Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

Nchi imepoteza mno kwenye sakata la Makanikia [ Fedha za kigeni $200M na TZS 430B Mapato ya Serikali]

  • mwaka 2016 Tanzania iliuza nje dhahabu iliyoingiza USD 1.8 bilioni
  • Mwaka wa Makanikia 2017 mauzo nje yalishuka mpaka USD 1.6 bilioni na;
  • Mwaka 2018, mwaka ambao athari ya Makanikia ilikuwa mwaka mzima mauzo nje yalikuwa USD 1.4 bilioni

Kati ya mwaka 2017-2018 Mauzo nje ya dhahabu yalishuka kwa jumla ya $200M saw na 11%.

Katika kipindi hicho uzalishaji wa dhahabu ulishuka kutoka tani 43 za dhahabu mwaka 2015 mpaka tani 39 mwaka 2018. Uzalishaji wa mwaka 2018 ulikuwa sawa na uzalishaji wa mwaka 2010.

Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka katika kipindi cha Makanikia. Kwa mujibu wa Kitabu cha Mapato ya Serikali kwa Wabunge ( Revenues Book Vol. 1 ).

  • mwaka 2016/17 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 341 bilioni
  • Mwaka 2017/18 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 230 bilioni
  • Mwaka 2018/19 makusanyo yalikuwa TZS 220 bilioni.
Serikali imekadiria kukusanya TZS 350 bilioni mwaka 2019/2020.

Kwa mujibu wa Dkt. Genuine Martin kwenye mada yake kwa Policy Forum Breakfast Debate Julai, 2019 Mapato yote ya sekta ya Madini yameshuka kwa 32% katika zama za Makanikia.

  • mwaka 2016 Mapato yalikuwa TZS 1.3 trilioni
  • Mwaka 2018 Mapato yalikuwa TZS 867 bilioni.
Katika Miaka 2 Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka kwa TZS 430 bilioni.

Tunapata nini kutoka Barrick Gold baada ya sakata la Makanikia?

Mapato ambayo Serikali ya Magufuli imepoteza kwenye sekta ya Madini kati ya mwaka 2017 - 2019 ni makubwa zaidi ya malipo* ambayo Serikali inasema tutalipwa na Barrick Gold Corporation ili kumaliza mgogoro baina ya Kampuni ya Acacia na Serikali.

Tumeona hapo juu kuwa tumepoteza Mapato ya Fedha za kigeni $200M na Mapato ya Serikali kushuka kwa TZS 430 bilioni. Kutoka Barrick tunatarajiwa kupata $300M ambazo chache kulinganisha na kiasi tulichopeteza.

* Malipo yenyewe hayo ya $300M kwanza yatalipwa kwa miaka 7, pili yana masharti ya wao kulipwa kwanza Fedha zao za VAT ( $240M ), na tatu watasamehewa Kodi ya Capital Gains Tax ya mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick Gold ($85.6M). Hatimaye Tanzania ndio itakuwa imeilipa Barrick $25M ( Net of payments and receipts to and from Barrick Gold ).

Kwa hiyo Tanzania imepoteza Mapato iliyokuwa yakusanywe kama mgogoro usingekuwepo [ $200M exports revenues and $170M tax revenues ] na imeishia kuilipa Barrick badala ya yenyewe kulipwa.

Tumepata hasara kubwa sana kutokana na maamuzi yetu wenyewe, maamuzi ambayo hayakuzingatia maslahi ya nchi yetu. Tunapaswa kuwawajibisha waliotupa hasara hiyo.
Mh. Zitto unafiki wako umefanya watu wengi wasikuelewe hata kama wakati fulani unaleta hoja za maana.
Ninaomba utusaidie hiyo taarifa mliyopewa nyie waheshimiwa wabunge ili nasi tuisome kama inawezekana
 
Rais Magufuli huwa anasema kupanga ni kuchagua. Tuchague kuendelea kuibiwa rasilimali zetu au tuziache kwanza hadi hapo tutakapoona tunafaidika vipi. Zitto ni kipaza sauti cha mabeberu na hana hata soni kusema kwamba kuzuia makinikia tumepoteza zaidi, yaani watu wasafirishe mchanga wenye madini mbalimbali kwa ujanja ujanja useme kuwazuia tumepoteza stupid!!!
 
Kilichofanya ufikie hitimisho hilo Nini!? Kwani swala hili limeshaisha!? Mimi nadhani alipaswq kusubiri hadi pale tutakapoambiwa swala limeisha na yale watakayokubaliana yaanze kutekelezwa ndio hapo tinaweza kusema kama njia zilikuwa sahihi au si sahihi. Tatizo lako na wewe na Zitto mnataka kila mtu arifikirie na kutenda kama mnavyofikiria nyie. Kwa ufupi nyie ni wabinafsi!

Amesema mapema ili mkose la kusema baadae mambo yatakokuwa mabaya mkose la kusema kuhusu ujinga uliofanyika zitto ye atakachofanya ni kukutag tu thread ya leo basi mana mtaanza sema ooh we ulikua wp mbona ukusema hapo ndo technologia itakapomaliza mambo na anafanya hivi kwa manufaa yetu ili kama serikali hii inajitambua itajilekebisha mana ipo sana humu mitandaoni we uliechagua upande wa kusifia kila kitu ndo mbaya sana baadae
 
Kama una akiri timamu kwenye comment zangu nimebainisha wazi kuwa kujaribu/kuleta changes kwenye mining industry Tanzania hakuna namna negative effects zilikuwa zinazuilika na it's something ambacho mtu yeyote mwenye angalau elimu ya Darasa la Saba alipaswa kukitegemea. Sembuse Zitto na "Masters yake sijui ya Ecomomics"!!!
Kweli Rais wetu amezungukwa na wapumbavu
 
Yes, kwa mtazamo wako, ambao siyo lazima kila mtu aone hivo. Tatizo bro wewe ni mbinafisi, unaamini una akiri Sana, hivyo unataka kila mtu afikirie na kuona kama unavyoona wewe.

Mkuu we ndo wale watu baadae wanaosema wabunge wanakula hela bure tu awafanyi chochote kila mtu ana haki ya kusema kile kilicho sahihi sasa je hao unaowasifia wanafanya mazuri na wanaakili zaidi ya wengine
 
Amesema mapema ili mkose la kusema baadae mambo yatakokuwa mabaya mkose la kusema kuhusu ujinga uliofanyika zitto ye atakachofanya ni kukutag tu thread ya leo basi mana mtaanza sema ooh we ulikua wp mbona ukusema hapo ndo technologia itakapomaliza mambo na anafanya hivi kwa manufaa yetu ili kama serikali hii inajitambua itajilekebisha mana ipo sana humu mitandaoni we uliechagua upande wa kusifia kila kitu ndo mbaya sana baadae
Nisome vizuri Bingwa, nimesema kabisa alichokifanya JPM kwenye Mining Industry kifanikiwe au kisifanikiwe kwangu siyo issue. Ukweli ni kwamba Watanzania akiwemo Zitto tunakubaliana sekita ya Madini ina mambo ya ovyo, so mtu anayejaribu kuleta changes nitamuunga mkono bila kujali ni Nani, kama tulivyomuunga mkono Zitto wakati huo akitoa povu kuhusu Madini kabla hajawa corrupted. It is better to die trying kuliko kukaa tu wakati unaona huridhishwi na mambo yalivyo.
 
Mkuu achana na huyo muha,
Hawa jamaa wa kigoma(sio wote) anaweza kuwa shabiji wa manchester na kavaa jezi kabisa ya man u. but akiingia kwenye eneo ambapo akakuta hakuna mpinzani wa man u basi gafla anakuwa upande wa timu nyingine ilimradi aanzishe varangati la ubishi...hawa ndo akina zitto.
Sasa wewe tumia mstari mmoja kutuainishia faida tuliyoipata kupitia ripoti ya Mruma na Osoro.

Weka 'digit' zinazo represent faida tuliyopata.
 
