Tanzania inahitaji Rais Fyatu?

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
39,725
2,000
rais fyatu huyu awe na ujasiri wa kutimua na kupitia upya mikataba ya wawekezaji wanaoneemesha makwao kwa kutumia rasilimali zetu na kutuacha hohe hahe! asile meza moja na mafisadi, ambaye yuko tayari na uwezo wa kujiuliza ni kwa nini pamoja na utajiri wote tuliobarikiwa na mungu bado tumeendelea kuwa masikini, mwenye utayari wa kutoa upofu huu uliotugubika...................nani sasa?! ..........labda mm
10 Years later... Rais Magufuli ni raisi katili nchi haina furaha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kummmae zenu Watanzania! Uliyotaka yote ameyafanya bila kupepesa macho ila mnamuita raisi dikteta
 
Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,508
2,000
Kupanga mipango na Watanzania ni kupoteza muda

Awali kila mmoja tulikuwa tukikubaliana kwamba, Tungelipenda kupata Rais atayetupeleka mputamputa, baada ya kumpata, Sasa kila mmoja analia lia tu na huwezi kuwatambua tena iwapo walikuwa wakimaanisha kutaka mtu isiyocheka na nyani, mutu jasiri ambayo inaweza kudhibiti hata marais wastaafu na wake zao

Mtu isiyoogopa hata watu wa chama chake, mtu isiyoogopa kampuni za kidunia zilizo na mitaji mikubwa kuipita hata nchi yetu kwa makusanyo ya miaka nane

Hii inamaana, Wengi wa Wabongo ndio wanaupenda uwoga uwoga na wanapenda maisha ya starehe bila kuyatolea jasho, na ndio maana ofsi nyiingi zimejaa wapigaji, wabongo utamkuta kajenga nyumba nzuuuri ya mamilioni ya fedha, lakini pesa ya jasho lake iliyotumika hapo, Haifiki hata laki moja! zingine zoote ni za wizi!!

Sasa kama ni waoga, mlitaka Rais asiye muoga wa nini awafanyie nini sasa??

Pumbavu zenu
 
mzee74

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
10,833
2,000
Tunahitaji Rais mwenye maono ya kuthubutu kama Obama, mbishi na mbwatukaji kama Ahmedinajad, asiyetishiwa na wawekezaji kama Hugo Chavez, mwenye kuzungukwa na watu wenye uwezo kama Lula na mwenye mvuto kwa watu wa kawaida kama Zuma. Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kidogo (au sana kutegemea na kipimo) ambaye hatopiga magoti kwa kila mtu anayejiita "mwekezaji" na ambaye hatozungukwa na wenye kuimba sifa zake.

Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kama Mrema!!!!!!
Fyatu ni mwenye wazimu ama?

Je Dkt.Mrema ana wazimu??Tuanzie hapo
 
triumvirate

JF-Expert Member
May 4, 2021
207
500
rais fyatu huyu awe na ujasiri wa kutimua na kupitia upya mikataba ya wawekezaji wanaoneemesha makwao kwa kutumia rasilimali zetu na kutuacha hohe hahe! asile meza moja na mafisadi, ambaye yuko tayari na uwezo wa kujiuliza ni kwa nini pamoja na utajiri wote tuliobarikiwa na mungu bado tumeendelea kuwa masikini, mwenye utayari wa kutoa upofu huu uliotugubika...................nani sasa?! ..........labda mm
Mungu alijibu maombi yenu afu mkaanza harakati feki tena kumwita dikteta
 
triumvirate

JF-Expert Member
May 4, 2021
207
500
10 Years later... Rais Magufuli ni raisi katili nchi haina furaha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kummmae zenu Watanzania! Uliyotaka yote ameyafanya bila kupepesa macho ila mnamuita raisi dikteta
Kuna yule bibi kikongwe wa twita yeye yuko kwenye rekodi kabisa ya video akihojiwa enzi za Kikwete akisema Tz inahitaji rais wa namna hiyo halafu baadae kikaanza harakati za kumuita dikteta.
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
3,297
2,000
Tunahitaji Rais mwenye maono ya kuthubutu kama Obama, mbishi na mbwatukaji kama Ahmedinajad, asiyetishiwa na wawekezaji kama Hugo Chavez, mwenye kuzungukwa na watu wenye uwezo kama Lula na mwenye mvuto kwa watu wa kawaida kama Zuma. Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kidogo (au sana kutegemea na kipimo) ambaye hatopiga magoti kwa kila mtu anayejiita "mwekezaji" na ambaye hatozungukwa na wenye kuimba sifa zake.

Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kama Mrema!!!!!!
Tunahitaji Raisi kama China,Malaysia,India,Vietnam,Hongkong,Philippines,sio jitu linalowaza kuua wananchi kisa tu wapo upinzani,au wamelipinga
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom