omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 145
Nakubaliana na Netanyahu kabisa..
Tanzania tuna priority nyingi sana za zinazotugusa maisha yetu ya kila siku kwa karibu kabisa zaidi ya kuingilia mgogoro ulioko maelfu ya kilometa mbali na nchi yetu. Sijui ni nani alietuloga watanzania tukawa na tukawa na kimbelembele kisichosaidia cha kuingilia mambo yasiyotuhusu na kuacha kushughulikia yale ya muhimu yanayotuhusu......kwenda kuandamana kuwatetea wapalestina si priority kwa nchi yetu hata kidogo....
Sijui ni kwanini Tanzania hatuwezi kujifunza kutokana na makosa sijui ni uvivu wa kufikiri au ni nini hasa kinachotusumbua. Tulipoteza resource nyingi sana kuwatetea nchi nyingine zipate uhuru hali sisi wenyewe tukiwa tumebakia masikini wa kutupwa na wale tuliokua tunawatetea wakiwa na maisha mazuri na zaidi sana wakiwa hawataki hata tukanyage katika nchi zao.
"Everybody is for himself" .Nashangaa sana bado watanzania wanakua na wema wa mshumaa (kuwamulikia wenzio huku wao wakiteketea) na kupoteza muda wao kutetea kitu ambacho hakitawasaidia wao kwa namna yeyote. By the way hao wapalestina mnaojifanya kuwatetea hawana mpango na sisi hata kidogo ndio maana hata siku moja sijasikia maandamano ya waarabu kutetea mauaji wanayofanyiwa watu weusi au matatizo ya Somalia.
I can assure you, kama ingekua ni waafrika weusi wangekua wanabutuliwa hivi sasa wapalestina wasingepoteza hata lepe la usingizi wao kuandamana kuwatetea. Lets be mature, tuache kupoteza muda kwa kujiingiza katika mambo ambayo hayatuhusu.
Pande zote mbili zikae pamoja zikubaliane. wapalestina waache uchokozi wao kwa kudhani kua ipo siku wataiondoa Israeli katika ile nchi. Watafute suluhisho la kuishi kama raia wema wakifuat asheria na kuacha uchokozi wa kurusha maroketi kwa Israeli. Kama wanaona kuishi kwa Amani na Israeli ni vigumu na kuchagua kutumia ubabe basi matokeo ya kumchokoza mbabe ndio hayo wanayoyavuna sana.
Watu wenyewe hawana nguvu alafu wanampiga Mbabe makonzi, Mbabe anapojibu mapigo kwa kuwakata mitama wanaaanza kulalamika....Oooh anatuonea, anapiga ngumi za machoni...n.k.
Lastly. Ningefurahi sana kwama watanzania tungeamka na kuwa tunafanya vitu kwa faida sit u kwa ushabiki usioleta manufaa kwa taifa. Nasikitika sana ni kwanini hatuna ubalozi wa Israeli hapa Tanzania wakati tunajua ya kwamba kama taifa tungefaidika sana kwa kupata teknolojia na utaalamu wa hali ya juu waliokua nao waisraeli.
Na huu ndio muono wako unayewaasa wengine kuwa MATURE....
Tanzanianjema