Nchi imepoteza mno kwenye sakata la Makanikia [ Fedha za kigeni $200M na TZS 430B Mapato ya Serikali]

  • mwaka 2016 Tanzania iliuza nje dhahabu iliyoingiza USD 1.8 bilioni
  • Mwaka wa Makanikia 2017 mauzo nje yalishuka mpaka USD 1.6 bilioni na;
  • Mwaka 2018, mwaka ambao athari ya Makanikia ilikuwa mwaka mzima mauzo nje yalikuwa USD 1.4 bilioni

Kati ya mwaka 2017-2018 Mauzo nje ya dhahabu yalishuka kwa jumla ya $200M saw na 11%.

Katika kipindi hicho uzalishaji wa dhahabu ulishuka kutoka tani 43 za dhahabu mwaka 2015 mpaka tani 39 mwaka 2018. Uzalishaji wa mwaka 2018 ulikuwa sawa na uzalishaji wa mwaka 2010.

Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka katika kipindi cha Makanikia. Kwa mujibu wa Kitabu cha Mapato ya Serikali kwa Wabunge ( Revenues Book Vol. 1 ).

  • mwaka 2016/17 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 341 bilioni
  • Mwaka 2017/18 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 230 bilioni
  • Mwaka 2018/19 makusanyo yalikuwa TZS 220 bilioni.
Serikali imekadiria kukusanya TZS 350 bilioni mwaka 2019/2020.

Kwa mujibu wa Dkt. Genuine Martin kwenye mada yake kwa Policy Forum Breakfast Debate Julai, 2019 Mapato yote ya sekta ya Madini yameshuka kwa 32% katika zama za Makanikia.

  • mwaka 2016 Mapato yalikuwa TZS 1.3 trilioni
  • Mwaka 2018 Mapato yalikuwa TZS 867 bilioni.
Katika Miaka 2 Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka kwa TZS 430 bilioni.

Tunapata nini kutoka Barrick Gold baada ya sakata la Makanikia?

Mapato ambayo Serikali ya Magufuli imepoteza kwenye sekta ya Madini kati ya mwaka 2017 - 2019 ni makubwa zaidi ya malipo* ambayo Serikali inasema tutalipwa na Barrick Gold Corporation ili kumaliza mgogoro baina ya Kampuni ya Acacia na Serikali.

Tumeona hapo juu kuwa tumepoteza Mapato ya Fedha za kigeni $200M na Mapato ya Serikali kushuka kwa TZS 430 bilioni. Kutoka Barrick tunatarajiwa kupata $300M ambazo chache kulinganisha na kiasi tulichopeteza.

* Malipo yenyewe hayo ya $300M kwanza yatalipwa kwa miaka 7, pili yana masharti ya wao kulipwa kwanza Fedha zao za VAT ( $240M ), na tatu watasamehewa Kodi ya Capital Gains Tax ya mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick Gold ($85.6M). Hatimaye Tanzania ndio itakuwa imeilipa Barrick $25M ( Net of payments and receipts to and from Barrick Gold ).

Kwa hiyo Tanzania imepoteza Mapato iliyokuwa yakusanywe kama mgogoro usingekuwepo [ $200M exports revenues and $170M tax revenues ] na imeishia kuilipa Barrick badala ya yenyewe kulipwa.

Tumepata hasara kubwa sana kutokana na maamuzi yetu wenyewe, maamuzi ambayo hayakuzingatia maslahi ya nchi yetu. Tunapaswa kuwawajibisha waliotupa hasara hiyo.

Unaweza pia kutufafanulia mapato yatakayopatikana baada ya kuongezewa hiyo 16% shareholding in the long run? Life is about giving and taking. Ni bahari peke yake inayopokea maji tu bila kuyapeleka sehemu nyingine rasmi at least...
 
Huyu member alitimiza wajibu wake vizuri sana.

Kuwapa moyo kina kabudi ili watumie brain kuhakikisha tunapata faida. Hongera Pascal Mayalla.

