Tanzania itabidi tufikirie ku adopt mfumo wa Technocracy ili mambo yaende.

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Huwa napenda kukaa chini na kuangalia namna wenzetu duniani wanafanya nini, ambacho na sisi tunaweza kuiga kwa manufaa ya taifa letu.

Kuanzia February mwaka huu, nchi ya Italia imekuwa ikiongozwa na waziri mkuu mpya, anayeitwa Mario Draghi. Kwa kifupi, huyu ni nguli wa uchumi wa bara la ulaya, alikuwa ni Rais wa benki kuu ya ulaya, na anatajwa kama mtu aliyeiokoa sarafu ya Euro katika kipindi ambacho nchi za ulaya zilikuwa zinapambana na mzozo wa madeni. So huyu mwamba ni mbobezi haswa wa uchumi na bora.

Huyu jamaa amekuwa waziri mkuu wa Italia baada ya serikali iliyokuwa madarakani ya akina Mateo Renzi na Conte kushindwa kuongoza nchi kutokana na Crisis ya Covid-19.

Hawa akina Renzi, Conte na akina Belusconi, ni watu ambao ni purely politician, so zilivokuja issue za Covid19 pandemic ambayo ika trigger economic and social crisis, hawa jamaa akili zao za kuongoza ikawa zimeishia hapo.

So ilivofika kwenye mwezi wa kwanza, ilibidi serikali ijiuzulu, so Rais wa Italia akamuita nguli la uchumi Mario Draghi aunde serikali ya ki Technocrats, ambayo ni muhimu sana kwa kipindi hichi cha Covid19 economic crisis.

So Mario Draghi akaunda serikali yake February mwaka huu ambayo ilipata uungwaji mkono wa kihistoria na vyama vyote nchini Italia, kwa sababu ndo mtu ambaye anaweza kufanya mageuzi ya kiuchumi kwenye nyakati kama hizi za Crisis.

Hapa ndo nlipojifunza haswa mfumo wa Technocracy na namma unavoweza kufanya kazi hata Tanzania, tuna wasomi wazuri sana mfano mtu kama Prof. Assad, mi naamini kama Technocracy ingeapply kwa huyu mtu kwenye moja ya wizara zetu, mambo yangekuwa tofauti sana.

Na sio kwa Assad tu tuna watu wengine ni ma expert wazuri sana kwenye field zao wanaweza kuwa wanaingizwa kwenye serikali ili walete mabadiliko.

Ni hayo tu.

N.Mushi
 
Nyie na huyo pro Hassadsi huwa hamwamini katika strong people Bali ni strong institution inakuwaje tena bwashe kuwaamini mtu mmoja anaweza kuleta mapimduzi kwanza mtu mwenyewe alishindwa kwwnye taasisi Kama NSSF
 
Tatizo wabongo HUBADILISHWA na mfumo wanaoukuta au maslahi binafsi , wabongo wengi wakipata madaraka tu nao hubadilika MF: Humpley polepole na wengine

Lakini pia husifananishe Nchi tajiri kama Japan na hizi nchi zetu za ulimwengu wa tatu. Wenzetu ni matajiri wakubwa hawana tena na shida za pesa bali mabadiliko ya kushika uchumi wa Dunia huku kwetu mtu akipata madaraka tu anaiba kwa ajili yake, kisha anaanza kuiba kwa ajili ya familia yake baadae anaanza kuiba kwa ajili ya ukoo wake akimaliza anastaafu kazi kwisha hakuna kilichofanyika. ( au kutengeneza connection za watoto wao pindi wakitoka madarakani )

Wajapan karibu wote hawana shida na pesa tayari wana maisha mazuri ndio maana wapo tayari kuachia ngazi wenye uwezo wakae sisi tutafikia level hizo miaka 100 ijayo.
 
Nyie na huyo pro Hassadsi huwa hamwamini katika strong people Bali ni strong institution inakuwaje tena bwashe kuwaamini mtu mmoja anaweza kuleta mapimduzi kwanza mtu mwenyewe alishindwa kwwnye taasisi Kama NSSF

Lini Assad alikuwa nssf?
 
Sisi tuna shida ya kujenga Taifa kwanza...
Si ndo sasa turuhusu wataalamu mkuu.. mi naamini nyumba nzuri inajengwa na mafundi wazuri. So hapo lazima tuanze kutafuta mafundi wazuri kwanza kabla ya kufikiria kujenga nyumba nzuri
 
Nyie na huyo pro Hassadsi huwa hamwamini katika strong people Bali ni strong institution inakuwaje tena bwashe kuwaamini mtu mmoja anaweza kuleta mapimduzi kwanza mtu mwenyewe alishindwa kwwnye taasisi Kama NSSF
Na hauwezi kupata strong institution bila kuwa na mtu mwenye uwezo wa kuunda hiyo institution yenyewe, na hapo ndipo watu kama kina Assad wanapaswa kuanza kuingia.
 
Sisi huku tupambane kwanza kuiondoa CCM. Huyu ndiye mchawi namba moja wa maendeleo ya kiuchumi na kisiasa nchini mwetu.
 
Watanzania karibia wote ni wezi au ni wezi watarajiwa (potential thiefs). Pia kiwango cha unafiki ni cha hali ya juu sana hata humu jf angalia hoja zinavyochangiwa, wenye kuchangia objectively ni wachache mno ndio maana humu kuna watu hawaoni zuri la JPM hata moja.
 
Mkuu issue kubwa inayotusumbua wa Tz, ni kukosa mifumo imara, na taasisi zetu hazijitegemei.
Kama tungekuwa na taasisi imara basi kila kitu kingebadilika Automatically.

Ikubukwe kwa sasa tuna Vp bora kwenye masaala ya kiuchumi. Ambaye anaweza kutoa ushauri bora juu ya mienendo ya kiuchumi.
 
tuna wasomi wazuri sana mfano mtu kama Prof. Assad, mi naamini kama Technocracy ingeapply kwa huyu mtu kwenye moja ya wizara zetu,
Naye hatabiriki kuna mambo alimuunga mkono Mwendazake na kuyaponda baadaye akiwa hayupo
 
Subiri amalize angalau nusu mwaka madarakani ndio uanze kuupigia debe huo mfumo.
 
Back
Top Bottom