BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Kati ya Juni hadi Septemba 2023, kulikuwa na Vifaa 70,613,504 vya Mawasiliano ya Simu za Kawaida (Feature Phone) na Simu Janja (Smart Phone) zilizounganishwa na Mitandao ya Simu sawa na 83% ambapo Simu Janja zilikuwa Milioni 18.9 na Simu za Kawaida za Mkononi (Feature Phone) zilikuwa Milioni 51.6.
Ripoti ya Huduma za Mawasiliano iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeonesha hadi kufikia mwishoni mwaka Septemba, kulikuwa na Vifaa vya Mkononi vilivyounganishwa na Huduma za Mawasiliano 1,698,654, Modem 562,325 na vinginevyo 838,817.
Simu za Kawaida (Feature Phone) zimechukua zaidi ya 70% ya Vifaa vilivyounganishwa na Mawasiliano huku Simu Janja (Smart Phone) zikichukua nafasi ya pili kwa 25.72%