Tanzania inahitaji Rais Fyatu?

Tunahitaji Raisi kama China,Malaysia,India,Vietnam,Hongkong,Philippines,sio jitu linalowaza kuua wananchi kisa tu wapo upinzani,au wamelipinga
Naomba kukuuliza mambo yafuatayo, kwa uelewa wako:
1. Je China ina vyama vya upinzani?
2. Je unajua China Mainland inawafanya nn wapinzani or watu wa dini nyingine hasa waislam wa jimbo la Xianjing.?
3. Je Vietnam ina vyama vya upinzani?
4. Je Hong Kong ni inchi or ina Raisi?
5. Je unamfaham Raisi wa Philippines Rodrigo Duterte na km jibu ni ndio, Je unazijua sifa zake?

Ukishapata majibu heb rudi utafakari tena km ulichokiandika ni relevant...au ulikurupuka kuandika vitu usivyovifaham.
 
Tunahitaji Rais mwenye maono ya kuthubutu kama Obama, mbishi na mbwatukaji kama Ahmedinajad, asiyetishiwa na wawekezaji kama Hugo Chavez, mwenye kuzungukwa na watu wenye uwezo kama Lula na mwenye mvuto kwa watu wa kawaida kama Zuma. Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kidogo (au sana kutegemea na kipimo) ambaye hatopiga magoti kwa kila mtu anayejiita "mwekezaji" na ambaye hatozungukwa na wenye kuimba sifa zake.

Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kama Mrema!!!!!!
Bahati mbaya dunia haiwataki watu kama haoo... Ndo maana wanakufaa
 
Tunahitaji wananchi wenye uelewa na kufuatilia mambo, sio wanaopelekeshwa kwa propaganda na kufuatilia mambo yasiyo na tija...

Kuhusu kiongozi tunahitaji mifumo imara ambayo hata kama Kiongozi akiwa Mpuuzi (upuuzi wake uishie ikulu bila kuleta matatizo kwa Taifa)
 
Kwa matatizo tuliyonayo sasa hivi, kama kweli tunataka kufika salama tunakokwenda, kiongozi ni lazima awe na kichwa cha mwendawazimu. Hata China,USSR na leo hii Russia chini ya Putin, zilijengwa na watu ambao vichwa vyao vilikuwa vimefyatuka. Na mfano mwingine hauko mbali...ni hapa jirani Rwanda. Kagame hataki kujipendekeza kwa mtu
Uenda ukawa ulishabadilika aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
rais fyatu huyu awe na ujasiri wa kutimua na kupitia upya mikataba ya wawekezaji wanaoneemesha makwao kwa kutumia rasilimali zetu na kutuacha hohe hahe! asile meza moja na mafisadi, ambaye yuko tayari na uwezo wa kujiuliza ni kwa nini pamoja na utajiri wote tuliobarikiwa na mungu bado tumeendelea kuwa masikini, mwenye utayari wa kutoa upofu huu uliotugubika...................nani sasa?! ..........labda mm
Natamani niyaone maoni yako kwasasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunahitaji Rais mwenye maono ya kuthubutu kama Obama, mbishi na mbwatukaji kama Ahmedinajad, asiyetishiwa na wawekezaji kama Hugo Chavez, mwenye kuzungukwa na watu wenye uwezo kama Lula na mwenye mvuto kwa watu wa kawaida kama Zuma. Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kidogo (au sana kutegemea na kipimo) ambaye hatopiga magoti kwa kila mtu anayejiita "mwekezaji" na ambaye hatozungukwa na wenye kuimba sifa zake.

Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kama Mrema!!!!!!
We need strong institutions and not strong persons?
 
Kwa matatizo tuliyonayo sasa hivi, kama kweli tunataka kufika salama tunakokwenda, kiongozi ni lazima awe na kichwa cha mwendawazimu. Hata China,USSR na leo hii Russia chini ya Putin, zilijengwa na watu ambao vichwa vyao vilikuwa vimefyatuka. Na mfano mwingine hauko mbali...ni hapa jirani Rwanda. Kagame hataki kujipendekeza kwa mtu
Safi
 
Wakuu tuache kufikiria tawala za kijeshi.Mimi nadhani tupate raia mmoja tu mzalendo mwenye vision na uchungu wa kweli na maendeleo ya nchi hii.Hawa watu wapo isipokuwa bado hawajapewa nafasi au wanabaniwa au wanavurugwa na system isiyoitakia mema nchi.
Embu tuchukulie mfano tumpe urais Pombe Magufuli leo hii,hivi hatutaweza kusonga kweli?
La uliandika kama nabii,lakini nabii hana heshima kwao,kaenziwa UN,huku nyumbani na wengine wakipambana kupiga kiwi nyeusi kwenye reputation yake.
Wenye masikio tulisikia,wenye macho wakaona ndege alizonunua tangu ziyeyuke miaka kadhaa tangu enzi za Nyerere..
Mikataba ya madini kaifumua pamoja na vitisho vyote.

Corona akasema hakuna kuogopa tujifunze kuishi nayo kuishi nayo kama magonjwa mengine,akazifungulia shule na vyuo na maisha kuendelea kama kama kawaida.

wakati wazungu wakijifunza kuishi nayo ili maisha yaende,leo huku ndo tunatishwa tuogope corona badala ya kuogopa Malaria inayoua kila siku.
RIP Jiwe,ila tulikuelewa sana.
 
Ila Mwendazake alikua jabari aisee
 
We need strong institutions and not strong persons?
Hiyo strong institution iko nchi gani? Au Russia ambako Putin anajiongezea muda wa kutawala? Au China ambao wameondoa ukomo wa kuongoza rais wao?
au Marekani ambapo Trump analazimisha kujenga ukuta na ukaanza kujengwa ana kuja rais mwingine anapuuzia,au Trump pale anazuia raa wa nchi fulani wasikanyage,anaingia mwengine anaondoa hiyo marufuku.
Nieleweshe kiongozi ni nchi ipi.
 
Ni mambo ya kufikirika tu (nadharia), ukichambua undani hayapo ila kwa kuwa wanayaimba wao, sie tuna demka kwa sana tu.
 
Kweli mkuu kama rais wa nchi beberu kama USA,anakataa matokea yamechakachuliwa kuna tofauti gani na huku?
 
Back
Top Bottom