Tanzania ivunje uhusiano na Israel? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ivunje uhusiano na Israel?

Discussion in 'International Forum' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 14, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 14, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Huko nyuma tuliwahi kusema kuwa "kila mtu anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Pia tulisema kwamba kila watu wana haki ya kuwa na mahali ambapo watakuwa salama kutoka vitisho vyovyote vya utu wao na nafasi yao kama jamaa.

  Kwa sababu hiyo tuliunga mkono POLISARIO na PLO, kama vile tulivyounga mkono Biafra, kuunga mkono ANC, FRELIMO n.k Tuliamini ya kwamba hakuna mwanadamu mwingine ambaye ana haki ya kumtawala kwa nguvu mwanadamu mwingine kwa kisingizio chochote kile. Hii ilikuwa ni falsafa yetu dhidi ya ukoloni.

  Leo hii tunashuhudia yanayoendelea Palestina ambapo karibu maelfu ya watu wameshauawa. Je, Bunge linapokutana siku chache zijazo zilaani mauaji hayo? Je serikali ilaani pande zote mbili kwa kusababisha mazingira ambayo yanamnyima mwanadamu nafasi ya kuwa huru kufanya lolote? Je tuungane na nchi kama Venezuela na Bolivia ambazo zimevunja uhusiano na Israel kutokana na suala la Gaza?

  Je tukifanya hivyo hatutaulizwa uhusiano wetu na nchi kama Sudan, Somalia, Iran, n.k ambapo rekodi zao kuhusu haki za binadamu na raia si za kupewa sifa?

  Au tuendelee kukaa pembeni tu na kuwaacha "wafu wawazike wafu wao"?
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  tuvunje uhusiano upi?
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Tuvunje uhusiano upi?
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kwanini Israel aonekane ndiyo mkosaji? Hamas wanafanya poa? so long as i know, wote wanamakosa. Tunachotakiwa kufanya ni kuwa na ubalozi wa Israel, wa palestina tayari tuano.
   
 5. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  MKJJ! Kwa kumbukumbu zangu sidhani kama TZ ina uhusiano wa kibalozi na Israeli. Sasa basi hilo suala la kuvunja uhusiano halipo kwani tulishauvunja siku nyingi tangu enzi za Mwalimu. Kwa hali iliyopo sasa ni afadhali TZ ichague kukaa kimya na kuwaacha wafu wawazike wafu wao, maana angalia tumefanya nini Sudani, Somalia, au hata hapo Kongo ambao ni majirani zetu kabisa. Sembuse hao walio, masafa ya mbali ambako ni bayana kabisa kwamba hata tukisema chochote ni sawa na tone la maji baridi baharini effect yetu ni ndogo saaaaaaannnaa!!.

  Tumesikia rais ameongea kitu nadhani inatosha hatuna haja ya kuendelea mbali na mambo hayo, ila kama kuna wakimbizi wanataka kuja kwetu waje tu tutawapokea kama ada yetu na kama binadamu wengine, kitu ambacho sitarajii sana maana nani asiye penda kwenda ulaya?
   
 6. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Vipi siasa ya kutofungamana na upande wowote? What are you vunjaring? For what reason? What bad did Israel do? What good are Gazanians doing to Israel? Halooooo
   
 7. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tungeanza na Congo na Uganda kabla hatujahamia Israel
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jan 14, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hili ni tamko la Wizara yetu ya Mambo ya Nchi za Nje:

  GOVERNMENT REACTION ON GAZA STRIKE

  Date : 8-01-2009

  The United Republic of Tanzania has followed with great concern the prevailing situation in the Gaza Strip.

  Today as the hostilities heighten and destruction worsens, the Palestinians are facing the worst situation they have ever experienced. The Tuesday attack on one of the 23 United Nation Schools, killing 50 Palestinians and injuring more than 100, demonstrates that the escalation of hostilities will result in even higher civilian deaths and casualties. More than 700 Palestinians have dead and about 3000 injured since Israel raided the Gaza Strip.

  Tanzania much as it urges the end to the irresponsible provocations which has lead to this situation, strongly condemns the ongoing Israel military brutality against Palestinian people and calls for immediate halt to those attacks.

  Tanzania believes that there is no military solution to Palestine-Israel conflict, and that such actions serve only to increase tension in the region and further complicate and undermine the international efforts and initiatives that are underway to find a peaceful solution to the conflict.

  Tanzania appeals to the UN Security Council and Members of the Quartet to fully assume their responsibility to end the crisis in Gaza Strip. Furthermore, it urges the International Community to respond with prompt and generosity demanded by the desperate situation in Gaza.

  Meanwhile Jakaya Mrisho Kikwete, the President of the United Republic of Tanzania on 7th January, 2009 held talks with the Ambassador of the State of Palestine, H.E. Dr. Nasri Khalil Abu Jaish and the Ambassador of the State of Israel to Tanzania, H.E. Jakob Kdeidar on two separate occasions.

