Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

Nchi imepoteza mno kwenye sakata la Makanikia [ Fedha za kigeni $200M na TZS 430B Mapato ya Serikali]
  • mwaka 2016 Tanzania iliuza nje dhahabu iliyoingiza USD 1.8 bilioni
  • Mwaka wa Makanikia 2017 mauzo nje yalishuka mpaka USD 1.6 bilioni na;
  • Mwaka 2018, mwaka ambao athari ya Makanikia ilikuwa mwaka mzima mauzo nje yalikuwa USD 1.4 bilioni
Kati ya mwaka 2017-2018 Mauzo nje ya dhahabu yalishuka kwa jumla ya $200M saw na 11%.
Katika kipindi hicho uzalishaji wa dhahabu ulishuka kutoka tani 43 za dhahabu mwaka 2015 mpaka tani 39 mwaka 2018. Uzalishaji wa mwaka 2018 ulikuwa sawa na uzalishaji wa mwaka 2010.
Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka katika kipindi cha Makanikia. Kwa mujibu wa Kitabu cha Mapato ya Serikali kwa Wabunge ( Revenues Book Vol. 1 ).
  • mwaka 2016/17 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 341 bilioni
  • Mwaka 2017/18 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 230 bilioni
  • Mwaka 2018/19 makusanyo yalikuwa TZS 220 bilioni.
Serikali imekadiria kukusanya TZS 350 bilioni mwaka 2019/2020.
Kwa mujibu wa Dkt. Genuine Martin kwenye mada yake kwa Policy Forum Breakfast Debate Julai, 2019 Mapato yote ya sekta ya Madini yameshuka kwa 32% katika zama za Makanikia.
  • mwaka 2016 Mapato yalikuwa TZS 1.3 trilioni
  • Mwaka 2018 Mapato yalikuwa TZS 867 bilioni.
Katika Miaka 2 Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka kwa TZS 430 bilioni.
Tunapata nini kutoka Barrick Gold baada ya sakata la Makanikia?
Mapato ambayo Serikali ya Magufuli imepoteza kwenye sekta ya Madini kati ya mwaka 2017 - 2019 ni makubwa zaidi ya malipo* ambayo Serikali inasema tutalipwa na Barrick Gold Corporation ili kumaliza mgogoro baina ya Kampuni ya Acacia na Serikali.
Tumeona hapo juu kuwa tumepoteza Mapato ya Fedha za kigeni $200M na Mapato ya Serikali kushuka kwa TZS 430 bilioni. Kutoka Barrick tunatarajiwa kupata $300M ambazo chache kulinganisha na kiasi tulichopeteza.
* Malipo yenyewe hayo ya $300M kwanza yatalipwa kwa miaka 7, pili yana masharti ya wao kulipwa kwanza Fedha zao za VAT ( $240M ), na tatu watasamehewa Kodi ya Capital Gains Tax ya mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick Gold ($85.6M). Hatimaye Tanzania ndio itakuwa imeilipa Barrick $25M ( Net of payments and receipts to and from Barrick Gold ).
Kwa hiyo Tanzania imepoteza Mapato iliyokuwa yakusanywe kama mgogoro usingekuwepo [ $200M exports revenues and $170M tax revenues ] na imeishia kuilipa Barrick badala ya yenyewe kulipwa.
Tumepata hasara kubwa sana kutokana na maamuzi yetu wenyewe, maamuzi ambayo hayakuzingatia maslahi ya nchi yetu. Tunapaswa kuwawajibisha waliotupa hasara hiyo.
Hivi ni maamuzi yetu au maamuzi ya malaika mmoja ambaye sina hakika kama ni malaika wa Mungu au waShetan,wanaomjua vizuri mtanisaidia
 
Hii nchi siasa zake sijui nani aliziasisi, wakati yanafanyika mabadiliko ya sheria ya madini kwa nia njema kabisa, wengine walikomaa kuponda tena bila hata adabu na staha!

Ilikuwa kama vile bora tubakie na sheria ile ya zamani! Sasa hivi wapingaji wale wale wanaitumia sheria ile ile waliyoipinga kuisema serikali kuwa inakiuka sheria mpya ya madini!

Kuna watu wanaweza kabisa kumfanya malaika aonekane shetani na shetani aonekane malaika. Huoni wakati gani wanakubaliana na serikali kwenye mambo ya msingi na wakati gani wanapinga.

Siasa za fitna, kukwamishana n.k hizi mambo zilianzia wakati wa harakati za uchaguzi wa 1995 na zinatutafuna hadi leo. Hoja inajengwa kwa kutegemea upande uliopo na si maslahi ya Taifa.
 