Kinachotuudhi ni kwamba pamoja na uungwaji mkono (uliokuwa na lengo la kuweka tranquility atmospheric balance) kina Osoro, Mruma na Kabudi wametusababishia hasara kubwa (kwa mujibu wa takwimu za Zitto ambazo tuna kila sababu ya kuziamini)
 
Dont forget Evaporation effects.
 
Hata mimi namshangaaga huyu jamaa (Zitto)..ila kitu kimoja tunachofanana mimi na WEWE ni kwamba tunakosa FACTS za kujibu the so called LIES zake na hatimaye tunabakia kumshambulia na kumtuhumu ni KIBARAKA. Naomba tujitahidi kucounter facts zake ili tumuweke sawa aache the so called political stunts. Nakuomba saana nisaidie kutafuta facts tumuumbue la sivyo JF watatushambulia kwa PERSONALTY ATTACK and not FACTS.

Tafadhalii.
Bravo..!
 
Huyu member alitimiza wajibu wake vizuri sana.

Kuwapa moyo kina kabudi ili watumie brain kuhakikisha tunapata faida. Hongera Pascal Mayalla.

Kinachotuudhi ni kwamba pamoja na uungwaji mkono (uliokuwa na lengo la kuweka tranquility atmospheric balance) kina Osoro, Mruma na Kabudi wametusababishia hasara kubwa (kwa mujibu wa takwimu za Zitto ambazo tuna kila sababu ya kuziamini)
Upo sawa na kiukweli Kuhusu makinikia japo kwauchache tongotongo alinitoa Pascal Mayalla ndiomana najaribu kumcheck kila nikiona uzi unaohusu makinikia kama ana chochote anaweza kuongea
 
Inawezekana aliyoyaongea Musiba kuhusu haka kajamaa jana ni ya kweli.
Yaani miaka yote tangu 2008 wewe umekuwa mbele kupiga kelele juu ya wizi unaofanywa na Migodi ya Madini.

Leo ametokea mtu amejaribu kuweka mambo sawa unapiga kelele tena. Haijalishi Kama amefanikiwa au laa, lakini atleast amejaribu kupambana na kile ambacho Watanzania wengi wamekuwa wakikipigia kelele ukiwemo wewe.
Kiufupi wewe ni tapeli wa kisiasa you do things just for political stunts. Hufanyi kwa maslahi ya Taifa bali kujipatia umaarufu binafsi. The good thing JPM ameweka a benchmark ya aina ya watu wanaopaswa kuwa Marais wa Nchi hii, hadhi ya Urais ameiweka kwenye standard ya juu sana na kutufumbua macho juu ya watu wa aina yako ambao kimsingi hamna chochote ila siasa za ulaghai ziliwafanya mfike hapo mlipo.
Mnapambana kuona JPM aonekane ameshindwa ili muendelee kuonekana nanyi mnasifa za kuwa Marais, kwani akifanikiwa of which is about to hadhi ya Urais itapanda sana na you will automatically be disqualified kwani Watanzania wataanza kufikiria aina ya watu wenye vinasaba kama vyake of which nyie Pro-JK mnavikosa.
Mkuu asanate sana. Maneno yako ni kama dhahabu na yamejaa ukweli. Shida ya hawa watu ni kuwa wanaona standard za kupata urais zinazidi kuwa juu na uwezekano wa wao kupotea kwenye ulingo wa siasa ni mkubwa. BTW hiyo anayosema kuwa tumepoteza siyo kweli. Mtu ukiwa na mali isiyoharibika na ukakataa kuiuza unakuwa hujapoteza bali ni kama akiba. Ni bora tusipate pato lolote sasa hivi mpaka hapo mambo yatakapowekwa vizuri. Kuendelea kuuza ili tu kuingiza pato bila kuangalia thamani ya unachouza ni uendawazimu.
 
Kama yameshuka inamaana hayajachimbwa na nikama hayajachimbwa bado yapo kwenye aridhi ya Tanzania na nikama bado yapo yatachimbwa badae na mapato yataongezeka kuliko mapato yawe juuu kwa kuwa na unequal exchange
 
Back
Top Bottom