  During the talks with Israeli Ambassador, President Kikwete urged the Israel government to stop its military campaign in Gaza Strip and seek the current diplomatic initiative to engage Palestinian to reach a peaceful solution to the current crisis. While assuring Tanzania support for the right to existence of viable Palestine State living side by side with the State of Israel, the President also pleaded to the Palestinian Ambassador to pressurize Hamas to stop the provocation.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Balozi wa Israel Tanzania anakaa Kenya. Serikali ya Tanzania katika suala la uvamizi wa Gaza imechukua msimamo "neutral" kwa kulaumu "irresponsible provocations" meaning makombora yanayofyatuliwa na Hamas na "military brutality" ya Israel. Hiyo ndiyo sera yetu kwa sasa. Sidhani itapelekea kuvunjwa uhusiano na Israel. Tuko neutral.
   
 10. l

  lageneral Member

  #10
  Jan 15, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashangaa waislamu wanavyoandamana Dar kwa vifo vya wapalestina wakati waislamu weusi wa Darfur wanauwawa kwa wingi huko Sudani ya kusini.Nawataka waache double stardard
   
 11. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mada inayojadiliwa umeiona na kuielewa au umetoka 'kulala'?

  Anyways, mi naona msimamo wa serikali yetu mpaka sasa ni mzuri. Tusivunje uhusiano.
   
 12. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180

  Mwanakijiji:

  Mimi nina wazo. Kama hawa watu wanagombea ardhi tu. Basi waje Tanzania kuishi. Kuna watu wanakimbia vijiji vyao kutafuta maisha bora mijini. Wayahudi na waPalestina ni wafanyabiashara wazuri.
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Zakumi,
  Hao wabaki huko huko. Tumeshindwa kuwapa Wanyarwanda na Warundi ardhi leo tuwakaribishe Wayahudi na Wapalestina? Wabaki huko huko!
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Jasusi:

  Nilijua watu mtashtuka. Maana usafishaji wa dhahabu na ukataji wa almasi utabaki hapohapo bongo. Watu hamtaki hicho kitu. [​IMG]
   
 15. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Pengine Mkjj anataka tufungue ubalozi hapa Dar, halafu tuvunje uhusiano ! Mi nawaona Hamas ni hatari zaidi kuliko Israel.
   
 16. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ubalozi wa Israel upo mtaa gani hapa nchini?
  is it not in Kenya?
   
 17. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kama tungekuwa tuko huru sawaa. Ila si unajua kabisa tunategemea misaada na kuambiwa nini cha kufanya kutoka West! USA ikiwa mmoja wao, na unajua uhusiano wa US na Israel sasa sijui kama viongozi wetu watakuwa na ubavu wa kuongea lolote na wakati inategemea misaada kutoka kwa watu wanaoisapoti Israel. Mpaka tutakapokuwa huru (Uhuru wa kujiamulia) kama Venezuela ndio tutakuwa na ubavu wa kusema lolote.
   
 18. K

  Koba JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ....hao Hamas wangekuwa na uwezo dunia nzima tungelazimishwa kuvaa kanzu na kibaraghashia,acha wachapwe tuu maana nao nia yao ni kuwamaliza na kuwafuta Israelites ila hawana uwezo tuu,wako pale kwa agenda za extremist kama Osama na Irans hardliners,hata 2 state solution hawataki,wanachotaka kuona ni Israel amekuwa wiped out,Israel watakuwa wajinga sana kutowachapa hawa..inabidi tuanzishe uhusiano na Israel haraka sana na ikibidi tuwape mashamba Dodoma walime for 99yrs!
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Tanzania ina uhusiano wa kibalozi na Israel. Lakini kusema kuwa Tanzania ivunje uhusiano huo kutokana na watu elfu kadhaa waliokuawa itakuwa si haki. Kama ndio hivyo basi tungeanza kuvunja uhusiano na Russia iliyouwa wachechen, then US iliyoua wairaq, halafu serikali ya kagame iliyoua wahutu elfu 20 and list goes on. Watu wakimua kuuana au kushambuliana kwa sababu ya kulinda usalama wao, wanakuwa na kisingizio kizuri kwa hiyo huwezi kuwalaumu au kuvunja uhusiano nao. Ukiangalia Israel wanastahili kujilinda dhidi ya Hamas, na Hamasi wanastahili kupambana na uvamizi. Definitions za kujilinda kwa Israel zinaweza kuhusisha kushambulia, na definiion ya occupation ya Hamas ni kuwa Jirani na wayahudi. Hapo ndio mgogoro.
   
 20. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Walatini husema " Abyssus abyssum invocati" Meaning HELL INVOKES HELL.

  Hatuwezi kuvunja uhusiano nao .Ina maana Idd amini alipobreak hell bongo tukamchapa watu hawakufa? Ni nani alifikiri kutunyanyapaa. Nasi tusiwanyanyapae maana na wao sio vichaa kuwachapa HAMAS. Hamas must have invoked the hell.
   
Loading...