Mkuu pointi yangu ni kwamba Zitto alikuwa mmoja Kati ya watu waliolalamikia sana swala la Madini. Sasa amekuja mtu anajaribu kurekebisha, na kama alitaka kurekebisha anadhani ingekuwa rahisi, andhani katika kipindi cha marekebisho isingetokea standout, Zotto kama msomi alitegemea zifanyike changes bila kuathiri shughuli za uzalishaji.
Ndio maana nakwambia huyu jamaa amekuwa akitumia umbumbu wa watu kudanganya. Juzi ameleta uongo huju watu wakamuumbua Leo kaja na uongo mwingine.

Umeambiwa toa facts; sio sweeping statements. Nawe njoo na takwimu zinazopingana na hizo za Zitto ili umuumbue.
 
Zito ni mchumia tumbo

Mmi namshauri zito siki zingine nae tunataka tuone kaja na uzi wenye faida, kwamba jambo flani limefanyika na lina faida kwa inchi ndi uzalendo wake utakuwa sawa, ila kama kila siku anatafuta ubaya tu kwani hakuna hata zuri lililofanyika?
Ninachojua makinikia bado yapo, labda aseme kama nayo yameoza kwa hiyo hayana thamani ndo tutajua kuna hasara.

Lakini kama yapo yakiuzwa hiyo pesa kwa miaka yote hiyo itajifidia na kuwa na faida kubwa zaidi.

Mkuu pointi yangu ni kwamba Zitto alikuwa mmoja Kati ya watu waliolalamikia sana swala la Madini. Sasa amekuja mtu anajaribu kurekebisha, na kama alitaka kurekebisha anadhani ingekuwa rahisi, andhani katika kipindi cha marekebisho isingetokea standout, Zotto kama msomi alitegemea zifanyike changes bila kuathiri shughuli za uzalishaji.
Ndio maana nakwambia huyu jamaa amekuwa akitumia umbumbu wa watu kudanganya. Juzi ameleta uongo huju watu wakamuumbua Leo kaja na uongo mwingine.
 
Hii nchi siasa zake sijui nani aliziasisi, wakati yanafanyika mabadiliko ya sheria ya madini kwa nia njema kabisa, wengine walikomaa kuponda tena bila hata adabu na staha!

Ilikuwa kama vile bora tubakie na sheria ile ya zamani! Sasa hivi wapingaji wale wale wanaitumia sheria ile ile waliyoipinga kuisema serikali kuwa inakiuka sheria mpya ya madini!

Kuna watu wanaweza kabisa kumfanya malaika aonekane shetani na shetani aonekane malaika. Huoni wakati gani wanakubaliana na serikali kwenye mambo ya msingi na wakati gani wanapinga.

Siasa za fitna, kukwamishana n.k hizi mambo zilianzia wakati wa harakati za uchaguzi wa 1995 na zinatutafuna hadi leo. Hoja inajengwa kwa kutegemea upande uliopo na si maslahi ya Taifa.

Fair enough kwa ulichokiandika; lakini sheria iliyopingwa ILIPITISHWA na ndio inayotumika. Kwa mantiki hiyo isipotekelezwa watu wanapaswa kulisemea hilo. Au unataka sheria ya zamani ndio itumike?
 
Umeambiwa toa facts; sio sweeping statements. Nawe njoo na takwimu zinazopingana na hizo za Zitto ili umuumbue.
Ambacho huelewi nini kwa mfano?!. Zitto wakati anatoa povu kuhusu sekita ya Madini alichokuwa anataka si mabadiliko!? Kama ni mabadiliko unadhani yangeweza kufanyika bila kuleta athari yoyote kwenye shughuli za Madini!? It is obvious alikuwa anajua hilo, sasa anapoleta tena huu upuuzi hapa sisi tumueleweje.

Yaani huyu ni sawa na mtoto anamlilia mzazi ampeleke shule, halafu mzazi anauza shamba ili ampeleke shule, halafu huyo huyo mtoto anarudi kumlaumu mzazi eti kwanini ameuza shamba.
 
Nchi imepoteza mno kwenye sakata la Makanikia [ Fedha za kigeni $200M na TZS 430B Mapato ya Serikali]

  • mwaka 2016 Tanzania iliuza nje dhahabu iliyoingiza USD 1.8 bilioni
  • Mwaka wa Makanikia 2017 mauzo nje yalishuka mpaka USD 1.6 bilioni na;
  • Mwaka 2018, mwaka ambao athari ya Makanikia ilikuwa mwaka mzima mauzo nje yalikuwa USD 1.4 bilioni

Kati ya mwaka 2017-2018 Mauzo nje ya dhahabu yalishuka kwa jumla ya $200M saw na 11%.

Katika kipindi hicho uzalishaji wa dhahabu ulishuka kutoka tani 43 za dhahabu mwaka 2015 mpaka tani 39 mwaka 2018. Uzalishaji wa mwaka 2018 ulikuwa sawa na uzalishaji wa mwaka 2010.

Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka katika kipindi cha Makanikia. Kwa mujibu wa Kitabu cha Mapato ya Serikali kwa Wabunge ( Revenues Book Vol. 1 ).

