24m? We do not need pennies, we are rich, filthy rich, just check out the money available at BOT for Mafisadi!
 
Masaka Wewe Nadhani Ni Raia Wa Zambia Mji Wa Masaka, Ambaye Hajui Hata Nchi Inaendaje.
 
See!
Right there,a very crooked way of looking at matters.
Oh!Yes,yes...the money.Oh!How we need the money!
I haven't read anything on the report that tells us about the sustainability principles of the scheme.What are some of the tradeoffs?
Okay,forget about the tradeoffs,every action has some but, will we care to question the efficiency of the transportation means in use?
I mean,seriously,who does not know about handling techniques and requirement for the ''element'' in relation to the conditions of our railway systems?Who does not have the basic idea on the fact that some forms of sulphur can be extremely harmful to the human body?
Mbona tunafanya mambo kinyemela hivi?
Can we for once think outside the ''weighed value'' and consider the long term effects both on the economy and the environment?
Do we ever start by questioning the legitimacy of our actions?
Nooo,no ways...it's too complicated,and of course,it will take too long.
Let's reap the benefits chachap.
Well,I got news for you gentle people.
Hakuna mambo ya chapchap tena.Every step counts and every move worth consideration
 
Huyu Masaka sijui ana akili gani huy.Kila mwaka bilioni 8 tu? Halafu unaleta kanma leading story?
 
kweli siku hizi hapa watu wanacheza BORA LIENDE, badala ya kuongelea hoja watu wanamuongelea mtoa hoja !
 
hawa watu wanaoingiza mizigo ya zambia na nnchi nyengine jirani huwa wanalipishwa road tax? .......manake kutumia barabara zatu kwa mizigo yao pia iwe counted
 
Tusiruhusu cynicism itupelekeshe kiasi hiki!

Ni vigumu kujua kama bil 24 kwa kazi iliyotajwa ni nyingi au ndogo kwa sababu mwandishi wa habari hakugusia kama hiyo ni gross au net income.

Ndio hapo uone kuwa changa la macho linaanza. Iwapo wanashindwa kutoa maelezo ya kueleweka tangu mwanzo, unadhani kitafuata nini?
 
Hii mbona imekaa ki-Sinclairsinclair vile, yaani hawa jamaa wanasimamia usafirishaji wa sulphur toka bandari ya dar hadi Zambia kwa kutumia vifaa vyetu, mabehewa yetu, reli yetu, bandari yetu, labda na magodauni yetu halafu wanatupa dola milioni $24(sijui wanalipwa kiasi gani na hao wasaudia na wazambia lakini naamini ni zaidi sana tu ya hiyo dola milioni 24) kwa miaka mitatu. Hilo dili mbona wizara husika ingeweza tu tena si ajabu kwa pesa na mazingira mazuri zaidi, tukafaidika au ndio kuna vijisenti vishapenyezwa...
 
Back
Top Bottom