  • mwaka 2016/17 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 341 bilioni
  • Mwaka 2017/18 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 230 bilioni
  • Mwaka 2018/19 makusanyo yalikuwa TZS 220 bilioni.
Serikali imekadiria kukusanya TZS 350 bilioni mwaka 2019/2020.

Kwa mujibu wa Dkt. Genuine Martin kwenye mada yake kwa Policy Forum Breakfast Debate Julai, 2019 Mapato yote ya sekta ya Madini yameshuka kwa 32% katika zama za Makanikia.

  • mwaka 2016 Mapato yalikuwa TZS 1.3 trilioni
  • Mwaka 2018 Mapato yalikuwa TZS 867 bilioni.
Katika Miaka 2 Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka kwa TZS 430 bilioni.

Tunapata nini kutoka Barrick Gold baada ya sakata la Makanikia?

Mapato ambayo Serikali ya Magufuli imepoteza kwenye sekta ya Madini kati ya mwaka 2017 - 2019 ni makubwa zaidi ya malipo* ambayo Serikali inasema tutalipwa na Barrick Gold Corporation ili kumaliza mgogoro baina ya Kampuni ya Acacia na Serikali.

Tumeona hapo juu kuwa tumepoteza Mapato ya Fedha za kigeni $200M na Mapato ya Serikali kushuka kwa TZS 430 bilioni. Kutoka Barrick tunatarajiwa kupata $300M ambazo chache kulinganisha na kiasi tulichopeteza.

* Malipo yenyewe hayo ya $300M kwanza yatalipwa kwa miaka 7, pili yana masharti ya wao kulipwa kwanza Fedha zao za VAT ( $240M ), na tatu watasamehewa Kodi ya Capital Gains Tax ya mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick Gold ($85.6M). Hatimaye Tanzania ndio itakuwa imeilipa Barrick $25M ( Net of payments and receipts to and from Barrick Gold ).

Kwa hiyo Tanzania imepoteza Mapato iliyokuwa yakusanywe kama mgogoro usingekuwepo [ $200M exports revenues and $170M tax revenues ] na imeishia kuilipa Barrick badala ya yenyewe kulipwa.

Tumepata hasara kubwa sana kutokana na maamuzi yetu wenyewe, maamuzi ambayo hayakuzingatia maslahi ya nchi yetu. Tunapaswa kuwawajibisha waliotupa hasara hiyo.
huu ni uhujumu wa uchumi uliokithiri!

Rais ajaye itabidi awe na action plan kama ifuatavyo:

Nov 2020 - March 2021:
upanuzi wa magereza yaliyopo na kuongeza mapya kadhaa

April - July 2021:
fasttracked cases za wahujumu uchumi na mafisadi wote wa awamu zilizotangulia. kwa hali ilivyo, kutakuwa na mamia (kama si maelfu) watakaoswekwa gerezani

August - September 2021:
kutaifisha mali za wahalifu zote

action plan ya namna hii ita set positive precedence ya kuondoa power abuse inayofanywa na watu wanaoaminiwa kupewa dhamana ya kutuongoza!
 
Inawezekana aliyoyaongea Musiba kuhusu haka kajamaa jana ni ya kweli.
Yaani miaka yote tangu 2008 wewe umekuwa mbele kupiga kelele juu ya wizi unaofanywa na Migodi ya Madini.

Leo ametokea mtu amejaribu kuweka mambo sawa unapiga kelele tena. Haijalishi Kama amefanikiwa au laa, lakini atleast amejaribu kupambana na kile ambacho Watanzania wengi wamekuwa wakikipigia kelele ukiwemo wewe.
Kiufupi wewe ni tapeli wa kisiasa you do things just for political stunts. Hufanyi kwa maslahi ya Taifa bali kujipatia umaarufu binafsi. The good thing JPM ameweka a benchmark ya aina ya watu wanaopaswa kuwa Marais wa Nchi hii, hadhi ya Urais ameiweka kwenye standard ya juu sana na kutufumbua macho juu ya watu wa aina yako ambao kimsingi hamna chochote ila siasa za ulaghai ziliwafanya mfike hapo mlipo.
Mnapambana kuona JPM aonekane ameshindwa ili muendelee kuonekana nanyi mnasifa za kuwa Marais, kwani akifanikiwa of which is about to hadhi ya Urais itapanda sana na you will automatically be disqualified kwani Watanzania wataanza kufikiria aina ya watu wenye vinasaba kama vyake of which nyie Pro-JK mnavikosa.
Tusaidie angalau jambo moja liliowekwa sawa in 4 years?Akili ndogo na mpumbavu wa Lumumba,Zito anasema hivi,kama ulithani Malaika anaweka mambo sawa,unajidanganya.yaani huyu malaika anafanya mambo yawe mabaya zaidi,kwani hata kile kidogo tulichokuwa tunapata after wezi sasa hatukipati tena
 
Back
Top Bottom